Na Stella Kalinga
Kikao
cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC) kimeridhia wanafunzi wa shule za
Msingi na Sekondari za Kutwa katika mkoa huo kupata chakula cha mchana shuleni
ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujifunza.
Uamuzi
huo umefikiwa kufuatia hoja iliyowasilishwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa
Simiyu kupitia Chama cha Mapinduzi , Mhe. Leah Komanya juu ya taarifa
iliyotolewa na Afisa Elimu Mkoa Mwl. Julius Nestory kuwa takribani asilimia 38
ya wanafunzi katika Mkoa wa Simiyu hawahudhurii masomo kikamilifu.
Mhe.
Komanya alisema moja ya sababu inayopelekea wanafunzi kutokwenda shule ni
kukosa chakula, hivyo endapo watapata chakula shuleni watashawishika kusoma na
muda waliokuwa wanakwenda kutafuta chakula watautumia kwa ajili ya masomo.
Komanya
alisema kwa mujibu wa taarifa ya shirika moja la Kimataifa lililofanya utafiti
wa athari za mabadiliko ya tabia nchi katika Wilaya ya Meatu, ilibanishwa kuwa watoto kutoka familia za
wanawake wajane zimeathiriwa na uwezo duni, hivyo watoto hawaendi shuleni kwa sababu
ya kukosa chakula, hli inayopelekea watoto hao kwenda kujitafutia chakula, jukumu
ambalo lingepaswa kufanywa na baba zao .
“Matokeo
ya darasa la saba Wilaya ya Meatu mwaka 2015, shule iliyokuwa ya mwisho katika
Wilaya ya Meatu ilitoka kata ya Mwamanimba na Kata ya Mwamanimba
nilivyofuatilia ni kata iliyofanyiwa tathmini ya athari za mabadiliko ya tabia
nchi, kwa hiyo ni wazi kwamba chakula kikipatikana uwezo wa wanafunzi wa
kuhudhuria na kuchangia shuleni utakuwa mkubwa” alisema Komanya.
Mhe.Komanya alisema wazazi kwa umoja wao
washirikiane na Serikali katika kuchangia chakula ili kusaidia familia ambazo
hazina uwezo wa kuchangia fedha ziweze kutoa mazao ya chakula kwa kuwa wakazi
wa Mkoa wa Simiyu walio wengi ni wakulima.
Aidha,
Mhe. Komanya ametoa wito kwa mashirika na taasisi mbalimbali kuunga mkono Mkoa wa
Simiyu kwa kusaidia kutoa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na majiko banifu
katika shule, nishati itakayotumika kupikia, vyakula na vyombo vya kupikia,
ambapo yeye ameahidi kutoa vyombo vya kupikia katika Wilaya zote na
akaombaWabunge wote wa Mkoa wa Simiyu wamuunge mkono.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema suala la wazazi
kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi ni la hiari, hivyo akatoa maelekezo kwa Viongozi Ngazi ya
Wilaya kuwafafanulia wananchi ili wawe na uelewa wa pamoja na wafuate taratibu
zinazotakiwa kupata vibali vya kuanza kwa zoezi hilo.
Aidha,
Mtaka amewatakahadharisha watendajiwa ngazi zote kuhakikisha wanapotoa vibali
hivyo kwa Kamati za Shule na Wazazi kuzingatia taratibu ili wanafunzi wapate
chakula badala ya kutafuta mianya ya kujinufaisha kwa namna moja au nyingine.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Mickness Mahela amesema
anaunga mkono utaratibu wa chakula mashuleni na katika kata yake ya Nyashimo
vikao vya Maendeleo ya Kata vimeshakaa na kukubaliana kuanza kutoa chakula kwa
wanafunzi, ambapo Shule ya Sekondari Nasa inatarajia kuanza kutoa chakula kwa
wanafunzi Novemba Mosi, 2016.
Mbunge
waViti Maalum mkoa wa Simiyu (CCM), Mhe. Leah Komanya akizungumza na wandishi
wa habari hawapo pichani) mara baada ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika
leo Mjini Bariadi.
|
0 comments:
Post a Comment