Thursday, May 31, 2018

SIMIYU YAJIPANGA KUIIMARISHA SHULE YA SEKONDARI BARIADI KAMA SHULE MAALUM YA MICHEZO

Serikali mkoani Simiyu imesema imekusudia kuiimarisha shule ya Sekondari ya Bariadi ambayo ilitengwa kuwa Shule ya Michezo, kwa kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike na wa kiume na kuiwekea miundombinu yote muhimu,  ikiwemo viwanja vya michezo yote kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipokuwa akifunga mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa katika viwanja vya Shule ya sekondari ya Wasichana Maswa.

"Ningehitaji tuifanye Shule ya Sekondari Bariadi kuwa shule maalum ya kimichezo ya Kimkoa, yenye mabweni ya wavulana na wasichana na tuiwekee miundombinu yote ya michezo ili watoto wote wenye vipaji vya michezo waende pale na nitaomba kibali walimu wa michezo wahamie hapo,  tufike mahali ambapo Bariadi Sekondari itatoa wachezaji wa kutumainiwa kwenye Taifa" amesema Mtaka.

Aidha, amewataka wanafunzi wote kuwa na mtazamo tofauti katika michezo kwa kuondokana na nadharia ya kuwa michezo ni afya, burudani na kwenda kwenye dhana ya michezo kama taaluma, ajira na biashara, ambapo amehimiza kuwa mkoa huo unafanya uwekezaji na mapinduzi ya michezo kibiashara katika Shule hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka wanafunzi hao kuuwakilisha vema mkoa na kuwatakia heri na ushindi katika mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa yatakayofanyika jijini Mwanza, huku akiwataka kuwa na nidhamu kipindi chote watakachokuwa huko na akaahidi kutoa zawadi mbalimbali kwa washiriki wote watakaporudi na ushindi.

Katika hatua nyingine Mtaka akiwakabidhi walimu na wanafunzi jezi zilizotolewa kwa udhamini wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, kupitia mradi wake wa Kiwanda cha Chaki (MASWA CHALKS) amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi mkoani humo kujipanga kwa ajili ya kudhamini mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA mwaka 2019 kupitia miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao ili kuendelea kuutangaza mkoa huo.

Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema changamoto kubwa zilizowakabili washiriki wa mashindano hayo ni pamoja na upungufu wa viwanja katika shule za msingi na sekondari na kukosa wafadhili kutoka nje ili kuwezesha wanafunzi kukaa kambini muda mrefu kujiandaa na mashindano.

Kwa upande wao wanafunzi/ washiriki wa UMISSETA na UMITASHUMTA mkoa wa Simiyu wamemhakikishia Mkuu mkoa na wananchi kwa ujumla kuwa watarudi na ushindi katika mashindano hayo Kitaifa.

"Mwaka 2018 tumejipanga na ushindi ni lazima kwa mwaka huu sisi tunaenda Mwanza kushinda na kuchukua makombe, tunamhakikishia Mkuu wa Mkoa  na wananchi wote wa Simiyu kuwa tunarudi na ushindi" Alisema Mwanaidi Khamis kutoka  Maswa.

Jumla ya washiriki 811 wa michezo mbalimbali kutoka katika Halmashauri zote Sita za Mkoa wa Simiyu wameshiriki mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa kwa mwaka 2018.

MWISHO 



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia) akikabidhi kombe la msindi wa jumla michezo ya UMISSETA kimkoa mwaka 2018 kwa Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mwl. Yassin Kitentya wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa  


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wanamichezo katika hafla ya kufunga Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA  katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kulia) na baadhi ya wana michezo wakionesha jezi zilizotolewa na Kiwanda cha MASWA CHALK kama udhamini katika michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA, wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa  

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe (wa nne kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia), wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa .

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe (wa nne kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia), wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtakaakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa michezo, mara baada ya kufunga  Mashindano  ya UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Wanamichezo kutoka Wilaya ya Busega wakionesha onesho lao la ngoma za asili mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mashindano hayo  katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick  Sagamiko akitoa taarifa ya vitu ambavyo kiwanda cha Maswa Chalks Kimedhamini katika Mashindano  ya UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa, wakati wa kufunga mashindano hayo  katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa na baadhi ya viongozi na wawakilishi wa wanamichezo wakionesha jezi zilizotolewa na Kiwanda cha MASWA CHALK kama mdhamini katika michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA, wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akionesha moja ya jezi zilizotolewa na Kiwanda cha MASWA CHALK kama mdhamini katika michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA, wakati wa kufunga mashindano ya UMISSETA UMITASHUMTA katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa, mara baada ya kufunga mashindano hayo katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya wanamichezo mara baada ya kufunga  Mashindano  ya UMISSETA na UMITASHUMTA kimkoa katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!