Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Mhe.Angelina Mabula amezitaka Halmashauri mkoani Simiyu kutumia
Wataalam wake kupima maeneo ili wananchi waweze kupata hati miliki ya maeneo
yao na kupunguza adha mbalimbali hususani migogoro.
Mhe.Mabula ameyasema hayo wakati wa ziara yake
Mkoani Simiyu iliyokuwa na lengo la kukagua jengo litakalotumika kama Ofisi ya
Kanda ya Ardhi ya Simiyu na kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyotoa wakati
wa ziara yake mwezi Agosti mwaka jana Mjini Bariadi.
Amesema
ikiwa kuna Halmashauri inahitaji kupima viwanja na mashamba na ina watumishi
wachache katika Idara ya Ardhi ufanyike utaratibu wa kuomba watumishi kutoka
katika halmashauri nyingine ili waweze kuungana na kuweka kambi katika Halmashauri
husika wafanye kazi ya kuwahudumia wananchi wengi kwa wakati mmoja.
“
Hatuna wataalam wa kutosha kuweza kupima viwanja vingi kwa wakati mmoja katika
Halmashauri, lakini tunao wataalam katika Mkoa husika ambao tulishasema kama
kuna uhitaji wa kupima maeneo katika Halmashauri moja wataalam wote ndani ya
mkoa wakusanywe waweke kambi hapo mpaka hiyo kazi iishe , wakimaliza wanahamia wilaya
nyingine” alisisitiza Mabula.
Ameongeza
kuwa Halmashauri yoyote itakapoona ina uhitaji wa watalaam kutoka Ofisi ya
Kanda kwa ajili ya kuongeza nguvu katika zoezi la upimaji, Ofisi hiyo ipo
tayari kufanya kazi na Halmashauri yoyote itakayoomba.
Aidha,
amezitaka Halmashauri mkoani Simiyu kupima maeneo yote ya Mjini pamoja na
maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na uwekezaji.
Kwa
upande wake Kaimu Kamishna wa Kanda ya Ardhi ya Simiyu, Ndg. Makwasa Biswalo ametoa
wito kwa Watalaam mkoani humo kuona namna ya kutenga eneo la mipango miji katika
eneo lililopitiwa na barabara ya lami ya kilomita 70 kutoka Bariadi mpaka Lamadi(kilomita
kadhaa kwenye kila upande wa barabara) ambalo ni eneo zuri kwa ajili ya uwekezaji.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema ameshazungumza na Watendaji
wa Halmashauri zinazopitiwa na barabara hiyo ya Bariadi-Lamadi(KM 70) kuwa, waone namna
Halmashauri hizo zinavyoweza kumiliki maeneo hayo walau kilomita moja kushoto
na kulia kwa barabara hiyo.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Mhe. Angelina Mabula(wa tatu kushoto) akiangalia
baadhi ya hati za kimila zilizoandaliwa kwa ajili wananchi wa Wilaya ya Bariadi
katika Ofisi ya Idara ya Ardhi ya Halmashauri hiyo, wakati wa ziara yake Mkoani
Simiyu.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Mhe. Angelina Mabula
akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani humo, (kushoto)
Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Mhe. Angelina Mabula alipokuwa Mkoani
humo kwa ziara ya siku moja.
Kaimu
Kamishna wa Ardhi Kanda ya Simiyu,Ndg.Makwasa Biswalo
akifafanua
jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi,
Mhe. Angelina Mabula Mkoani Simiyu,(kulia) Afisa Ardhi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bi.Grace Mgombera.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini akifafanua jambo wakati wa ziara ya
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Mhe. Angelina Mabula
Mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Idara ya Ardhi na Maliasili katika
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg.Mazengo Sabaya akifafanua jambo wakati wa
ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Mhe. Angelina
Mabula Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg.Abdallah Malela akifafanua jambo
wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula Mkoani Simiyu.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(kulia) akitoa
maelekezo kwa baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu baada ya kukagua Jengo la
Ofisi linalotarajiwa kutumika kama Ofisi ya muda ya Kanda ya Ardhi Simiyu,
wakati wa ziara yake Mkoani humo.
Baadhi
ya viongozi na wataalam wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula (hayupo pichani) wakati wa
ziara yake Mkoani humo.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(kulia)
pamoja na baadhi ya viongozi na Watalaam wa Mkoa wa Simiyu akitoka katika Jengo
linalotarajiwa kutumika kama Ofisi ya muda ya Kanda ya Ardhi Simiyu,
wakati wa ziara yake Mkoani humo, (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga.
0 comments:
Post a Comment