Na Stella Kalinga
Mkoa
wa Simiyu unatarajia kuanza kutumia chaki zilizozalishwa na vijana wa Wilaya ya
Maswa mkoani humo kuanzia tarehe Mosi Oktoba, 2016.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika kikao cha
Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Kanisa
Katoliki Mjini Bariadi.
Mkuu
huyo wa Mkoa amesema Mkoa huo unatumia jumla ya shilingi milioni 25 kununua
takribani katoni 1200 za chaki( ambazo zinatengenezwanje ya nchi) kwa mwezi katika shule za Msingi na Sekondari,
hivyo akawaasa Watanzania kujenga utamaduni wa kupenda na kuthamini vitu vya
nchini kwetu ili kuinua uchumi wa Vijana wazalishaji na Taifa kwa ujumla.
“Tuanze
kuwafundisha Watanzania kutoka kwenye dhana ya kuwa Chaki ya Kichina ndiyo bora
kuliko inayotengenezwa hapa nchini, nahitaji Maafisa Elimu mkae na Walimu Wakuu,
Wakuu wa Shule na Waratibu mjadili na muone namna nzuri ya kupata hizo chaki
ambazo zitakuwepo katika Banda la Maswa Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi katika
wiki ya vijana na baadaye katika maduka yatakayokuwepo kwenye kila wilaya”,
alisema Mtaka.
Mtaka
amesema Maafisa Elimu wote wa Wilaya wahakikishe wazabuni wanaopeleka chaki
katika Shule za Msingi na Sekondari wananunua chaki zinazozalishwa na Vijana wa
Wilaya ya Maswa ambazo zitatambulika kama ‘MASWA CHALKS’, ambapo Vijana wa
Maswa watafungua duka kwa kila wilaya
hivyo badala ya kuzifuata chaki hizo mahali zinapozalishwa kila wilaya
itazipata chaki hizo katika eneo husika
Aidha,
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama atakapokuja katika Uzinduzi wa wiki
ya vijana Oktoba 08, 2016 atakwenda kutembelea kiwanda hicho, kujione uzalishaji unavyoendelea na baadaye Mkoa
utaomba kibali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John
Pombe Joseph Magufuli, kuruhusu Vijana hawa
wa Kitanzania kuzalisha bidhaa hii kwa kutumia malighafi
kutoka hapa nchini na kuiuza nchi nzima.
Aidha,
Mtaka amesema katika Azma ya Mkoa ya kila wilaya kuzalisha bidhaa moja yaani
(one distict one product) pamoja na Vijana wa Maswa kuzalisha chaki, Vijana wa Wilaya
ya Meatu watakuwa wakisindika maziwa ya ng’ombe kwa kuwa ni Wilaya ya Meatu ndiyo yenye ng’ombe wengi, hivyo kupitia mradi
huo wafugaji wa Meatu na Simiyu kwa ujumla watapata soko la maziwa na thamani
yake itaongezeka na yatauzwa katika maduka yatakayokuwepo katika kila wilaya.
Amewataka
viongozi kuondokana na dhana ya kuwa kupungunza mifugo ndio njia pekee ya
kuwakomboa wafugaji na badala yake wawasaidie kupata majawabu ya changamoto zao
ikiwa ni pamaja na kuongeza thamani mazao ya mifugo kama maziwa, ngozi na nyama.
Sanjali
na hilo Mtaka ameeleza azma ya kuufanya Mkoa wa Simiyu kuwa Mkoa wa mfano wa
kuigwa hasa katika utekelezaji wa maagizo ya Viongozi Kitaifa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya
mwaka 2015.
Kwa
upande wake Naibu ,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Luhaga Mpina amepongeza jitihada hizo
zinazofanywa na akaahidi kushirikiana na Serikali ya Mkoa katika suala la
uanzishwaji wa viwanda vidogo ambapo aliahidi kusaidia Mkoa wa Simiyu upate
kiwanda cha kutengeneza mkaa kwa kutumia mimea mingine tofauti na miti ili
kulinda na kutunza mazingira.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya
Ushauri ya Mkoa (RCC) (hawapo pichani) katika kikao kilichafanyika leo, mjini Bariadi
|
Mkurugenzi
wa Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza akimmiminia maziwa yaliyotengenezwa na Vijana
wa Wilaya hiyo; Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka |
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Simiyu wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Mjini Bariadi |
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia jambo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika
leo Mjini Bariadi.
|
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Simiyu wakifuatilia mijadala
mbalimbali katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Mjini Bariadi
|
0 comments:
Post a Comment