Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amepewa tuzo ya cheti na Asasi ya
Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ikiwa ni alama ya kutambua mchango wake
na kazi za kizalendo na maendeleo
anazozifanya Mkoani humo.
Akikabidhi
tuzo hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa, Mwenyekiti wa AWAMATA Mkoa
wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo
amesema Asasi hiyo imehamasika kutoa tuzo ya cheti kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
kwa sababu ni mzalendo na amekuwa akifikiri juu ya maendeleo ya wananchi na namna
mbalimbali za kuzalisha ajira kwa vijana.
Amesema
Mhe.Mtaka ni moja ya viongozi wabunifu sana na kama kiongozi kijana amekuwa na
maono makubwa yenye manufaa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla,
ambapo amehamasisha uanzishwaji wa viwanda katika Mkoa kupitia Kauli Mbiu ya
“Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” na
Kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega.
“Mhe.Mtaka
tumeanza kumfuatilia toka akiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Wilaya ya Hai mpaka
na baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, tumekaa kama asasi
tukashawishika kumpa tuzo hii, kwa sababu amekuwa anafanya kazi ya kizalendo na
maendeleo hasa anapoumiza kichwa kwa ajili ya kutengeneza ajira; tena kila
wilaya kwenye mkoa wake ina kitu cha kufanya” alisema Golyo.
Akipokea tuzo
hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameishukuru Asasi ya AWAMATA
kwa kutambua mchango wa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na akabainisha kuwa
imeipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Viongozi wa Mkoa huo pamoja na wadau wote wanaounga
mkono juhudi za Serikali katika maendeleo ya Mkoa na wananchi kwa ujumla.
Mtaka amesema
viongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataendelea kujenga
nuru ya matumaini kwa vijana ambao matarajio yao makubwa ni kuona kuwa wanapata
kitu cha kufanya ili waweze kuendesha maisha yao.
Ameongeza kuwa
miradi mingi inayoendelea ya Kiwanda cha Chaki, kiwanda cha kusindika maziwa na
mingine inayofanywa katika ngazi ya viwanda vidogo vidogo ilianzishwa kwa
sababu, mkoa unataka kujenga utamaduni kwa wananchi hususani vijana kujua
kwamba wanaweza kuthubutu kwa kuanzia ngazi ya chini.
“ Pale Mkula
Busega tulianza na vijana waliokuwa wanatengeneza viatu pair mbili tumewapa
mtaji wa milioni 12 wameongeza uzalishaji na tumeomba Baraza la uwezeshaji
wananchi Kiuchumi watawapa fedha ili wanunue mashine kubwa, pia tunajipanga kwa
kilimo cha umwagiliaji; tunataka kuwa Mkoa ambao wananchi wake wana kitu cha
kufanya na wanakiona kwenye vitendo badala ya kukiona kwenye hotuba nzuri.”
Katika hatua
nyingine Mtaka amewaambia viongozi wa AWAMATA kuwa, pamoja na kutoa tuzo kwa
viogozi kama walivyofanya kwake wanapaswa pia kuwakosoa viongozi hususani
vijana bila kuwaonea (kuwakosoa katika haki) pale wanapoona hawafanyi vizuri,
hii itawasaidia kuthibitisha dhamira ya Mhe.Rais ya kuwateua, maana ya kupewa
uongozi katika kipindi hiki na kubeba dhamana kwa vizazi vijavyo.
Wakati huo huo
ametoa wito kwa Viongozi wenzake vijana kutimiza wajibu wao, kuepuka maneno yanayowasahaulisha
walikotoka wanapozungumzia maisha ya vijana wenzao na kukubali kukosolewa, ili
wajengwe kuwa viongozi wazuri wa leo na vizazi vijavyo; kwa kuwa matarajio ya
Rais katika kuwateua ni kuwa na kizazi endelevu kwenye uongozi wa nchi.
Asasi ya Wazalendo
na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ni asasi ya Kiraia inayojishughulisha na uelimishaji
wa uzalendo kwa Watanzania na kufundisha mbinu za kujitegemea ili kuondokana na
umaskini pia inatoa tuzo kwa watu wanaofanya vizuri masuala mbalimbali ya
kizalendo na kuwasaidia wananchi kutoka katika umaskini.
Mwenyekiti
wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Ndg. Joseph Gimonge Golyo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony
Mtaka, tuzo ya cheti kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWAMATA Taifa, ambayo imetolewa
kwa Mkuu huyu wa mkoa kama alama ya kutambua kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani
humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akionesha tuzo ya cheti aliyokabidhiwa
na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua
mchango wake na kazi za kizalendo na
maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Kutoka
kulia Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka, Katibu wa AMAWATA mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo na Afisa
Uhusiano wa AWAMATA, Ndg Shushu Joel wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya kukabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa kwa Mhe.Mtaka kama alama ya kutambua mchango
wake na kazi za kizalendo na maendeleo
anazozifanya Mkoani humo
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu(wa tatu kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa AWAMATA na wadau wengine
wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya Mkuu huyo
wa Mkoa kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo
Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua kazi
za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa waSimiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akipongezwa na Katibu wa Asasi ya
Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA)
Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo mara baada ya kukabidhiwa
tuzo ya cheti na Asasi hiyo ngazi ya Taifa kama alama ya kutambua mchango na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani
humo.
Mkuu
wa Mkoa waSimiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
Afisa Vijana, Zena Mchujuko(kushoto) naAfisa Habari(kulia) wote watumishi
katika Ofisi yake mara baada kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na
Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani
humo.
Mwenyekiti
wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Ndg. Joseph Gimonge Golyo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(hayupo pichani)
kabla ya kumkabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa na Asasi hiyo Ngazi ya Taifa, kama alama ya
kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani
humo
Katibu
wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo
akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(hayupo pichani) kabla ya kumkabidhi
tuzo ya cheti iliyotolewa na Asasi
hiyo Ngazi ya Taifa, kama alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani
humo.
0 comments:
Post a Comment