Na Stella Kalinga
*Mtaka
asema wako tayari*
*Dk Bamwenda afichua kuwa Simiyu inaweza*
*Dk Diallo asisitiza ushirikishwaji sekta binafsi*
Serikali mkoani Simiyu imeshauriwa
kuwekeza katika kilimo cha pamba kitakacholeta tija kwa haraka.
Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti
za Kiuchumi na kijamii(ESRF), Dkt.Gratian Bamwenda ametoa ushauri huo mjini
Bariadi leo katika kikao maalum cha kujadili Rasimu ya Mwongozo wa Uwekezaji katika
mkoa wa Simiyu kwa mwaka 2017, kilichowahusisha
viongozi wa mkoa huo na wadau wa maendeleo kutoka sekta binafsi
Dkt. Bamwenda amesema endapo wananchi
watatumia mbegu bora, mbolea, viuatilifu na kutumia huduma za maafisa ughani
ipasavyo, uzalishaji wa pamba mkoani humo utaongezeka kwa kiwango kikubwa.
Amesema Simiyu inashika nafasi ya 64
duniani kwa uzalishaji wa pamba na ili ifike katika kumi bora ni lazima gharama
za uzalishaji zikiwemo za nyenzo za uzalishaji zipungue na wakulima waelimishwe
na kuhimizwa kutumia mbegu bora na mbolea pale inapobidi.
"Kwa mujibu wa utafitituliofanya
tuliona eneo lingine linaloweza kuwatoa zaidi ni kilimo cha pamba ya oganiki
(pamba hai) ambayo inahitajika sana duniani na bei yake ni nzuri,"
alisema.
Dk Bamwenda kusisitiza kuwa kama
watazalisha pamba hai inaweza kuwaletea pato kubwa," alisema.
Ameongeza kuwa pamoja na kilimo cha
pamba mkoa wa Simiyu unayo fursa kubwa katika kilimo cha umwagiliaji kwa mazao
ya mpunga, mboga mboga, matunda pamoja na kilimo cha mazao ya mikunde ambayo
soko lake ni kubwa ndani na nje ya nchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, amesema pamba ya oganiki katika mkoa huo inalimwa katika wilaya
ya Meatu na inauzwa kwa bei nzuri hivyo viongozi wajipange kupata masoko ya
uhakika ya mazao mengine ya oganiki, hasa mboga mboga na matunda.
“Nisingehitaji kuwa kiongozi wa kuhamasisha
wananchi kulima mazao ya oganiki wakati sijui watayauaza wapi, kama kiongozi wa
mkoa na stakeholders wetu tunajipanga kuona tunapata masoko ili kujua wananchi
wetu wanalima mazao yapi ya oganiki hasa katika maeneo yenye uhakika wa maji”
alisema.
Mtaka amewataka viongozi wa mkoa wa Simiyu kubadili mtazamo wao katika
kufikia azma ya kuubadilisha mkoa huo katika kufanyia kazi ushauri wa wataalam
wakiwemo watafiti wa ESRF juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji katika wilaya
zote ili kutekeleza Sera ya Tanzania ya Viwanda katika kufikia Uchumi wa Kati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa
Mwanza ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Media Group Limited, Dk
Anthony Diallo, ameshauri Serikali ya Mkoa wa Simiyu kuwavutia kuwekeza
katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo kwa kutoweka urasimu usio wa lazima na
kuishirikisha sekta binafsi katika utekezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda.
Wakati huo huo Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu Ndg. Jumanne Sagini amewataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri mkoani
humo kupitia rasimu ya mwongozo wa uwekezaji wa ESRF ili kubaini maeneo ya
kipaumbele yaliyopo katika fursa za uwekezaji zilizoanishwa kwenye mwongozo.
"Sasa hivi tuko katika maandalizi
ya bajeti kaeni katika vikao vyenu vya mabaraza mpitie, angalieni namna ya
kuyaingiza yale yatakayowezekana katika mipango ya bajeti za Halmashauri,"
alisema.
Rasimu ya mwongozo wa uwekezaji Simiyu inalenga
kuongeza pato la mwananchi wa Simiyu kutoka dola za Kimarekani 3600 hadi 12,000
kwa mwaka ifikapo mwaka 2050.
Hello.
ReplyDeleteMimi ni Mr Rahel binafsi wakopeshaji mkopo ambao hutoa maisha wakati nafasi ya mkopo kwa watu binafsi, makampuni ya biashara, bima, nk Je, katika shida yoyote ya kifedha au katika haja ya mkopo wa kuwekeza au unahitaji mkopo kulipa bili yako kutafuta hakuna zaidi kama sisi ni hapa kufanya matatizo yako yote ya kifedha kitu cha zamani. Sisi kutoa kila aina ya mkopo katika dhehebu lolote fedha kwa kiwango cha 2% bila fee.I upfront wanataka kutumia kati hii kubwa ya kukufahamisha kwamba tuko tayari kukusaidia kwa aina yoyote ya mkopo kutatua kwamba tatizo.Kama yako ya kifedha ndiyo basi kupata nyuma sasa kupitia barua pepe (rahelcohranloan@gmail.com) kwa maelezo zaidi, wewe ni sana makala.