Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amemwagiza
Mkandarasi wa Kampuni ya China ya CCECC inayotekeleza mradi wa maji LAMADI
kuukamilisha kabla ya mwezi Septemba 2019.
MTAKA ametoa agizo hilo baada ya
kuukagua mradi huo unaoanzia katika kijiji cha KARAGO hadi LAMADI wilayani
BUSEGA na hadi kukamilika kwake unatarajiwa kunufaisha zaidi ya kaya elfu tano
za kata ya Lamadi.
“Matarajio ya Serikali utekelezaji
wa Mradi huu umalizike kabla ya Septemba
2019 ili uweze kukidhi mahitaji ya watu wa Lamadi na utumike vizuri na viongozi
wa CCM watakaoomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi katika Serikali za Mitaa
mwakani kundi utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo” alisema Mtaka.
Mbunge wa Jimbo la Busega Dkt Raphael
Chegeni pamoja na wananchi wa Lamadi wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza ahadi ya kuwapelekea maji wa mradi wa maji ambao
utawasaidia kupata huduma ya maji safi na salama iliyo ya uhakika.
Mradi
huo unaotekelezwa kwa miezi 24 unatarajiwa kugharimu jumla ya shilingi Bilioni
TISA
.
Katika hatua nyingine akiwa katika
Mkutano wa Hadhara katika kijiji cha LAMADI Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony
Mtaka ametangaza kuwa biashara zifanyike kwa saa 24 katika Eneo (centre) la Lamadi
Wilayani Busega.
“Eneo la Barabara Kuu
ya Musoma Mwanza kutoka Benki ya Azania Tawi la Lamadi mpaka eneo la mwisho
pale kwenye daraja letu, hili litakuwa
eneo mahususi la kufanya biashara saa 24” alisisitiza Mtaka.
Amewataka wakazi wa
Lamadi kuitumia kwa faida barabara Kuu ya Musoma-Mwanza na kituo(centre)
kikubwa kinachoyakutanisha magari yaendayo mikoani na nchi jirani kwa kufanya
biashara saa kama ilivyo kwa maeneo kama hayo katika mikoa mingine,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji wa Lamadi wakati alipotembelea mradi
huo jana, wilayani Busega.
Mhandisi Mshauri wa
Mradi wa Maji Lamadi, Baraka Alphayo(kulia) kutoka Kampuni ya EGIS EAU CONSULT akitoa
maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa pili kushoto) na viongozi wengine wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipotembelea
mradi huo jana wilayani Busega.
Mhandisi Mshauri wa
Mradi wa Maji Lamadi , Baraka Alphayo(kushoto) kutoka Kampuni ya EGIS EAU CONSULT akitoa
maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) wakati alipotembelea
mradi huo jana wilayani Busega(kattikati) Mbunge wa Busega, mhe.Dkt.Raphael Chegeni.
Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji Lamadi , Baraka Alphayo kutoka Kampuni ya EGIS EAU CONSULT akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto)wakati alipotembelea Ofisi zitakazotumiwa na Mamlaka ya Maji Lamadi jana wilayani Busega,(kulia)Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera.
Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji Lamadi , Baraka Alphayo kutoka Kampuni ya EGIS EAU CONSULT akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto)wakati alipotembelea Ofisi zitakazotumiwa na Mamlaka ya Maji Lamadi jana wilayani Busega,(kulia)Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera.
0 comments:
Post a Comment