Baada
ya mikakati ya upanuzi wa kiwanda cha kutengeneza chaki Wilayani Maswa, Mkoa wa
Simiyu umejipanga tena kufanya upanuzi wa Kiwanda cha kusindika Maziwa
kilichopo Wilayani Meatu na Ujenzi wa kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili
wilayani Busega.
Hatua
hiyo imefikiwa kufuatia zoezi la upembuzi yakinifu kwa viwanda hivyo
lililofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa Ufadhili
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP), kukamilika na taarifa yake
kuwasilishwa kwa Viongozi na wadau wa Maendeleo Mkoani Simiyu katika kikao
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Akiwasilisha taarifa ya Upembuzi
Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Wilayani Meatu, Profesa Lusato
Kurwijila kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) amesema Tanzania inazalisha
maziwa lita bilioni 2.1 kwa mwaka, lakini yanayopelekwa viwandani kusindikwa ni
asilimia tatu ya maziwa yote, kutokana na ukosefu wa miundombinu ya kukusanyia
maziwa.
Amesema upanuzi wa kiwanda cha
Maziwa Meatu ni mradi unaotekelezeka hivyo ni vema ukafanyika uwekezaji katika ufugaji
wa kisasa ili kupata maziwa ya kutosha, miundombinu ya kukusanyia na kupozea maziwa, kuwahamasisha wafugaji kuunda vyama vya
ushirika ambavyo vitamiliki na kuendesha vituo vya kukusanyia maziwa na kutoa
ajira kwa wananchi hususani vijana na wanawake.
Akizungumzia uanzishwaji wa
Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, Mtaalam wa Bustani na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine(SUA) Profesa Theodosy Msogoya
amesema, mradi huo unaweza kutekelezwa kwa mafanikio, hivyo ametoa wito kwa Serikali
kuajiri watalaam wa Bustani na kuwahamasisha wakulima kujiunga katika vikundi
ili waweze kukopesheka.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine(SUA) Profesa Jeremia Makindara amesema, uwepo wa fursa mbalimbali ikiwa
ni pamoja na utashi wa kisiasa,upatikanaji wa malighafi, nguvu kazi, maji,
kiwanda kujengwa katika njia kuu ya usafirishaji (barabara ya Mwanza-Musoma), upatikanaji
wa soko la uhakika kutasaidia kukiletea kiwanda hicho faida.
Kwa upande wao Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya na Mkurugenzi wa Wilaya ya
Meatu, Ndg. Fabian Manoza wamesema, viwanda hivyo vitakuwa vyanzo vipya vya
mapato kwa Halmashauri zao na kuwasaidia wananchi kupata ajira na kukukuza
uchumi wao.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi
wa UNDP hapa nchini Ndg, Amoni Manyama ametoa wito kwa Serikali Mkoani Simiyu
kuona namna ya kuwashirikisha wanufaika wa TASAF katika maendeleo ya viwanda na
kuhakikisha kuwa makundi yote hususani wanawake yanashirikishwa na kunufaika na
uanzishwaji wa viwanda hivyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka
amesema watayafanyia kazi yote yaliyoanishwa katika Tafiti zilizofanywa na
Watalaam hao kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine(SUA)na upembuzi yakinifu huo na kuyaweka katika matendo.
“Tumekuwa ni mkoa ambao tunawashirikisha
wataalam kutoka katika vyuo vyetu, dhamira yetu ni kuona matokeo na position(Nafasi)
yetu kama Mkoa ni kujipanga kimkakati na
mpango kazi wetu, dira ya mkoa na tunasema kwenye miaka mitatu tutatekeleza” alisema
Mtaka.
Aidha, Mtaka amesema Serikali Mkoani
humo iko tayari kushirikiana na sekta binafsi katika uwekezaji, hivyo ametoa
wito kwa Watanzania walio tayari kuwekeza Mkoani humo kwa kushirikiana na
Halmashauri ambazo zimeanzisha miradi hiyo ya viwanda.
Sambamba na hilo amezishukuru
Taasisi za Fedha zilizo tayari kufanya kazi na Mkoa wa Simiyu katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ukiwepo mradi wa kilimo cha Umwagiliaji wilayani
Busega hususani Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) ambayo imesema iko tayari
kufanya kazi na Mkoa huo, katika miradi mbalimbali ya Kilimo.
Upembuzi yakinifu wa ujenzi wa
kiwanda cha kusindika nyanya na pilipili wilayani Busega na Upanuzi wa Kiwanda
cha Maziwa wilayani Meatu uliofanywa na Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam(UDSM) na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) chini ya Taasisi ya Utafiti
wa Kiuchumi na Kijamii(ESRF) ulianza kufanyika Mwezi Julai mwaka huu na
kukamilika mapema mwezi Septemba.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza na Viongozi na wadau wa
maendeleo mkoani humo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha
taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na
Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi
ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi wa
Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini Ndg.Amoni Manyama (kushoto)
akizungumza na Viongozi na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu katika kikao
kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi
Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na
Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa
Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) uliofadhili na shirika hilo.
Mtaalam wa
Maziwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA), Profesa Lusato Kurwijila
akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa
Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF)
Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi
na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Mtaalam wa
Uchumi na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Mutahyoba Baisi
akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa
Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF)
Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi
na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Mtaalam wa Kilimo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine(SUA) Profesa Theodosy T. Msogoya akiwasilisha taarifa ya Upembuzi
Yakinifu wa Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya
Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa
Mkoa wa Simiyu.
Mhandisi na
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA) Profesa Benard
Chove akiwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Upanuzi wa Ujenzi wa
Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa
Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Mkurugenzi wa
Vipind na uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba(kulia) akichangia hoja
katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya
Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega
na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa
Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mhe.Festo
Kiswaga.
Mhadhiri kutoka
Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA), Dkt. Jeremia Makindara akizungumza na
waandishi wa Habari baada ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa
Upanuzi wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, uliofanywa na Taasisi
ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa maendeleo wa
Mkoa wa Simiyu.
Mkuu
wa Wilaya ya Meatu , Mhe.Dkt.Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao kilichofanyika
Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi
wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha
Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF)
Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndg.Fabian Manoza akichangia hoja
katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya
Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega
na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa
Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkuu
wa Wilaya ya Busega Mhe.Tano Mwera
akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha
taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na
Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi
ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko akichangia
hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa
ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili
Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti
wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi wa
FURSA, Suma Mwaitenda akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi
kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha
kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa
na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buseg, Ndg.Anderson Njiginya akichangia hoja katika kikao kilichofanyika
Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi
wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha
Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na
Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yaItilima, Ndg.Mariano Mwanyigu akichangia
hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa
ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili
Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti
wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP).
Baadhi ya
viongozi na wadau wa maendeleo Mkoani Simiyu wakifuatilia taarifa ya Upembuzi
Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na
Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa
Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), iliyowasilishwa katika kikao maalum Mjini Bariadi.

Meneja wa
Kitengo cha Kukuza Biashara kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kuwasilishwa kwa taarifa ya Upembuzi
Yakinifu wa Upanuzi wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, uliofanywa
na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa
maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo
Kikuu cha Kilimo (SUA) wakifuatilia mjadala wa viongozi na wadau wa maendeleo
Mkoani Simiyu, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi baada ya kuwasilishwa
kwa taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa
Upanuzi wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili, uliofanywa na
Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwa viongozi na wadau wa
maendeleo wa Mkoa wa Simiyu.
Msanii wa Muziki
wa Kizazi Kipya Nickson Simon kutoka FURSA akichangia hoja katika kikao kilichofanyika
Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi
wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha
Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na
Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Daktari
wa Mifugo wa Halmashuri ya Wilaya ya Itilima Faustine Musoke akichangia hoja
katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya
Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha kusindika Nyanya na Pilipili Busega
na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa
Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP).
Ndg.Hassan Ngoma
kutoka FURSA akichangia hoja katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi kwa
ajili ya kuwasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu wa Ujenzi wa Kiwanda cha
kusindika Nyanya na Pilipili Busega na Upanuzi wa Kiwanda cha Maziwa Meatu, uliofanywa
na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) Kwa ufadhili wa
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
0 comments:
Post a Comment