Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema njia nzuri ya
kufikia Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025 ni kupitia Uchumi wa Viwanda jumuishi.
Waziri
Mwijage ameyasema hayo alipozungumza na wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji
wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake Mkoani humo, ambapo alisisitiza juu ya Ujenzi
wa Uchumi wa Viwanda ulio imara, shindani na endelevu, utakaozingatia mambo
muhimu matatu ambayo ni soko, malighafi na teknolojia.
Amesema
lengo la Serikali ni kuhamasisha ujenzi
wa Uchumi wa Viwanda Jumuishi ambao unawahusisha watu wengi kupitia viwanda
vidogo na vya kati,vitakavyotumia malighafi zitakozozalishwa hapa nchini vilivyopo
katika maeneo mbalimbali nchini, ukiwepo
mkoa wa Simiyu ambao umeonekana kufanya vizuri katika eneo hilo.
“Safari
ya Simiyu imeanza vizuri na lengo la safari ni kuhamasisha Watanzania kujenga
uchumi wa viwanda jumuishi, viwanda ambayo malighafi yake inazalishwa na wananchi wenyewe, vitatoa ajira kwa wananchi
walio wengi, vitatumia malighafi asilia na kutoa mazao yenye matumizi makubwa”
alisema Mwijage.
Waziri
Mwijage amepongeza juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Simiyu katika Ujenzi wa
Uchumi wa Viwanda kupitia Falsafa ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja”
ambapo sasa umejipanga kuelekea kwenye “Kijiji Kimoja Bidhaa Moja”.
Ameongeza
kuwa mwaka 2018/2019 Serikali kupitia Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO)
litawasaidia wananchi kupata mafunzo ya ujasiriamali, uzalishaji na uchakataji,
ambapo ameuhakikishia Viongozi wa Mkoa wa Simiyu kuwa Ujenzi wa Ofisi ya SIDO ya
Mkoa huo eneo la Isanga Mjini Bariadi utakamilika kabla ya kuanza kwa vikao vya
Bunge la Bajeti mwaka 2018, kwa kuwa
fedha za ujenzi zipo.
Sanjali
na hilo Waziri Mwijage amewataka Maafisa Ushirika kuwahamasisha wananchi
kujiunga katika vikundi ili waweze kukopeshwa mitaji ya kuanzisha viwanda
vidogo na Serikali pamoja na Taasisi nyingine za Kifedha kwa kuwa ni rahisi
zaidi vikudi kufikiwa kuliko mtu mmoja mmoja.
Wakati
huo huo Mwijage amewataka watendaji wote wa Serikali kuondoa vikwazo na kuacha
urasimu unaoweza kuwakwamisha wawekezaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili
kuweza kuufikia Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Akiwasilisha
tarifa ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema ili
kuandaa mazingira mazuri yatakayowawezesha wawekezaji kuvutiwa na kuwekeza
mkoani humo, wametenga maeneo ya uwekezaji na madawati ya uwekezaji kwa kila Halmashauri
na timu mahsusi ya Mkoa ya kuanzisha na kuendeleza dhana ya Simiyu ya Viwanda
inayoongozwa na Katibu Tawala Mkoa.
Mwenyekiti
wa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, Njalu Silanga amesema wako tayari kuunga
mkono juhudi za Serikali kwa vitendo katika Ujenzi wa Viwanda vidogo na vya
kati na akaomba Meneja wa SIDO Mkoa atembelee viwanda vilivyopo ili aweze kutoa
ushauri juu kuboresha uendeshaji wa viwanda hivyo katika tija.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema kupitia SIDO mkoa huo unaweza
kufikia Uchumi wa Kati. “Tungehitaji kuwa ni Mkoa ambao value addition(kuongeza
thamani) itafanyika kupitia SIDO, mahali ambapo mtu mwenye milioni tatu
wakiungana kikundi cha walima alizeti wanaprocess(wanachaka) wenyewe mafuta”
alisema Mtaka.
Pamoja
na kuzungumza na wadau wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu,
Waziri Mwijage alifungua Jengo la muda la Ofisi ya SIDO Mkoa wa Simiyu lililopo
Mtaa wa Malambo Mjini Bariadi na kukagua eneo la ujenzi wa Ofisi mpya ya SIDO itakayojengwa
na SUMA JKT, ambayo inatarajiwa kukamilika kabla ya kuanza kwa vikao vya Bunge
la Bajeti mwaka 2018.
0 comments:
Post a Comment