Saturday, November 30, 2019

MASWA YAZINDUA MFUKO WA WALIMU KUWASAIDIA KUPATA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU

Wilaya ya Maswa imezindua mfuko wa walimu kwa lengo la kuwasaidia walimu ambao hawana sifa za kukopesheka katika taasisi zingine za fedha ili waweze kupata mikopo kwa riba nafuu.
Mfuko huo umezinduliwa na Katibu wa Chama cha Walimu nchini, Mwl. Deus Seif wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu zaidi ya 1400 wa shule za msingi 123 za wilaya hiyo kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019.
Akizungumza na mamia ya walimu walioshiriki katika uzinduzi huo, Seif amewaasa walimu kutambua thamani waliyopewa na viongozi wa wilaya na mkoa kwa kuendelea kuwajibika kwa uadilifu mkubwa.
“ Nitoe wito kwa walimu wenzangu ambao si waadilifu wabadilike, wale watoro waache utoro, ambao ni walevi wache ulevi wafundishe watoto; lakini wazazi na ninyi mtusaidie kuhimiza watoto wawe na mahudhurio mazuri shuleni ili walimu waweze kufanya kazi yao vizuri,” alisema Seif.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko amesema hadi sasa mfuko huo umeingiziwa kiasi cha shilingi milioni 15 na halmashauri na baadaye wadau kuongeza kiasi cha shilingi milioni 15 na kuufanya mfuko huo kuwa na jumla ya shilingi milioni 30.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Antony Mtaka amewataka walimu kuacha tabia ya kukopa fedha katika taasisi nyingine za fedha hususani za binafsi zenye riba kubwa ambazo huwalazimu kuweka kadi zao za benki kama rehani, huku akishauri Benki ya walimu kuja na huduma zinazojibu changamoto za walimu ikiwemo kutoa mikopo kwa riba nafuu
Kwa upande wake Katibu wa CWT ameipongeza Wilaya ya Maswa kwa kuona haja kuwapongeza walimu na ya kuwasaidia walimu kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu kupitia mfuko huo, ambapo CWT pia imeunga mkono juhudi Wilaya kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni Nane (8).
Wilaya hiyo pia imetoa zawadi ya majiko ya gesi 101 kama zawadi kwa shule hizo ili kuwawezesha walimu kupata chai asubuhi wakiwa shuleni na kuwapunguza walimu muda wa kwenda kutafuta huduma hiyo nje ya maeneo ya shule.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe amesema mwaka 2018 Wilaya ilitoa majiko ya gesi kwa  shule 20 zilizofanya vizuri hivyo, majiko hayo yanatolewa kwa shule 101 ambazo hazikupata awali, pamoja na zawadi ya majiko shule zilizofanya vizuri zimepewa fedha taslimu shilingi 500,000.
Katika uzinduzi huo pia ilifanyika harambee kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa nyumba nne za walimu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa nyumba za walimu
MWISHO



Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif (kulia) na viongozi wengine wa mkoa wa Simiyu wakiwa wameshika mfano wa hundi ya shilingi milioni 15 ambayo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa ajili ya kuanzisha mfuko wa walimu uliozinduliwa rasmi Novemba 29, 2019 Mjini Maswa. 

 Kutoka kulia Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe, Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Antony Mtaka wakikata keki kuashiria uzinduzi wa Mfuko wa walimu, Novemba 29, 2019 katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019.


 Kutoka kulia Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredricka Sagamiko(kushoto) wakipokea hudni ya shilingi milioni nane kutoka kwa Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif(kulia) zilizotolewa an chama hicho kuchangia Mfuko wa walimu uliozinduliwa rasmi Novemba 29, 2019 mjini Maswa.


 Baadhi ya walimu kutoka shule mbaimbali wilayani Maswa wakishangilia jambo wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019 ambayo imefanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.


 Mmoja wa Wakurugenzi katika Benki ya Walimu akitoa maelezo kwa viongozi wa Mkoa wa Simiyu juu ya namna benki hiyo itakavyounga mkono mfuko wa walimu wilayani maswa uliozinduliwa rasmi Novemba 29, 2019 Mjini Maswa.


 Mmoja wa Walimu akipokea zawadi ya jiko la gesi iliyotolewa na  Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kila shule kwa ajili ya kutumia kupikia chai asubuhi wakiwa shuleni, katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019 ambayo imefanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019.
 Baadhi ya Maafisa Elimu Kata wakifutailia matukio katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa. 


Baadhi ya walimu wa shule za msingi wilayani Maswa, wakifutailia matukio katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa. 

 Baadhi ya viongozi na wadau wa elimu wakicheza wimbo maalum uliondaliwa na kwaya ya walimu Maswa wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa. 


 Baadhi ya viongozi wa Chama na  Serikali mkoa wa Simiyu na viongozi wa CWT na wakifutailia matukio katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa. 


 Baadhi ya viongozi wa Chama na  Serikali mkoa wa Simiyu na viongozi wa CWT na wakiwa katika  picha ya pamoja baada ya kuhitimishwa kwa hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa. 


 Majiko 101 yaliyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Maswa kwa ajili ya shule za msingi kwa ajili ya kupikia chai asubuhi, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa. 


 Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif akizungumza na walimu wa shule a msingi wilayani maswa(hawapo pichani), katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa. 


Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif akimshukuru Mbunge wa Maswa mashariki na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo kwa kukubaki kuchangia ujenzi wa nyumba za walimu wilayani Maswa, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
 Mmoja wa Walimu akipokea zawadi ya jiko la gesi iliyotolewa na  Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kila shule kwa ajili ya kutumia kupikia chai asubuhi wakiwa shuleni, katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019 ambayo imefanyika Novemba 29, 2019 mjini Maswa.
 Baadhi ya walimu wa shule za msingi wilayani Maswa, wakifutailia matukio katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa.

Baadhi ya walimu wa shule za msingi wilayani Maswa, wakifutailia matukio katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa.

 Baadhi ya walimu wa shule za msingi wilayani Maswa, wakifutailia matukio katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa. 
Kutoka kulia Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe, Katibu wa CWT Taifa, Mwl.Deus Seif na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Antony Mtaka wakiteta jambo katika  hafla ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi 123 wilayani Maswa kwa kuwezesha wilaya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya darasa la saba na kuongeza ufaulu  kutoka asilimia 34.9 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 88.73 mwaka 2019, hafla iliyofanyika  Novemba 29, 2019 mjini Maswa.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!