Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista
Mhagama amefanya kikao cha ndani na Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu leo
katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Mjini Bariadi, ili kupata taarifa ya
maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana
na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo
tarehe 8 na 14 Oktoba 2016 .
Mkoa wa Simiyu umepewa
heshima ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo kwa mwaka huu. Maadhimisho ya wiki
ya vijana yatafunguliwa rasmi tarehe 08 Oktoba 2016 na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista
Mhagama na kuhitimishwa tarehe 14 Oktoba, 2016, ambapo Vikundi vya Vijana na
Wajasiriamali kutoka mikoa yote nchini watashiriki na kuonesha kazi zao za
uzalishaji ikiwa ni pamoja na shughuli za ugunduzi wa vitu mbalimbali katika
Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi.
Pamoja na maonesho ya
kazi za vijana, Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu
ya Baba kifo cha Baba wa Taifa Mwl.
Julius Kambarage Nyerere yatafanyika tarehe 14 Oktoba 2016 katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli .
Mhe. Mhagama amesema Maadhimisho
ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016 ni ya Kihistoria kwa kuwa ni
ya kwanza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli na tukio la kihistoria
kwa Mkoa wa Simiyu pia.
Akiwa Wilayani
Bariadi Mhe. Mhagama pamoja na kufanya
kikao na viongozi na watendaji, alitembelea na kuona Kanisa la Mtakatifu
Yohana(John) la Mjini Bariadi, ambapo Ibada ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl.
Julius Kambarage Nyerere itafanyika, Uwanja wa Sabasaba utakaotumika katika
maonesho ya kazi za vijana katika wiki ya vijana na Uwanja wa Halmashauri ya
Mji Bariadi ambao utatumika katika Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa
Uhuru Oktoba 14, 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na
Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama Katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
|
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye
Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni mara baada ya
kutembelea Kanisa la Mtakatifu Yohana(John) la Mjini Bariadi, mahali ambapo
Ibada ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa itafanyika tarehe 14 Oktoba 2016.
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akiagana na Padre Kizito Nyanga mara baada ya kutembelea Kanisa la Mtakatifu Yohana (John) la mjini Bariadi , mahali ambapo Ibada ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa itafanyika tarehe 14 Oktoba 2016 |
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akitoa
maelekezo baada ya kukagua sampuli ya mabanda yatakayotumiwa na vijana katika
maonesho ya kazi zao wakati wa maonesho ya wiki ya vijana atakayoyafungua rasmi
tarehe 08 Oktoba, 2106 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi, (kulia)
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi ,
Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Jemasi Kajugusi
|
:
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama
akiangalia baadhi ya miundombinu (haipo pichani) itakayotumiwa na vijana katika
maonesho ya kazi zao wakati wa maonesho ya wiki ya vijana atakayoyafungua rasmi
tarehe 08 Oktoba, 2106 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi, ( kutoka kulia),
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, Katibu Tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne
Sagini, (kulia) Mkurugenzi wa Idara ya
Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye
Ulemavu, Bw. Jemasi Kajugusi.
|
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama
akizungumza na Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu baada ya kukagua sampuli ya mabanda takayotumiwa na
vijana katika maonesho ya kazi zao wakati wa maonesho ya wiki ya vijana
atakayoyafungua rasmi tarehe 08 Oktoba, 2106 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini
Bariadi, ( kutoka kulia), Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, Katibu
Tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini, (kulia) Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi ,
Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Jemasi Kajugusi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka katika Ofisi yake Bw. Jemasi Kajugusi(wa kwanza kulia), akiwa na Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa
Mkoa wa Simiyu baada ya kukagua sampuli ya mabanda yatakayotumiwa na vijana katika maonesho ya
kazi zao wakati wa maonesho ya wiki ya vijana atakayoyafungua rasmi tarehe 08
Oktoba, 2106 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi.
|
Baadhi
ya Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi ,
Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) katika
kikao kilichofanyika Mjni Bariadi kwa lengo la kupata taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho
ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha
Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba 2016 .
|
0 comments:
Post a Comment