Baada
ya kufanya uhakiki wa Wanafunzi Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umebaini uwepo wa
wanafunzi hewa 2331 katika shule za
Sekondari za Mkoa huo.
Taarifa
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipozungumza na
Walimu Wakuu na Waratibu Elimu Kata mara baada ya kuwakabidhi Vishikwambi (Tablets)
vilivyotolewa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la EQUIP Tanzania kwa ajili
ya utunzaji wa Takwimu muhimu za Sekta ya Elimu.
Mtaka
amesema kati ya Halmashauri sita za Mkoa huo, Ni Halmashauri ya Wilaya ya
Bariadi tu ambayo haina wanafunzi hewa
wakati Halmashauri ya Wilaya ya Busega ikiwa na wanafunzi hewa 110, Itilima 2137, Maswa 14, Meatu 125 na Halmashauri ya
Mji wa Bariadi 439.
.
Kufuatia
kuwepo kwa wanafunzi hewa Mkuu wa Mkoa huo amesema, Serikali Mkoani humo
imepanga kufanya mabadiliko ya Wakuu wa Shule za Sekondari katika Mkoa mzima,
wakati taratibu za kinidhamu zikiendelea kwa wakuu wa shule waliotoa takwimu za uongo za wanafunzi katika
shule zao, wakati kwa upande wa shule za Msingi, mabadiliko yatafanyika baada
ya kumaliza mtihani wa darasa la saba.
Mtaka
amesema kabla ya uteuzi wa wakuu wa shule na walimu wakuu utafanyika upekuzi
(vetting) kwa wale watakaopendekezwa ili kujiridhisha kama wahusika wana sifa na
uwezo wa kuendesha shule na kusimamia fedha za Serikali zinazopelekwa shuleni
kwa ajili ya kugharama elimu ya bila malipo.
“
Serikali inaendelea kupelekea fedha moja kwa moja katika akaunti za shule, kwa
hiyo mkuu wa shule au mwalimu mkuu ni afisa masuuli katika shule yake. Ipo haja
kwa sisi kujiridhisha kama Serikali kuwa anayeteuliwa kushika nafasi ya
kuongoza shule ana uwezo na sifa ya
uadilifu. Sitakuwa tayari kuona katika mkoa huu kuna walimu wakuu wazoefu wa
kula fedha za Serikali na wakaendelea kuongoza shule” alisema Mtaka.
Akitoa
shukrani kwa Shirika la EQUIP Tanzania, Mkuu wa Mkoa amesema Shirika hilo
limekuwa msaada katika kutatua baadhi ya changamoto za Watendaji katika Sekta
ya Elimu mkoani Simiyu ikwa ni pamoja na
kuwawezesha Waratibu Elimu Kata kwa kuwapa pikipiki na kuwapa fedha za
mafuta shilingi 206,000 kwa kila mwezi pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu wakuu
na walimu wakuu wasaidizi.
Aidha,
Mtaka amesema analishukuru shirika hilo kuona umuhimu wa kutoa vishikwambi kwa
Walimu wakuu na Waratibu Elimu Kata ambavyo ameelekeza vitumike kutunza takwimu
sahihi za kieleimu ikiwemo idadi ya walimu na wanafunzi.
Kwa
upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amewataka Walimu Wakuu
na Waratibu Elimu Kata kuvitunza vishikwambi hivyo na kuvitumia kwa malengo
yaliyokusudiwa.
Naye
Mkuu wa EQUIP Tanzania Mkoa wa Simiyu, Phoebe Okeyo amesema Vishikwambi
hivyo vitawasaidia Viongozi wa Elimu
ngazi ya Mkoa, Wilaya na kata kupata taarifa za masuala mbalimbali
yanayofanyika shuleni.
“Sasa
hivi mtegemee kupata taarifa sahihi katika sekta ya Elimu kwa sababu ya hivi
vifaa tulivyovitoa leo, tumeanza kama pilot study kwa Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mara, Tabora, Dodoma,Lindi
na Kigoma. Tunatarajia kuongeza mikoa ya Katavi na Singida Januari, 2017”
alisema Okeyo.
Jumla ya Vishikwambi(tablets) 637 vimetolewa kwa Walimu wakuu 516 na Waratibu Elimu Kata 121 kutoka Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu, ambapo kila kimoja kina thamani ya shilingi 315,000/=
Jumla ya Vishikwambi(tablets) 637 vimetolewa kwa Walimu wakuu 516 na Waratibu Elimu Kata 121 kutoka Halmashauri zote sita za Mkoa wa Simiyu, ambapo kila kimoja kina thamani ya shilingi 315,000/=
Baadhi
ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu Kata wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Anthony Mtaka (hayupo pichani) mara baada ya kukabidhiwa Vishikwambi
vilivyotolewa na Shirika lisilo la
Kiserikali la EQUIP Tanzania, kwa ajili ya kutunza kumbukumbu na tawimu sahihi
za masuala ya elimu.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa) .(Picha na Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa)
|
Afisa
Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Nelasi Mulungu(kushoto) akipokea
Vishikwambi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka(kulia) kwa ajili ya
Walimu Wakuu na Waratibu Elimu Kata wa Halmasahuri hiyo. .(Picha na Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa)
|
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (kushoto) akizungumza na Walimu wakuu na
Waratibu wa Elimu wa Kata baada ya kukabidhiwa Vishikwambi na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka
(katikati)vilivyotolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la EQUIP Tanzania, kwa
ajili ya kutunza kumbukumbu na tawimu sahihi za masuala ya elimu(kulia)ni Afisa
Elimu Mkoa, Julius Nestory. .(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
|
Mkuu
wa EQUIP Tanzania Phoebe Okeyo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) katika mahojiano maalum mara ya kukabidhi vishikwambi 637 kwa alimu
wakuu 516 na Waratibu Elimu Kata 121 Wa Halmasahuri zote za Mkoa wa Simiyu, kwa
ajili ya kuwasaidia kutunza takwimu za masuala ya elimu. .(Picha na Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa)
|
Afisa
Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa (kushoto) akipokea Vishikwambi kutoka
kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka(kulia) kwa ajili ya Walimu Wakuu na
Waratibu Elimu Kata wa Halmashauri hiyo. .(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
|
0 comments:
Post a Comment