Na Stella Kalinga
Serikali
Mkoani Simiyu imetangaza azma yake ya kuanza kutengeneza Chaki ambazo zitauzwa
katika Wilaya za Mkoa huo, mikoa jirani na baadaye nchi nzima kabla ya Oktoba 14 mwaka huu.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony John Mtaka wakati
alipohitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji wa Chaki kwa vikundi vya
vijana Wajasiriamali wilayani
Maswa, yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo
vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga.
Mtaka
amesema shule zote za Msingi na Sekondari za Serikali Mkoani humo zinatumia jumla ya katoni 1200 za chaki ambazo
zinagharimu shilingi 25,000,000 kwa kila mwezi, hivyo kama Vijana wa Wilaya ya
Maswa wakizalisha Chaki na kusambaza katika mkoa mzima watajipatia kipato na kuondokana
na umaskini.
Mkuu
huyo wa Mkoa amesema katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kuwa na Tanzania ya Viwanda, Mkoa huo
umejipanga kuimarisha uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo ambavyo
vitazalisha mahitaji ya kila siku ya wananchi, hivyo wamedhamiria kuwa na
uzalishaji wa bidhaa moja kwa kila wilaya ( one district one product), ambapo Wilaya ya Maswa itakuwa
ikizalisha chaki.
“
Wilaya ya Maswa imepokea shilingi 38,000,000 Meatu 31,000,000 kwa ajili ya vijana kutoka
Wizara yenye dhamana na Vijana, sasa hivi tumepeleka maombi ya wilaya zilizobaki. Tumedhamiria
kuutambulisha Mkoa kwa kuzalisha bidhaa zetu wenyewe, tumeanza na Chaki wilaya
ya Maswa, Wilaya ya Meatu wao watazalisha maziwa, tutaendelea kutengeza utambulisho(brand) wa wilaya
nyingine kwa kuzalisha bidhaa zinazoendana na malighafi zilizopo” alisema
Mtaka.
Akizungumza
katika hitimisho la Mafunzo hayo kwa Vijana, Meneja wa Shirika la Viwanda
vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga, Athanas Moshi ametoa wito kwa vikundi vya
vijana kuwa na mipango itakayowasaidia kutangaza bidhaa zao na kupata soko la
bidhaa hizo ndani na nje ya Mkoa ili kujiongezea kipato.
“Mtakapoanza
kuzalisha chaki, kulingana na tathmini iliyofanyika kama mtauza kwa Mkoa wa
Simiyu tu mtakuwa na uwezo wa kutengeneza faida ya shilingi 8,000,000 kila
mwezi, hiyo si fedha ndogo mkiwa na mipango thabiti mkazalisha chaki bora
mtaweza kuuza chaki zenu nchi nzima na hata nje ya nchi” alisema Moshi.
Naye
mmoja wa vijana waliopata mafunzo ya utengenezaji wa chaki, Kelvin Steven
ametoa wito kwa Wananchi wa Simiyu na
Watanzania kwa ujumla, kuunga mkono
juhudi za Vijana Wajasiriamali na kuthamini bidhaa zinazozalishwa hapa nchini
ili kuinua uchumi wa Vijana hao na Taifa kwa jumla.
Aidha,
Bi. Specioza Fundikira ambaye pia amepata mafunzo hayo amesema matarajio ya Vijana
waliopata mafunzo ni kuwa uzalishaji wa chaki utakapoanza kutakuwa na soko la
uhakika kwa Shule zote za Msingi na Sekondari za Serikali mkoani humo na mikoa
ya jirani, vijana watapata ajira na kuachana na shughuli zisizo halali kama wizi
na ulevi.
Kwa
Mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe vijana kutoka vikundi 8
vya Wajasiriamali ambao wameunda kikundi kimoja cha ‘Maswa Youth Enteprises’ wamepatiwa
mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji wa chaki na Shirika la Viwanda Vidogo
vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga kuanzia tarehe 29/08/2016 hadi tarehe
03/09/2016.
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akionesha aina tofauti za maboksi yatakayotumika
kufungashia chaki nyeupe na za rangi ambazo zinatarajiwa kuanza kuzalishwa na
Vijana wa Wilaya ya Maswa, Mkoani humo wakati alipohitimisha Mafunzo ya
Teknolojia ya Utengenezaji wa Chaki kwa vijana hao, (katikati) Mkuu wa Wilaya
ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe (kulia) Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa, Mhe.
Peter Bunyongoli.(Picha Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu)
|
|
Vijana
wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa wakiweka chaki walizotengeneza wakati wa
mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na SIDO katika maboksi
mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) kabla ya Mkuu huyo wa mkoa kuhitimisha mafunzo hayo. |
|
Baadhi ya Vijana
wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa wakiangalia sampuli za maboksi
yaliyopendekezwa kutumika kufungashia chaki pindi uzalishaji utakapoanza wakati
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) akihitimisha mafunzo
ya Teknolojia ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na SIDO kwa vijana hao,
wilayani humo
Meneja wa Shirika la
Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga, Athanas Moshi (aliyesimama)
akizungumza na vijana na wadau
wengine wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji chaki
yaliyotolewa na Shirika hilo kwa Vijana
wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa.
|
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe akizungumza na vijana na wadau wengine wakati wa
kuhitimisha mafunzo Teknolojia ya
utengenezaji chaki yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo SIDO kwa
Vijana wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa, katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya
Wilaya hiyo.
Baadhi ya Vijana
wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa na Wadau wengine wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo ya Teknolojia
ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO)
Mkoa wa Shinyanga kwa vijana hao.
Baadhi ya Vijana
wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa na Wadau wengine wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akihitimisha mafunzo ya Teknolojia
ya utengenezaji chaki yaliyotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO)
Mkoa wa Shinyanga kwa vijana hao.
Mwakilishi wa Vijana
wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa, Paschal Njige (kulia) akisoma risala kwa
niaba ya wenzake kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati wa kuhitimisha mafunzo ya Teknolojia ya utengenezaji wa chaki yaliyotolewa kwa vijana hao wilayani
Maswa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.
Seif Shekalaghe (katikati) mara alipotembelea jengo linakarabatiwa kwa ajili ya
kufanywa ofisi ya Vijana Wajasiriamali wa Wilaya ya Maswa wanaojiandaa kuanza
kutengeneza chaki baada ya kupata mafunzo kutoka SIDO, (kushoto) Afisa Vijana
wa Wilaya ya Maswa, Revocatus Bunduki.
|
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na Viongozi wa Wilaya
ya Maswa (baadhi hawapo pichani) kabla ya kuhitimisha mafunzo ya Teknolojia ya
utengenezaji chaki yaliyotolewa kwa vijana Wajasiriamali wa wilaya hiyo na Shirika
la Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Shinyanga.
|
0 comments:
Post a Comment