Wadau wa Maendeleo
Mkoani Simiyu wamekubaliana na Uchangiaji wa Ujenzi wa Miundombinu ya shule Mkoani
humo hususani vyumba vya madarasa katika shule za Msingi na Sekondari ili
kukabiliana na upungufu uliopo, kutokana na ongezeko la wanafunzi watakaoanza
darasa la kwanza na kidato cha kwanza mwaka 2018.
Makubaliano hayo
yamefikiwa katika Kikao cha Ushauri wa Mkoa(RCC) kilichofanyika jana Mjini
Bariadi.
Akifungua kikao
hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Mkoa huo unahitaji zaidi
ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule hususani
Vyumba vya madarasa , hivyo wananchi pamoja na wadau wengine wanaombwa
kuchangia ujenzi huo.
Mtaka amesema hadi
sasa wapo wadau kadhaa walioonesha nia ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa, matundu ya vyoo na nyumba za walimu kwa kutoa ahadi za vifaa vya
ujenzi vikiwemo saruji na mabati.
Mbunge wa Jimbo la
Bariadi, Mhe.John Chenge amesema suala la Elimu ni si la Serikali Kuu pekee
bali ni pamoja na wananchi, Serikali za Mitaa pamoja na wadau wengine, hivyo
wananchi wahamasishwe kuchangia ujenzi wa miundombinu hiyo kwa ajili ya maendeleo
ya Elimu mkoani humo.
Akichangia hoja
hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo ameshauri kuwa hamasa
ya ujenzi wa miundombinu ya shule
ifanywe na viongozi wote Mkoani humo, ikiwezekana kwa kubadilishana maeneo ya kwenda
kutoa hamasa ambayo ni tofauti na maeneo wanayofahamika zaidi.
“ Wakati tunaanza ujenzi wa Shule za Kata tulikubaliana
kuwa viongozi tubadilishane uzoefu kwa kila mmoja kwenda kuhamasisha maeneo
ambayo wananchi hawawafahamu na hawajawazoea;
viongozi wa Wilaya ya Bariadi walienda Meatu, wa Meatu wakaenda Maswa,
wa Maswa walienda Bariadi , lile jambo lilifanikiwa sana wananchi walihamasika
wakachangia nashauri tutumie pia mfumo huu tutafanikiwa”alisema.
Kaimu Afisa Elimu
Mkoa wa Simiyu, Ndg.Charles Maganga amesema Wanafunzi wanaotarajia kuingia
darasa la kwanza mwaka 2018 ni 109,899 wakati waliomaliza darasa la saba ni
30,898 hali inayosababisha mahitaji mapya ya vyumba vya madarasa 1757 na
madawati 26,334; wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 ni 20,818
waliohitimu kidato cha nne 6195 mahitaji mapya ya vyumba vya madarasa ni 367 na
madawati 14,623.
Aidha, Mkuu wa
Wilaya ya Maswa,Mhe.Dkt. Shekalaghe ametoa wito kwa viongozi wenzake
kuwahamasiha wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao ili waweze
kupatiwa chakula cha mchana kwa shule ambazo bado hazijaanza kufanya hivyo,
jambo na ambalo liliungwa mkono na
viongozi wengi
Kuhusu suala la
mimba shuleni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali Mkoani humo itaendelea kuwachukulia hatua
kali za kisheria wale wote watakaobainika kuwapa mimba wanafunzi wa kike.
Mtaka amesema Serikali
Mkoani humo imedhamiria na kuweka
mikakati madhubuti ya kuwalinda watoto wa kike ikiwa ni pamoja na kujenga mabweni kwa ajili ya wasichana katika
shule zote za kata, ili kuwasaidia kuondokana na vishawishi wanavyoweza
kuvipata kutokana na kutembea mwendo mrefu.
Mtaka pia alitumia
kikao hicho kuwajulisha viongozi na wadau wa Maendeleo Mkoani Simiyu kuwa Mkoa
huo umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania mwaka 2018, hivyo akawataka kujiandaa kwa ajili ya tukio hilo ambalo
litaleta watu zaidi ya 1500 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akifungua kikao cha Kamati yaUshauri ya Mkoa huo(RCC),
kilichofanyika jana Mjini Bariadi, (kushoto)Mbunge wa Bariadi Mhe. Andrew
Chenge,(wa pili kushoto) Katibu Tawala mkoa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini na ( kulia)
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia masuala mbalimbali
yaliyokuwa yakiwasilishwa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) wa
Simiyu kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika Kikao cha Kamati ya
Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe.Njalu Silanga akichangia hoja katika Kikao Kamati ya
Ushauri ya Mkoa (RCC) Mkoani Simiyu
kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia masuala mbalimbali
yaliyokuwa yakiwasilishwa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) wa
Simiyu kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Ndg Charles
Maganga akiwasilisha taarifa ya Mkoa ya
Maendeleo ya Elimu katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC),
kilchofanyika jana Mjini Bariadi.
Meneja wa AGPAHI Kanda ya Ziwa, Dkt.Nkingwa Mabelele
akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Shirika hilo ambao wadau wa Afya
Mkoani Simiyu, katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC), kilchofanyika
jana Mjini Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe.Andrew Chenge akichangia
hoja katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Simiyu kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa, Mhe.Paul Jidayi akichangia
hoja katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Simiyu kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi
wa Huduma zaMaji kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Hatari Kapufi
akiwasilisha Taarifa ya Huduma za Maji Mkoa, katika Kikao cha Kamati ya Ushauri
ya Mkoa(RCC), kilchofanyika jana Mjini Bariadi.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA)
Bariadi, Mashauri Bahini akichangia hoja katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa
(RCC) Simiyu kilichofanyia jana Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt.Seif Shekalaghe akichangia
hoja katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Simiyu kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima,
Ndg.Mariano Mwanyigu akichangia hoja katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa
(RCC) Simiyu kilichofanyia jana Mjini
Bariadi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Bariadi, Mhe.Robert
Lweyo akichangia hoja katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Simiyu kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
Kaimu
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa, Dkt.Gamitwe Mahaza akiwasilisha Taarifa ya Mkoa ya Maendeleo ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyia
jana Mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mageda Kihulya
akiwasilisha Taarifa ya Afya ya Mkoa, katika Kikao Kamati ya Ushauri ya Mkoa
(RCC) kilichofanyia jana Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment