Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako amesema Serikali inatarajia
kuanza ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) cha Mkoa wa Simiyu
kuanzia mwezi Machi, 2018.
Waziri
Ndalichako ameyasema hayo leo wakati
alipokuwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake ya
siku moja Mkoani humo.
“Kesho tarehe
28/12/2017 kwenye magazeti kutatoka tangazo la zabuni ya ujenzi wa VETA ya Mkoa
wa Simiyu na tunategemea kujenga VETA ya Kisasa itakayohudumia Mkoa na
inayoendana na mahitaji ya sasa; tukitangaza zabuni kesho itachukua siku 30
kupokea zabuni unahitajika mwezi mmoja kufanya tathmini, nawaahidi kuwa ujenzi utaanza
mwezi Machi” alifafanua Profesa Ndalichako.
Ameongeza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inasisitiza juu ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
inatambua umuhimu wa Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi ndiyo maana imejipanga
kujenga vyuo hivyo pamoja na kuimarisha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.
Aidha, Profesa
Ndalichako amepongeza ongezeko la wanafunzi walioandikishwa kuanza darasa la
kwanza Mkoani Simiyu na akasisitiza kuwa Wizara ya Elimu ambayo ndiyo inayotunga Sera
itahakikisha inasimamia kikamilifu ili wanafunzi wote wanaoanza darasa la kwanza wamalize
masoma yao.
Amesema ongezeko
hilo ambalo limesababishwa na mwamko chanya wa wazazi baada ya kuanza
kutekelezwa kwa mpango wa elimu bila
malipo limepelekea upungufu wa miundombinu shule na ndiyo maana Serikali kuu inashirikiana
na Halmashauri pamoja na wananchi katika ujenzi wa miundombinu ili kukabiliana
na upungufu kupitia Mradi wa Lipa kulingana na Matokeo(P4R).
“Kupitia mradi
wa Lipa kulingana na Matokeo tumeshajenga jumla ya vyumba vya madarasa 1104,
matundu ya vyoo 3396, mabweni 261. Tunaendelea pia kuimarisha miundombinu
katika sekta ya elimu kwa ujumla, kwa maana ya ukarabati katika vyuo vya Ualimu
ambapo tumeshakarabati vyuo 17 na shule kongwe 46 kati ya shule 88
zimeshakarabatiwa” alisema Waziri.
Profesa
Ndalichako amepongeza Uongozi wa Wilaya ya Itilima kwa kutumia vizuri jumla ya
shilingi bilioni 2.177 za Mradi wa Lipa Kulingana na matokeo(P4R) ambazo
zimetumka kujenga vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo wilayani humo.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema katika kipindi cha mwaka
2018-2020 Mkoa huo umejiwekea mpango wa kujenga mabweni kwa wanafunzi wa kike
katika kila shule ili kuwaondolea adha ya kutembea mwendo mrefu na changamoto
nyingine.
Akimshukuru
Waziri wa Elimu kwa kupeleka fedha za Mradi wa Lipa kulingana na matokeo (P4R)
katika Wilaya ya Itilima ambazo zimesaidia upatikanaji wa Mbunge wa Jimbo la
Itilima Mhe.Njalu Silanga amesema Wilaya hiyo imetekelezaji wa mradi huo kwa
kufuata taratibu na miongozo yote ya
Serikali kwa kushirikiana na wananchi.
Hii ni ziara ya
kwanza kwa Waziri Ndalichako Mkoani Simiyu ambayo imempa nafasi ya kutembelea,
kuweka mawe ya msingi, kukagua na kufungua vyumba vya madarasa, mabweni katika
maeneo tofauti Wilayani Itilima ikiwemo Kijiji cha Habiya, Lagangabilili, Itilima,
Mahembe na baadaye kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya Luguru.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Lagangabilili mara baada ya kufungua vyumba vya madarasa
vilivyojengwa kupitia Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) katika Shule ya
msingi Lagangabilili wilayani Itilima Mkoa wa Simiyu.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(kulia) akiweka Jiwe
la Msingi katika Mabweni ya Wasichana yaliyojengwa kupitia Mradi wa Lipa
Kulingana na Matokeo (P4R) katika Shule ya Sekondari Itilima wilayani Itilima
Mkoa wa Simiyu,(kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, mhe Anthony Mtaka.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako( wa tatu kushoto) na
baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu wakielekea kukagua
vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Lagangabili, wakati wa ziara yake
mkoani humo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(aliyekaa) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa
Simiyu mara baada ya kukagua vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia Mradi wa
Lipa Kulingana na Matokeo(P4R) katika Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani
Itilima.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(kulia) akisaini
kitabu cha Wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili
mkoani kwa ajili ya ziara ya siku moja(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) Katibu Tawala Mkoa, Ndg.Jumanne Sagini.
Mbunge
wa Itilima, Mhe.Njalu Silanga(kulia) akizungumza jambo wakati wa Ziara ya Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako (kushoto) aliyoifanya
wilayani Itilima.
Baadhi
ya wananchi wa Kijiji cha Habiya na Wanafunzi wa Shule tarajali/shikizi ya
Njalu iliyopo wilayani Itilima mkoani Simiyu, wakimsikiliza Waziri wa Elimu,
Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(hayupo pichani) wakati wa
ziara yake wilayani humo.
Baadhi
ya Viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu wakifurahia jambo wakati
ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(hayupo
pichani) mkoani humo.
:-
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako akizungumza
na wananchi wa Kata ya Luguru wilayani Itilima (hawapo pichani) wakati wa Ziara
yake mkoani Simiyu.
Vijana
wa Skauti wilaya ya Itilima wakivisha Skafu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Profesa. Joyce Ndalichako mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya
siku moja.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako akipokelewa na
viongozi wa Wilaya ya Itilima mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya
siku moja.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako(mbele kushoto) akiwa
na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Itilima na Mkoa wa Simiyu mara baada ya
kukagua jengo la Bweni linalojengwa kwa ya wanafunzi wa kidato cha Tano na sita
watakapoanza kusoma shuleni hapo
|
0 comments:
Post a Comment