WANARIADHA WA KIMATAIFA
KUSHIRIKI MASHINDANO YA KILI -MARATHON
Na
Stella Kalinga
Wanariadha wawili wa Kimataifa
kutoka katika jimbo la Hanover Nchini Ujerumani
wanatarajia kushiriki mashindano ya
riadha ya Kilimanjaro Marathon yatakayofanyika
Februari 26 mwaka huu, Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni moja kati ya
ushirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania.
Akifungua mafunzo ya
siku moja ya makocha na walimu wa michezo
mbalimbali kutoka mikoa minne ya kanda
ya Ziwa ,Rais wa Shirikisho la Riadha Nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka aliwataja wanariadha hao kuwa ni Christin Kulgemeyer
na Stephan Immega ambao watakuwa chachu ya kuwatia moyo wanariadha wengine
wa Kitanzania
.
Mtaka alibainisha kuwa
licha ya kushiriki mashindano hayo,wanariadha hao watapata fursa ya kuona Mlima
Kilimanjaro ikiwa ni moja kati ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake.
Aidha katika ufunguzi
huo Mtaka aliwataka makocha na viongozi
wa michezo mbalimbali kutoka mikoa ya Simiyu,Mwanza,Mara na Shinyanga kuyatumia
mafunzo hayo vizuri ili kujenga mtazamo chanya wa kimichezo katika mikoa ya
kanda ya Ziwa.
Aliongeza kuwa viongozi
hao wanapaswa kutambua kuwa riadha inakuwa ni moja kati ya njia ya kuitangaza
nchi kwa Mataifa nyingine ikiwa ni pamoja na kujenga ushirikiano baina ya Mkoa
wa Simiyu na jimbo la Hanover Nchini Ujerumani.
“Kupitia wanariadha hawa
imekuwa faraja kuona Tanzania riadha
inakuwa ni sehemu ya kuitangaza nchi yetu, kwa sababu hawa wanariadha wametoka
Ujerumani kuja kushiriki mashindano ya Kilimanjaro Marathoni mwaka huu 2017,
ikiwa ni pamoja na kuwa sehemu ya ushirikiano kati ya Mkoa wa Simiyu na Jimbo
la Hanover Ujerumani” alisema
Hata hivyo wanariadha
hao wameonyesha kufurahishwa na kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimichezo baina
ya nchi yao na Mkoa wa Simiyu kwani wanaamini watajifunza mengi kutokana na
kubadilishana uzoefu na kuifanya micheczo kuwa na nafasi kubwa Duniani.
0 comments:
Post a Comment