Naibu Waziri wa Madini
Mhe.Stanslaus Nyongo amefanya ziara yake ya kikazi leo Mkoani Simiyu.
Katika ziara hiyo Mhe.Nyongo
amekutana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu pamoja na watumishi wa Ofisi
ya Madini ya Mkoa huo, lengo likiwa ni kuzungumza masuala mbalimbali kuhusu
usimamizi wa Sekta ya madini katika Mkoa wa Simiyu, ili kuleta tija kwa wanachi
na Taifa kwa ujumla.
Mhe.Nyongo pia amepata fursa ya
kutembelea na kuona Jengo la sasa la Ofisi ya Afisa Madini Mkazi na kuahidi
kuwa Wizara yake ina mpango wa kujenga jengo la jipya la Ofisi hiyo.
Aidha, amesema atahakikisha
tafiti juu ya ubora wa chumvi inayozalishwa wilaya ya Meatu zinafanyika ili
kuweza kujua ikiwa inakidhi ubora unaotakiwa kwa matumizi ya binadamu iweze
kuongezewa thamani na kutangazwa.
“Tutahakikisha tafiti hizi
zinafanyika na mpango wetu ni kwamba zifanyike kwa haraka ili chumvi ya Meatu tuweze
kuitangaza, kwa sababu Simiyu tumeshaitangaza vizuri kupitia Chaki sasa tuitangaze
tena kwa chumvi yetu” amesisitiza.
Kwa upande wake Afisa Madini
Mkazi wa mkoa wa Simiyu, Fabian Mshai amesema wachimbaji wa chumvi wako tayari
na wanaomba Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kufanya utafiti kwenye chumvi hiyo
na kushauri namna bora ya kufanya chumvi
hiyo iwe bora, ili iweze kupata soko zuri ndani na nje ya nchi.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,
Ndg.Jumanne Sagini amesema ni vema Watendaji wa Ofisi ya Madini Mkoa wakasaidiwa
kwa kuwezeshwa vitendea kazi pamoja na mahitaji mengine ili waweze kutekeleza
vizuri majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kuwafikia wachimbaji kwenye maeneo
yanayochimbwa madini na Serikali iweze ipate stahili yake.
Naibu Waziri wa Madini,
Mhe.Stanslaus Nyongo akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu (baadhi hawapo
pichani) mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya siku moja (kushoto)
Katibu Tawala Mkoa huo, Ndg.Jumanne Sagini(katikati) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa
wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa
Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo aliyoifanya mkoani humo leo.
Afisa Madini Mkazi wa
Mkoa wa Simiyu, Fabian Mshai akiwasilisha taarifa ya Mkoa huo kwa Naibu Waziri
wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo wakati akiwa katika ziara yake mkoani humo.
Baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Simiyu na Watendaji katika Wizara ya Madini wakimsikiliza Naibu Waziri
wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo wakati Wizara yake Mkoani Simiyu leo.
Naibu Waziri wa Madini,
Mhe.Stanslaus Nyongo akiagana na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya
kukamilisha ziara yake Mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Madini, Mhe.Stanslaus Nyongo akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi
ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Simiyu alipokuwa Mkoani humo leo kwa ziara ya
siku moja
Naibu Waziri wa Madini,
Mhe.Stanslaus Nyongo akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi
Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mkoa huo wakati wa Ziara yake mkoani
humo.
0 comments:
Post a Comment