Tuesday, May 15, 2018

BALOZI WA INDONESIA AIHAKIKISHIA SIMIYU USHIRIKIANO WA KIBIASHARA KATIKA ZAO LA PAMBA


Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede amesema moja ya malengo makuu ya ziara yake mkoani Simiyu ni kwenda kuona  mkoa huo unavyozalisha pamba na kuona namna ya kuongeza ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania(Simiyu) katika biashara ya zao la pamba.

Balozi Pardede amesema hayo wakati wa kikao maalum kati yake na viongozi wa Serikali na baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa huo Mjini Bariadi.

"Nimekuja kuona Simiyu kama mkoa unaoongoza kwa kilimo cha  pamba Tanzania, nijue namna mnavyolima, mnavyoichakata, lengo hasa likiwa ni kuongeza kiwango cha pamba inayonunuliwa na nchi ya Indonesia kutoka Tanzania, kwa kuwa nchi yetu inahitaji pamba kwa ajili ya viwanda vya nguo "

Amesema Indonesia inahitaji zaidi ya asilimia 90 ya pamba kama malighafi  katika viwanda vilivyopo nchini humo ambayo huagizwa nje ya nchi hiyo, hivyo kutokana na Mkoa wa Simiyu kuwa kiongozi katika uzalishaji wa pamba nchini mkoa huo unaweza kuuza pamba yake nchini Indonesia.

Ameongeza kuwa ili pamba ya Tanzania iweze kununuliwa nchini Indonesia inapaswa kuzalishwa katika ubora unaotakiwa na kuuzwa kwa bei isiyokuwa ya juu zaidi ikilinganishwa na  pamba kutoka katika mataifa mengine yanayozalisha pamba.

Mhe. Balozi ameyataja maeneo mengine ambayo Indonesia itaongeza ushirikiano na Tanzania hususani mkoa wa Simiyu kuwa ni mifugo, miundombinu na umeme hasa unaozalishwa kwa kutumia maji(Hydroelectric Power).

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, amemuomba Balozi Pardede kuwakaribisha wawekezaji kutoka Indonesia kuja kuwekeza mkoani humo katika ujenzi wa viwanda vya nguo(textile industries), huku akiwahakikishia upatikanaji wa ardhi bila malipo yoyote.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amemuomba Balozi wa Indonesia hapa nchini na Serikali ya Indonesia kuona uwezekano wa kuanzisha mafunzo kwa watumishi wa Simiyu, kuwezesha wafanyabiashara wa Indonesia kushirikiana na wenzao wa Simiyu katika masuala mbalimbali ya kibiashara.

Aidha, Sagini ameomba  ushirikiano  kati ya  Tanzania na Indonesia kuendelea kuimarishwa katika ngazi ya Taifa na kwa Mkoa  ambapo ameomba Balozi huyo kuona namna ya kusaidia  Mkoa wa Simiyu kuwa na Mkoa au Mji pacha nchini Indonesia.

Mhe. Balozi Prof. Dkt. Ratlan Pardede yuko katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu ambayo inatarajiwa kuhitimishwa Mei 17  mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia), Katibu Tawala wa Mkoa, Jumanne Sagini(kushoto) wakiteta jambo na Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede mara baada ya kikao kati ya balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika kikao maalum mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku nne.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede mara baada ya kikao kati ya balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede mara baada ya kikao kati ya balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani. 


 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede katika kikao kati ya balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,  Jumanne Sagini akiwasilisha taarifa ya Mkoa kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede katika kikao kati ya balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo
.
Mwakilishi wa Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Emmanuel Luangisa akizungumza  katika kati ya Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani  Simiyu.

Baadhi ya viongozi wa Serikali, Viongozi wa dini na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (hayupo pichani) katika kikao na Balozi huyo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Baadhi ya viongozi wa Serikali, Viongozi wa dini na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (hayupo pichani) katika kikao na Balozi huyo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Baadhi ya viongozi wa Serikali, Viongozi wa dini na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede (hayupo pichani) katika kikao na Balozi huyo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kikao kati ya Balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Balozi wa Indonesia hapa nchini, Prof. Dkt. Ratlan Pardede(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na Wataalam wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kikao kati ya Balozi huyo na Viongozi wa Mkoa huo kilichofanyika Mjini Bariadi siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.







0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!