Jumla
ya wanafunzi 19,242 mkoani Simiyu sawa na asilimia 92.5 wamechaguliwa kujiunga na
shule za sekondari katika awamu ya kwanza kwa mwaka 2018.
Hayo
yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Ndg.Jumanne Sagini katika kikao cha
kutangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2018 kilichofanyika leo Mjini
Bariadi.
Sagini
amesema jumla ya wanafunzi 20,818 sawa na asilimia 67.73 ya wanafunzi
waliofanya mtihani wa darasa la saba walifaulu, ambapo kati yao 1576 sawa na
asilimia 7.5 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya kuanza kidato cha kwanza
kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na madawati katika baadhi ya
Halmashauri.
“Wanafunzi
waliokosa nafasi Halmashauri ya Mji wa Bariadi ni wale waliopaswa kwenda Shule
ya Sekondari Kidinda(207) na Biashara(162), Halmashauri ya Wilaya ya Busega walipaswa
kwenda shule za Lamadi (486), Nasa (358) na Sogesca (363). Ni wajibu wa Halmashauri
hizi kushirikiana na wananchi kuhakikisha miundombinu pungufu imekamilishwa
haraka ili ifikapo Februari 15, 2018
wanafunzi hao waripoti kwenye shule walizopaswa kwenda” amefafanua
Sagini.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Halmashauri
ya Mji Bariadi wamesema Halmashauri zao zinaendelea na ujenzi wa vyumba vya
madarasa katika shule hizo na wataendelea kufanya jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na
wananchi kuhakikisha kuwa miundombinu hiyo pungufu inakamilika haraka, ili
kufikia Februari 05 mwakani wanafunzi wote waliokosa nafasi awamu ya kwanza
waweze kwenda shule.
Wakati
huo huo Sagini amezitaka Halmashauri kuendelea kushirikiana na wadau wote wa
elimu kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote
waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2018 bila vikwazo vya aina yoyote.
Ameongeza
kuwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla washirikiane na uongozi wa wilaya, halmashauri
na shule kuhakikisha kwamba wanafunzi
wote waliochaguliwa wanaandikishwa, wanaripoti shuleni na kuendelea na masomo
yao kwa bidii hadi watakapomaliza elimu yao ya sekondari mwaka 2021.
Akielezea
hali ya ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa mwaka 2017, Afisa Elimu Mkoa, Mwl. Julius
Nestory amesema kwa mara ya kwanza mwanafunzi aliyeongoza katika Mkoa ambaye ni
(msichana) Hoka Lyaganda Saguda ametoka katika Shule ya Serikali ambayo ni Shule
ya Msingi Sima B iliyopo Mjini Bariadi.
Amesema
ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu na kuinua kiwango cha ufaulu mkoani
humo Mikakati ya kuinua ufaulu ya kila wilaya isimamiwe kikamilifu, Ofisi za Wilaya, Halmashauri, Kata na Wakuu wa
Shule zifanye ufuatiliaji kuhusu ufundishaji na ujifunzaji na Ukaguzi wa shule ufanyike kwa kiwango
kisichopungua asilimia 50 kwa mwaka na Wakurugenzi watenge fedha kwa ajili ya
ukaguzi wa shule.
Naye
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Itilima, Mhe.Mahamoud Mabula ameshauri kuwa ili
kuinua ufaulu suala la maendeleo ya Elimu liwe agenda ya kudumu katika vikao
vyote muhimu vya Halmashauri mkoani humo, ili kutoa nafasi ya kujadili
changamoto mbalimbali za sekta ya elimu na kuzitafutia ufumbuzi.
Idadi
ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu
imeongezeka kutoka wanafunzi 16,620 mwaka 2017 hadi wanafunzi 19,242.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini akifungua kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi
wa Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani humo,
kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Afisa
Elimu Mkoa, Mwl. Julius Nestory akiwasilisha taarifa ya hali ya ufaulu wa wanafunzi
wa darasa la saba kwa mwaka 2017, katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wiayaya
Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akichangia hoja katika katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Meatu, Mhe.Juma Mwiburi akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe.Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Wilaya ya
Meatu, Veronica Kinyemi akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndg.Anderson Njiginya, akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya
ya Maswa, Mhandisi Paul Jidayi akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Itilima, Mahamoud Mabula akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoaani Simiyu,
kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe.Benson Kilangi akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018 Mkoani Simiyu,
kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Mji wa
Bariadi, Ndg.Melkezedeck Humbe akichangia hoja katika kikao cha kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa
Wanafunzi wa Kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2018, Mkoani Simiyu kilichofanyika
leo Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa wanafunzi wa
kidato cha kwanza mwaka 2018 mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Bariadi
0 comments:
Post a Comment