Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ametoa
wito kwa Wakuu wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari Halmashauri za Wilaya
kuisadia jamii kuondokana na mila zilizopitwa na wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ametoa wito huo
katika tathimini ya elimu iliyofanyika katika Shule ya Msingi Lukungu Wilayani
Busega.
Ni kikao cha tathimini ya elimu Mkoa wa
SIMIYU kilichowakutanisha maafisa elimu na wakuu wa idara wa Halmashauri
SITA chenye lengo la kufanya taathimini ya kitaaluma na mikakati ya
ufaulu wa mitihani ijayo ya kitaifa.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mkoa wa
Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka anasema tathimini ya matokeo ya elimu ilenge kuangalia
changamoto zinazowakabili walimu sambamba na kuleta mabadiliko katika jamii.
Amesema jukumu lililombele yao ni kuhakikisha
wanaibadilisha jamii ya Simiyu ili iondokane na mila potofu zilizopitwa na
wakati ikiwemo ya kuwaadhibu walimu hadharani kwa kuwatandika viboko
almaarufu dagashida.
Kuhusu Wilaya ya MEATU
kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na
darasa la nne 2017 amewataka kuhakikisha wanabadilika ili kuuwezesha mkoa wa
simiyu kuingia kumi bora kitaifa.
‘Meatu punguzeni kuwa mkia mnatuaibisha
jitihidini muondoke huko alisema Mtaka.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu,
Julius Nestory amesema pamoja na changamoto zilizopo katika sekta
elimu lakini ufaulu umekuwa ukiongezeka .
Aidha amesema wametekeleza agizo la mkuu
wa mkoa la kulima zao la pamba katika shule za msingi na sekondari za
serikali ambapo jumla ya hekari 1,500 na
hekari 230 za mahindi ili kuwawezesha wanafunzi kupata chakula cha mchana
.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu wa Halmashauri za Mkoa huo (hawapo pichani) katika tathimini ya elimu iliyofanyika katika Shule ya Msingi Lukungu Wilayani Busega.
Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu,Mwl. Julius Nestory Maafisa Elimu wa Halmashauri za Mkoa huo (hawapo pichani) katika tathimini ya elimu iliyofanyika katika Shule ya Msingi Lukungu Wilayani Busega.
Baadhi ya Maafisa Elimu wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu wakimsikilizaMkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika tathmini ya Elimu iliyofanyika Wilayani Busega.
Baadhi ya Maafisa Elimu wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu wakimsikilizaMkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika tathmini ya Elimu iliyofanyika Wilayani Busega.
0 comments:
Post a Comment