Wizara ya Elimu pamoja na wadau wengine wa Elimu
wametoa vitabu 16,985 kwa shule za Sekondari za Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya matayarisho ya awali
ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza na elimu ya sekondari (baseline
course).
Akikabidhi vitabu hivyo kwa Maafisa Elimu wa Halmashauri
zote sita za Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka amesema vitabu
hivyo ni msaada mkubwa kwa Mkoa huo, vikitumiwa vizuri na walimu
wenye nia ya kufanya mapinduzi ya elimu na kuwasaidia wanafunzi kujua maana
halisi ya vitabu hivyo vitasaidia Mkoa
wa Simiyu kufikia malengo ya kiushindani katika Elimu.
Ameongeza
kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata vitabu pamoja na
mahitaji mengine ikiwa ni pamoja na madawati, walimu, vyumba vya madarasa
vinavyotolesheleza hivyo akasisitiza vitabu hivyo vikatumike kwa kusoma ili
viwasaidie.
“Vitabu
hivi mtakapogawiwa mkavitumie kwa ajili ya kusoma visiwe mapambo na kama
mwanafunzi hujui uliza, jibidiishe kujua kitabu hicho kinahusu nini na kama
hujaelewa muulize mwalimu ili kesho kwenye mtihani ufaulu kama wenzako
wananvyofaulu” alisema Mtaka.
Aidha,
Mtaka amewataka Maafisa Elimu mkoani humo kuzungumza na walimu kabla ya kugawa
vitabu hivyo ili vitakapogawiwa katika shule vigawiwe katika utaratibu mzuri utakowawezesha
walimu kuwasadia wanafunzi kuvitumia kwa manufaa.
Akitoa
taarifa juu mapokezi ya vikao hivyo Katibu Tawala Mkoa amesema Mkoa huo
umepokea jumla ya vitabu 16,000 kwa ajili ya wanafunzi na vitabu 985 kwa ajili
walimu(kiongozi cha mwalimu).
Akizungumza kwa
niaba ya Maafisa Elimu Sekondari mkoani humo,
Afisa Elimu Sekondari wa Halmahauri ya Mji Bariadi Mwl. Esthom Makyara amesema vitabu hivyo ni msingi mzuri kwa
wanafunzi wa kidato cha kwanza na Maafisa Elimu hao wanapaswa kuwaelekezaWakuu wa
shule kutofungia vitabu hivyo stoo
badala yake wanafunzi wapewe ili wavisome.
Naye Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Ndg.Charles Maganga
amesema Maafisa Elimu Sekondari wahakikishe vitabu hivyo vinagawiwa kwa wakuu
wa shule kabla ya shule kufunguliwa Januari 08, 2018, ili wanafunzi wa kidato
cha kwanza wanapoanza masomo wavikute shuleni.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari
Bariadi walioshuhudia zoezi la ugawaji wa vitabu hivyo kimkoa wamesema, vitabu
hivyo vitawasaidia wenzao wa kidato cha kwanza kujenga msingi mzuri wa maarifa ya jumla na lugha ya
Kiingereza.
Vitabu
hivi vimetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Msaada wa
Watu wa Marekani(UKAID) kupitia Mpango wa Taifa waKuinua Ubora wa Elimu hapa
nchini EQUIP-T.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya
matayarisho ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya
sekondari (baseline course), kwa Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji
Bariadi, Mwl. Esthom Makyara vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi
la ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu Sekondari na baaadhi ya
wanafunzi wa shule ya sekondari Bariadi(hawapo pichani), kabla ya kukabidhi
vitabu vya matayarisho ya awali ya kuwaandaa
wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari (baseline course), kwa
maafisa elimu wilaya vilivyotolewa na wadau mbaimbali wa Elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho
ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari
(baseline course), kwa Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Wilaya ya
Busega, Mwl. Jumanne Yasini vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la
ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akikabidhi vitabu vya matayarisho
ya awali ya kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari
(baseline course), kwa Afisa Elimu (Sekondari) wa Halmashauri ya Wilaya ya
Maswa, Mwl. Joseph Mashauri vilivyotolewa na wadau wa Elimu, wakati wa zoezi la
ugawaji wa vitabu hivyo lililofanyika kimkoa Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment