Ninafahamu kuwa leo tarehe 06/09/2017 vijana wetu walioanza
darasa la Saba wanaanza mitihani yao ya siku 2 ikiwa ni hatua muhimu ya
kuhitimu Elimu ya msingi.
Najua kwamba walimu, wazazi, walezi na viongozi wa ngazi zote
wametimiza wajibu wao na wanafunzi pia wamejiandaa vizuri. Nachukua nafasi hii
kuwaombea ufanisi vijana wetu wote wanaofanya mitihani kesho na
keshokutwa.
Nawatakia heri watoto wote wa Mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa
ujumla. Nawaombea utulivu wa akili na umahiri katika kujibu maswali yote ili
wapate ufaulu ulio bora na hivyo kuanza vema safari yao ya kitaaluma.
Aidha, wasimamizi wote wafanye kazi hiyo kwa uaminifu na
uadilifu mkubwa ili kuwa na matokeo yanayoaminika. Baraka za Mungu ziwe kwenu
nyote.
Jumanne
Abdallah Sagini
Katibu Tawala Mkoa Simiyu
06/09/2017
Katibu Tawala Mkoa Simiyu
06/09/2017
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Abdallah Sagini
0 comments:
Post a Comment