Saturday, May 26, 2018

KAMATI NA BODI ZA SHULE ZATAKIWA KUJIUZULU SHULE ZINAPOFANYA VIBAYA KWENYE MITIHANI


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema wakati umefika kwa kamati na bodi za Shule mkoani humo kujitathmini ikiwa zinafaa kuendelea na majukumu yao au kujiuzulu pale Shule zao zinapofanya vibaya katika mitihani  hususani ya Taifa.

Mtaka ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wenyeviti wa Kamati na Bodi  za Shule za Halmashauri ya Mji Bariadi na Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Bariadi,  katika kikao maalum kilicholenga  kujadiliana na kupanga maandalizi ya Kambi za kitaaluma kwa Kidato cha Nne na Darasa la Saba Wilayani humo.

Amesema mara nyingi wanafunzi wanapofanya vibaya kwenye mitihani wazazi wengi wamekuwa wakiwalaumu na kuwanyoshea vidole walimu badala ya kutathmini mchango wao katika ufaulu wa watoto wao.

“ Watoto wakifeli mnaanza kuwanyoshea walimu vidole, huu mwaka watoto wakifeli kamati za shule zijiuzulu, mnapowanyoshea walimu vidole hivi kamati za shule zenyewe huwa zinachukua wajibu gani, jiuzuluni ili waje wazazi wengine wenye mawazo mapya yatakayozivusha shule kwenda kwenye ufaulu mzuri” alisisitiza Mtaka.

Mtaka amewataka wazazi washikamane na Serikali pamoja na walimu katika kuhakikisha wanafanya mapinduzi ya Elimu kwa kuwa ufaulu wa wanafunzi unategemea ushirikiano wa wazazi, walimu na wanafunzi wenyewe, hivyo akasisitiza kuwa Wenyeviti wa Kamati na Bodi za Shule wakafanye vikao na wazazi kuweka mipango mizuri ya kufanikisha kambi za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na darasa la saba pamoja na maendeleo ya elimu kwa ujumla.

 Aidha, kama Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa Mtaka amewahakikishia wazazi kuwa wanafunzi wote watakaokuwa katika kambi watatunzwa na kulindwa huku akiwatahadharisha watu wenye nia mbaya kutowafuatilia wanafunzi wa kike kwa lengo la kuwarubuni kwa namna yoyote kwa kuwa Serikali itawachukulia hatua wote watakaobainika.

Mtaka amesisitiza wazazi wote kuchangia mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi watakaokuwa kambini ili kuwezesha kambi hizo kufanyika hususani chakula, huku akiwaeleza wazazi kuwa kupitia kambi hizo watarajie kuona mabadiliko ya kitaaluma kwa watoto wao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amezitaka Kamati na Bodi za Shule wilayani humo kufanya vikao na Wazazi kwa ajili ya kuwaeleza wajibu wao katika kufanikisha Kambi hizo za Kitaalamu na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo Mei 30, 2018 ofisini kwake.

Kiswaga amesema Kamati zote ambazo zitashindwa kutekeleza agizo hilo zitavunjwa na Wenyeviti na wajumbe wa Kamati hizo watawajibishwa
.
Wilaya ya Bariadi itazindua rasmi kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa  Kidato cha Nne na Darasa la Saba Juni 06 mwaka huu.
MWISHO:
Baadhi ya Wenyeviti wa Bodi na Kamati za Shule wa Wilaya ya Bariadi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21,   kilichofanyika Shule ya Sekondari Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wenyeviti wa Kamati na  Bodi za Shule za Wilaya ya Bariadi (hawapo pichani) , katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la Saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya Sekondari Bariadi
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na Wenyeviti wa Kamati na  Bodi za Shule za Wilaya ya Bariadi (hawapo pichani) , katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la Saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya Sekondari Bariadi
Baadhi ya Wenyeviti wa Bodi na Kamati za Shule wa Wilaya ya Bariadi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya Sekondari Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifurahia jambo katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la Saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya Sekondari Bariadi, (kulia) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkezedeck Humbe.
Baadhi ya Wenyeviti wa Bodi na Kamati za Shule wa Wilaya ya Bariadi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao maalum cha maandalizi ya Kambi za Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne na Darasa la saba zinazotarajiwa kufanyika mwezi Juni kwa siku 21, kilichofanyika Shule ya Sekondari Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!