Saturday, November 30, 2019

CWT KUJENGA KIWANDA CHA MIKATE LISHE SIMIYU


Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kinatarajia kujenga kiwanda cha mikate lishe kupitia kampuni yao inayosimamia Maendeleo ya Walimu ya biashara (TDCL), katika eneo la Ng’hami wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Akimkabidhi  Katibu wa Chama cha Walimu Nchini, Mwl. Deus Seif hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2), Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe amesema wilaya imetoa kiwanja hicho bure, ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda ambapo kumhakikishia upatikanaji wa malighafi ya kiwanda hicho (viazi lishe)
“Tumejipanga kuzalisha viazi lishe vya kutosha vitavyotumika kama malighafi ya kiwanda hiki na tayari wakulima wamepewa mbegu za viazi hivyo, niendelee kuwakaribisha CWT wilayani Maswa, kama kuna uwekezaji mwingine mnahitaji kufanya karibuni, hata kama ni tawi la benki yenu ile ya walimu tunawakaribisha sana,” alisema Dkt. Shekalaghe.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu amesema kukamilika kwa kiwanda hicho kutasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa lishe ambalo limekuwa ni changamoto kwa  Mkoa wa Simiyu.
Aidha, Mtaka amesisitiza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashautri na wataalam wa kilimo wahakikishe mbegu ya viazi lishe inapatikana kwa wingi ili wananchi wanapohitaji waipate
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Taifa, Mwl. Deus Seif amesema chama hicho kinaunga mkono sera ya Tanzania ya Viwanda huku akibainisha kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utaenda haraka kwa kuwa tayari kampuni ya CWT inayosimamia miradi imeshaanza kulifanyia kazi suala hilo.
Ameongeza kuwa pamoja na kujenga kiwanda cha mikate lishe, chama hicho pia kinatarajia kuchukua uwakala katika Kiwanda cha Chaki cha Maswa ili kusambaza chaki zinazozalishwa wilayani humo katika shule zote nchini.
MWISHO



 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe (mwenye tai kushoto) akimkabidhi Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif(mwenye suti nyeusi kulia) hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani humo  ambacho Halmashauri imekitoa bure kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe.


 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe (kulia) akiwaongoza viongozi mbalimbali kwenda katika kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani humo , kilichotolewa bure na Halmashauri kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanda hicho kati yake na Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif Novemba 29, 2019.


 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe  akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali katika kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani humo , kilichotolewa bure na Halmashauri kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja hicho  kati yake na Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif Novemba 29, 2019.


 Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani Maswa , kilichotolewa bure na Halmashauri kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja hicho  kati  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe na Katibu M wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif Novemba 29, 2019.  


 Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Simiyu, kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani Maswa , kilichotolewa bure na Halmashauri kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe,  kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja hicho  kati yake na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe Novemba 29, 2019.


 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe (mwenye tai kushoto) akimkabidhi Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif(mwenye suti nyeusi kulia) hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani humo  ambacho Halmashauri imekitoa bure kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza akizungumza kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja chenye ukubwa wa hekari mbili (2) kilichopo Ng’hami wilayani Maswa , kilichotolewa bure na Halmashauri kwa CWT kwa ajili ya kujenga kiwanda cha mikate lishe kabla ya makabidhiano ya hati ya kiwanja hicho  kati  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe na Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania, Mwl. Deus Seif Novemba 29, 2019


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!