Viongozi na wanachama wa Vyama vya
Ushirika wa Mazao -AMCOS Mkoani SIMIYU wamesema chanzo cha wakulima wa Pamba
kuchanganya mchanga na mafuta ya kenge kwa madai ya kuongeza uzito katika zao
hilo kinatokana na baadhi ya wanunuzi wasio waaminifu kuwaibia kupitia
mizani.
Hayo wameyasema katika majadiliano ya
namna ya uendeshaji vya Vyama vya Ushirika na uanzishwaji wa Chama Kikuu cha
Ushirika Mkoa wa SIMIYU mjadala ulioandaliwa ya Tume ya Maendeleo ya
Ushirika nchini.
Kikao baina ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Anthony Mtaka na viongozi na wanachama wa Vyama vya Ushirika wa Mazao -AMCOS
chenye lengo la kujadili changamoto zinazowakabili wakulima na uanzishwaji wa
Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa SIMIYU.
Katika mjadala huo wadau hao wamesema
udangangifu katika mizani ya kupima uzito wa Pamba umechangia kwa kiasi kikubwa
wakulima kutumia mbinu mbadala za kuongeza uzito
Moses Masalu Mwenyekiti wa chama cha
ushirika mhango halmashauri ya mji wa bariadi amesema kuwepo kwa wizi wa pamba
katika mizani za kupimia uzito kumesababisha wakulima wengi kutumia mbinu
mbadala za kuongeza uzito ili kufidia machungu ya kuibiwa pamba yao na makarani
wanapoenda kuuza pamba.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga
amesema kuchelewa kuanza kwa msimu wa pamba kunachangia kushuka kwa bei soko la
dunia kutokana na kugongana na mataifa mengine katika msimu na hivyo kupendekeza
kuanza april badala ya mei na juni.
Kwa upande wake Kaimu Mrajisi Masoko na
Uwekezaji Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini, EDMUND MASSAWE amesema nia ya
serikali ya kuimarisha ushirika nchini ni kuviwezesha vyama vikuu kununua
mazao ya wakulima.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amewasisitiza viongozi wa vyama hivyo kuwa
waadilifu .
Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa
SIMIYU kinatarajiwa kuundwa April mwaka huu kabla ya kuanza msimu wa ununuzi.
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Vyama vya Ushirika wa Mazao -AMCOS wakimsikilza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika kikao cha kujadili changamoto zinazowakabili wakulima na uanzishwaji wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa SIMIYU
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na wanachama wa Vyama vya Ushirika wa Mazao -AMCOS (hawapo pichani)katika kikao cha kujadili changamoto zinazowakabili wakulima na uanzishwaji wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa SIMIYU.
0 comments:
Post a Comment