Na Stella Kalinga
Serikali Mkoani Simiyu imekusudia kufanya
mabadiliko kwa Wakuu wa Shule , Walimu Wakuu na Waratibu wa Elimu Kata katika
Halmashauri zote mkoani humo, kwa kuzingatia sifa za kujiendeleza kielimu,
uwezo kiutendaji na uadilifu.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony John Mtaka katika kikao
alichofanya leo Ofisini kwake na Maafisa Elimu, Vifaa na Takwimu na Maafisa
Elimu Vielelezo kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa huo.
Mtaka
amesema ameamua kufanya kikao na Wataalam hao ili kupata mchango wao katika
suala la uwepo wa mkanganyiko wa takwimu mbalimbali za elimu hususani takwimu
za wanafunzi kwa Walimu wakuu na Maafisa Elimu ambazo zimekuwa zikitofautiana
kila zinapohitajika kwa nyakati tofauti.
“Ofisi
hiyo hiyo ya Afisa Elimu inatoa Idadi ya
Wanafunzi wanaoletewa ruzuku ya elimu bila malipo ( kabla ya uhakiki) nyingine, idadi ya wanafunzi baada ya uhakiki nyingine na idadi ya wanafunzi wanaochangiwa
fedha za Michezo (UMISETA) kwa Elimu ya Sekondari ni nyingine na anayeleta
taarifa zote ni huyo huyo, hatuwezi kuwa
na watu ambao kila wanapotoa takwimu hatuziamini mpaka zihakikiwe”alisema Mtaka.
Kufuatia uwepo wa mkanganyiko na
mabadiliko ya mara kwa mara ya takwimu hizo katika idara ya elimu, Mkuu wa Mkoa
huyo amesema kwa kuwa Elimu ni kipaumbele cha kwanza cha Mkoa; ipo haja ya
kufanya mabadiliko kwa Walimu wakuu, Wakuu wa shule na Waratibu wa Elimu kata
ili wapatikane watu wenye sifa watakaosimamia shule na fedha za Serikali kwa
uadilifu pasipo kufanya udanganyifu katika takwimu.
Mtaka amesema Walimu Wakuu na
Waratibu Elimu Kata wa Mkoa wa Simiyu wamewezeshwa ikiwa ni pamoja na kupewa
mafunzo na vitendea kazi kama vishikwambi kwa ajili ya utunzaji wa takwimu,
pikipiki na fedha ya mafuta hivyo wanapaswa kuwa mfano kwa kuwajibika na
kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu.
Aidha,
Mtaka amesema kama taarifa za udanganyifu katika idara ya Elimu zitaendelea
Wataalamu wa Vifaa, Takimu na Vielelezo katika Halmashauri watakuwa hawafanyi
kazi yao sawa sawa, hivyo aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri kutambua nafasi
ya wataalamu hao na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ili wawe na taarifa
sahihi za idara ya elimu.
Akitoa
mchango wake katika kikao hicho Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya
Busega, Mathayo Maingu amesema moja ya
sababu ya uwepo wa mkanganyiko wa takwimu ni uzembe kwa baadhi ya Walimu wakuu
na Wakuu wa Shule katika suala la utunzaji wa takwimu hali inayopelekea kutoa
takwimu zisizo sahihi.
Kwa
upande wake Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Itilima Ayubu Mbilinyi
amesema ili kukabiliana na udanganyifu katika takwimu Watendaji katika Idara ya
Elimu wanapaswa kuimarisha mfumo wa usimamizi wa nyaraka mbalimbali za usajili,
mahudhurio ya wanafunzi mashuleni na kuwa na mfumo sahihi wa kutambua idadi ya wanafunzi
katika nyakati zote.
Naye
Afisa Elimu Vielelezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Charles Martini
amesema hali ya udanganyifu wa takwimu imekuwa ikisababishwa na Maafisa Elimu,
Vifaa na Takwimu na Maafisa Elimu Vielelezo kutowezeshwa na Waajiri wao kwenda
kuhakiki takwimu mbalimbali za kielimu zinazowasilishwa.
Kwa
Mujibu Mkuu Mkoa wa Simiyu mkanganyiko umeonekana katika takwimu za wanafunzi
wa Elimu ya Sekondari kwa Mkoa mzima
zilizowasilishwa ambapo idadi ya
wanafunzi wanaoletewa ruzuku ya elimu bila malipo kwa mwezi Januari hadi Julai
2016 ni 41,616 ambayo ni tofauti na idadi ya wanafunzi baada ya uhakiki Agosti 2016 ya 39,283 na wanafunzi waliochangiwa fedha za UMISETA
mwaka 2016 ni ambayo ni 41,492.
Naunga mkono naziombea kwa Mungu zizae matunda jitihada hizo za RC kuiokoa elimu Simiyu!
ReplyDeleteAsante Bwana Myovela kwa kutambua na kuunga mkono jitihada za Mkuu wetu wa Mkoa, Mhe. Anthony John Mtaka za kuinua kiwango/ubora wa Elimu mkoani Simiyu.
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete