Thursday, February 2, 2017

WATUMISHI WA MAHAKAMA WAASWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Na Stella Kalinga
Watumishi wa idara ya mahakama wameaswa kufanya kazi zao kwa weledi pasipo kutia unajisi wadau wengine wa mahakama hususani jeshi la polisi.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya Mjini Bariadi, chini ya kauli mbiu"UMUHIMU WA UTOAJI WA HAKI KWA WAKATI KUWEZESHA UKUAJI WA UCHUMI".

"Ukikaa Mtaani utasikia huyo hapo alikuwa mwizi akakamatwa akapelekwa polisi akaachiwa, kumbe hawajui kuwa kaachiwa mahakamani aliposhinda kesi lakini mdau wenu mmoja analaumiwa sana, ni vizuri mkafanya kazi kwa weledi ili tafsiri ya wadau wenu kuwa kwenye mtazamo hasi kwa jamii uondoke", alisema.


Mtaka amesema kumekuwa na malalamiko mengi ya wananchi dhidi ya jeshi la polisi hata pale inapotokea mapungufu katika utendaji wa watumishi wa mahakama,  kwa kuwa baadhi yao hawajui kuwa baada ya mtu kupelekwa polisi hupelekwa mahakamani.

Amesema watoa haki wa mahakama wanatambulika kama wasomi (learned brothers and sisters) hivyo, wanapaswa kujiridhisha katika utoaji wa maamuzi yao ili wasiifedheheshe taaluma yao na mhimili wa mahakama kwa ujumla.

Aidha,ameipongeza idara ya mahakama na wadau wengine wakiwemo viongozi wa dini,jeshi la polisi kwa mchango wao wa kubadili taswira ya mkoa huo  katika kushughulikia kesi za uhalifu zikiwemo za kukatana mapanga kwa visasi,mauaji ya vikongwe na mauaji ya albino na kufanya mkoa huu kusikika kwa mema.

Ameongeza kuwa mkoa wa Simiyu umejitambulisha kama mkoa wa tofauti ktk masuala mbalimbali ya kiuchumi na Mhe.Rais amewataka wengine kujifunza Simiyu, hivyo akawataka watumishi wa mahakama kujituma na kutoa haki kwa wakati ili wengine waje kujifunza pia katika utendaji wa Mahakama.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) ambaye ni wakili, Polycarp Mtega amesema mambo yanayochelewesha utoaji wa haki kwa wakati ni pamoja na ukosefu wa maadili kwa baadhi ya watoa haki, upungufu wa watoa haki katika mahakama,watuhumiwa kutofikishwa mahakamani toka gerezani kwa misingi ya kisiasa, ukosefu wa mashahidi na kesi kuahirishwa pasipo sababu za msingi.

Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi(M) Mhe. John Nkwabi amesema Mahakama ya Tanzania imejipanga kuhakikisha wadau wote wanapata haki zao kwa wakati ili wajikite katika shughuli za kiuchumi badala ya kupoteza muda mwingi mahakamani, ambapo ameeleza kuwa jumla ya kesi 692 zimesikilizwa kwa mwaka 2016, pamoja na upungufu wa mahakimu uliopo mkoani Simiyu.

Nkwabi ametoa wito kwa wananchi wenye kesi kufika mahakamani kila wanapohitajika badala ya kusubiri kutumiwa hati za kuitwa mahakamani.


Siku ya sheria nchini huadhimishwa kila wiki ya kwanza ya mwezi Februari kila mwaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka  akizungumza na Watumishi wa Mahakama na wanannchi wa Mkoa huo, katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi (M)Mhe. John Nkwabi akiwasilisha hotuba yake kwa Mkuu wa Mkoa huo , Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani)  katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi
Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Yeriko Mlekano akiwasilisha hotuba yake kwa Mkuu wa Mkoa huo , Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani)  katika maadhimisho ya siku ya sheria  hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika  viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.

Mwakilishi wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) ,Mhe.Polycarp Mtega hotuba kwa niaba ya chama hicho mbele ya Mkuu wa Mkoa huo , Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Baadhi ya Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo katika Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo , Mhe.Anthony Mtaka katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (wa pili kulia)  na viongozi wengine wa mahakama na Serikali wakifuatilia burudani kutoka kwa waimbaji wa kwaya ya AICT Bariadi (hawapo pichani) katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika  viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa dini walioshiriki na kutoa sala maalum katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.

Mchungaji wa Kanisa la AICT Bariadi akitoa sala maalum ya kuliombea Taifa, Viongozi na watendaji wa mihimili yote katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka Mtaka (wa pili kulia)  na viongozi wengine wa mahakama na Serikali wakiwa kwenye  picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka Mtaka (wa tatu kulia)  na viongozi wengine wa mahakama na Serikali wakiwa kwenye  picha ya pamoja katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka Mtaka (wa tatu kulia)  na viongozi wengine wa mahakama na Serikali wakiwa kwenye  picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama mbalimbali za mkoa huo katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka Mtaka (wa tatu kulia)  na viongozi wengine wa mahakama na Serikali wakiwa kwenye  picha ya pamoja na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo za mkoa huo katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama mbalimbali katika Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo , Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama mbalimbali katika Mkoa wa Simiyu  na wananchi wa Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo , Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa Mahakama mkoa wa Simiyu kabla ya kuanza kwa sherehe za maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakama mbalimbali katika Mkoa wa Simiyu  na viongozi wa Serikali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo , Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.
Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la AICT Bariadi wakitoa burudani ya wimbo maalum wa Siku ya Sheria nchini katika maadhimisho ya siku hiyo, yaliyofanyika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.


 Sheikh wa Mkoa wa Simiyu,Mahamuod Kalokola akitoa sala maalum ya kuliombea Taifa, Viongozi na watendaji wa mihimili yote katika maadhimisho ya siku ya sheria hapa nchini, yaliyofanyika viwanja vya Mahakama ya Wilaya, Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!