Tuesday, April 24, 2018

VIONGOZI WA DINI WATAKIWAKUWA CHACHU YA MABADILIKO KWA JAMII KATIKA MATUMIZI YA NISHATI NA MAJI



Katibu Tawala wa Mkoa wa  Simiyu Ndg. Jumanne Sagini  amewataka viongozi wa dini  kwenda  kuwa chachu ya kuibadilisha jamii , kuhusu  matumizi ya nishati na maji ,na namna ya kutoa taarifa wanapouziwa bidhaa isiyo na kiwango  .

Sagini ametoa ushauri huo alipokutana  na viongozi hao mjini bariadi ,ikiwa ni mwendelezo wa Baraza la Ushauri watumiaji Nishati na Maji kuyafikia makundi mbalimbali kueleza umuhimu wa chombo hicho. .

Sagini amesema viongoni wa dini ni watu muhimu katika jamii ,hivyo ni vema elimu waliyoipata wakaitumie katika kupunguza changamoto za nishati na maji kwa kutumia ujumbe mbalimbali.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji Nishati na Maji Getruda Mbilinyi amesema kuwa kukutana na kundi la viongozi wa dini ambao wanaushawishi mkubwa katika jamii itasaidia wananchi wengi kuzijua haki zao ,pale wanapopata huduma zisizoridhisha

Baadhi ya viongozi wa dini wamesema kuwa mafunzo hayo waliyoyapata watayatumia kuwaelimisha waumini wao kupitia mahubiri faida za utumiaji nishati hiyo.

Mafunzo kwa viongozi wa dini yaliyokuwa ya siku moja yaliandaliwa na Baraza la Ushauri , Watumiaji wa huduma za Nishati na Maji baina ya  viongozi themanini na mbili wa dini na Kamati ya watumiaji wa huduma ya nishati na maji ,halmashauri ya mji wa bariadi ,lengo likiwa utoaji elimu kuhusiana na upatikanaji wa huduma bora kwa wateja.
 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(katikati) akizungumza na Viongozi wa dini na wajumbe wa Kamati ya watumiaji wa huduma ya nishati na maji wakati wa kufungua mafunzo maalum kwa ajili ya watu hao Mjini Bariadi.




Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya watumiaji wa huduma ya nishati na maji wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini wakati wa mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Baraza la Ushauri , Watumiaji wa huduma za Nishati na Maji mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!