Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus
Sangu amewataka Vijana kutokubali kutumiwa kuleta
vurugu, chuki na mafarakano hapa nchini.
Askofu
Sangu ametoa wito huo wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika
Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
“......Maandiko
Matakatifu yanasema Vijana wana nguvu; kwa
hiyo nawasihi vijana popote pale mlipo muwe chimbuko la Upendo, furaha na amani;
watu wengine wasitumie nguvu zenu vijana kuleta chuki, fitina na mafarakano,
muwe macho” alisema Askofu Sangu.
Askofu
Sangu amewaasa waumini wa Kanisa hilo kuishi maisha mema ambayo hayatakuwa chanzo
cha mateso kwa watu wengine katika familia, jumuiya , jamii wanaoishi na Taifa kwa
ujumla.
Aidha,
amewataka Watanzania wote kupinga na kukemea mauaji ya watu wenye ualbino kwa
kuwa wanayo haki ya kuishi kama watu wengine na watu wote wameumbwa kwa mfano
wa Mungu.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa wito kwa Kanisa kuwa na
mtazamo wa kuisaidia nchi katika
kupambana na tatizo la ajira hususani kwa
vijana.
Ameongeza kuwa
ni vema Kanisa liyavae maneno ya Mhe.Rais kuhusu Ujenzi wa Tanzania ya Uchumi wa Kati na
kuona namna linavyoweza kushiriki katika kufikia Tanzania Mpya, kwa kuimarisha
Idara za Kanisa na Vyama vya Kitume na kuzijenga idara
na vyama hivyo katika mtazamo
wa Kiujasiriamali.
“Kanisa
lione namna gani WAWATA tulionao wanakuwa WAWATA wa miradi, VIWAWA wanakuwa wa
miradi, TYCS wa miradi, lakini sasa Vyama vyetu vya Kitume navyo pia vianze
kujielekeza kusaidia Kanisa kwenye eneo la miradi”amesema Mtaka.
Mtaka amesema
upo umuhimu wa kufanya semina za Ujasiriamali kwa vijana, wanawake na Vyama vya
Kitume katika Kanisa na waumini wote kwa
ujumla ili kuwa na waumini waliojengwa kiuchumi na wanaoendana na mtazamo wa
Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati.
Akiwa katika Ziara yake Mkoani Simiyu, Mhashamu Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus
Sangu , Jumamosi Septemba 02 alizindua Parokia mpya ya Mtakatifu Luka iliyopo Mjini BARIADI, sambamba na kutoa kipaimara na leo ametoa
kipaimara kwa vijana 164, katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu
John Mjini Bariadi.
Mhashamu
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus
Sangu akiongoza Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki
Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Waumini wa Kanisa Katoliki
Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi katika Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara
iliyoongozwa na Mhashamu Askofu wa
Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA
Liberatus Sangu.
Mhashamu
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus
Sangu akiwapaka mafuta vijana wa Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya
Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Mhashamu
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus
Sangu akiwabariki vijana wa Kipaimara katika Ibada ya Sakramenti ya
Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Baadhi ya
Vijana waliopata Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu John Mjini Bariadi wakiimba katika ibada .
Kwaya ya
Shirikisho ikiimba katika Ibada ya
Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika
katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi.
Mhashamu
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus
Sangu akiingia katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini
Bariadi ambapo aliongoza Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (mwenye shati jeupe) na Mkewe Neema
Mbiha(kulia) wakifuatilia mahubiri wakati wa Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika
Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi iliyoongozwa na Mhashamu
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
Vijana wa
Kipaimara (wenye sare ya rangi nyekundu) katika Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu John Mjini Bariadi wakiingia
Kanisani kwa ajili ya ibada ya Sakramenti hiyo, ambayo iliongozwa
Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu.
Mhashamu
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus
Sangu akizindua Kitabu cha “MWANZO WA KUWA TAJIRI” wakati wa Ibada ya Sakramenti
ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi, kilichoandikwa
na Muumini wa Kanisa hilo Ndg.Vincent Mabula Jilala.
Mhashamu
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus
Sangu (katikati), Paroko wa Parokia ya Mtakatifu John Mjini Bariadi Padre
Kizito(kulia) Nyanga na Mapadri wengine wakifuatilia Ujumbe wa Mkuu wa Mkoa wakati wa
Ibada ya Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu
John Mjini Bariadi.
Baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John wakiwa katikaIbada ya Sakramenti ya Kipaimara iliyoongozwa na Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la SHINYANGA Liberatus Sangu (hayupo pichani)
0 comments:
Post a Comment