Tuesday, May 1, 2018

RC MTAKA AWATAKA WAFANYAKAZI MKOANI SIMIYU KUCHANGAMKIA FURSA ILI WAJIIMARISHE KIUCHUMI



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka wafanyakazi  mkoani humo kuchangamkia fursa ya kununua viwanja katika maeneo ambayo  uwekezaji mkubwa utafanyika ili waweze kujenga nyumba na majengo mengine ya biashara ambayo yatawawezesha kujiongezea kipato cha ziada.

Mtaka ameyasema hayo  wakati akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Mkoa wa Simiyu katika Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa wilayani Itilima.

“Mwaka huu tutakuwa wenyeji wa NaneNane Kitaifa, karibu na eneo la Nanenane tunatoa eneo kwa ajili ya kujenga Chuo cha Mipango kajengeni hosteli wanafunzi wapange; tunajenga kiwanda cha vifaa Tiba Dutwa jengeni nyumba watumishi wakapange, tunajenga VETA pale Bunamhala jengeni vyumba vya biashara  watu waje wapange,  Simiyu ni mahali penye fursa nyingi” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka amesema mkoa wa Simiyu ni Mkoa wenye agenda ya maendeleo hivyo akawataka wafanyakazi, viongozi na wananchi kujiepusha kuwa watu wa matukio badala yake wajikite katika agenda ya maendeleo ya Mkoa huo.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wafanyakazi Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu(TALGWU)  Wandiba Kongoro ameomba Serikali izifanyie kazi changamoto mbalimbali za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na madeni hususani ya uhamisho, likizo na matibabu, utararibu wa upandishaji wa madaraja, baadhi ya waajiri kutoitisha mabaraza ya wafanyakazi na baadhi ya waajiri kutowapa watumishi hodari zawadi zao.

Kongoro amesema changamoto nyingine ni Michango ya wafanyakazi katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutolipwa kwa wakati hasa kwa watumishi wanaolipwa kwa kutumia Makusanyo ya ndani na akawaomba waajiri kulishughulikia hili katika kipindi hiki cha mpito kabla mifuko haijaunganishwa ili kuepusha adha kwa watumishi watakapostaafu.

Nao watumishi na wananchi walikuwa na maoni mbalimbali kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Kimkoa ambayo yamefanyika kwa mara ya sita sasa tangu kuanzishwa kwa Mkoa wa Simiyu mwaka 2012

“Wana Itilima tumeipokea Mei Mosi kwa furaha sana kama mnavyoona mwitikio wa wananchi na wafanyakazi ni mkubwa, mpangilio wa matukio uko vizuri, nimevutiwa na utaratibu wa kuwasoma wafanyakazi hodari mbele ya wenzao na kuwapa zawadi, hii itawafanya wafanyakazi wengine kuwa na bidii ili nao wapate ” alisema Peter Karume Shimo mwananchi kutoka Itilima.

“Siku hii tumeipokea vizuri na  Mkuu wetu wa Mkoa ametuambia mambo mazuri ya kutufanya tuweze kujiimarisha kiuchumi kama watumishi na vile vile kufanya kazi zetu kwa weledi, binafsi nawashauri wafanyakazi wenzangu tufanye vile tunavyoelekezwa na viongozi wetu” alisema Mwamba Isaya Venance Mwalimu wa Shule ya Msingi Munze wilayani Itilima,

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei  Mosi mwaka 2018 yamefanyika chini ya Kaulimbiu inayosema “KUUNGANISHWA KWA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII, KULENGE KUBORESHA MAFAO YA WAFANYAKAZI


Baadhi  ya Wafanyakazi wa  Mkoa wa Simiyu wakiwa katika Maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili).

Baadhi  ya Wafanyakazi wa  Mkoa wa Simiyu wakiwa katika Maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili).


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa mkoa wa Simiyu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili).
Kutoka kushoto, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa  wa Simiyu Bw.Kulwa Dwese, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka , Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Donatus Weginah na Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga wakifurahia jambo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili).
Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Simiyu(TALGWU)  Wandiba Kongoro akisoma risala ya wafanyakazi wa mkoa huo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili  
Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselemu akitoa salamu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili).

Baadhi ya wafanyakazi hodari wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani)  wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili).


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( mwenye skafu) na viongozi wengine wa Mkoa huo wakishuhudia maandamano ya wafanyakazi wa mkoa huo(hawapo pichani)  wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili).

Baadhi  ya Wafanyakazi wa  Mkoa wa Simiyu wakiwa katika Maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili).
 Baadhi  ya Wafanyakazi wa  Mkoa wa Simiyu wakiwa katika Maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( mwenye skafu) , viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi wakicheza wimbo maalumu wa kwaya ya walimu wa Bariadi mkoani humo, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi ambayo yalifanyika  Kimkoa katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima (Lagangabilili).



0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!