Thursday, October 13, 2016

RAIS WA ZANZIBAR MHE. DKT. ALI MOHAMED SHEIN AWASILI SIMIYU

Na Stella Kalinga
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amewasili Mjini Bariadi jioni hii kwa ajili ya Maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana yatakayofanyika kitaifa kesho tarehe 14 Oktoba, 2016 Mjini, Bariadi mkoani hapa.

Mhe. Rais wa Zanzibar ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Kifo cha Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana, tukio ambalo ni la kihistoria kwa mkoa wa Simiyu.


Rais Shein amepokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo viongozi wa Chama na Serikali pamoja na wananchi wa Mjini Bariadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipewa heshima na vijana wa Skauti Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokelewa Ikulu ndogo Mjini Bariadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa amevalishwa skafu na vijana wa Skauti Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokelewa Ikulu ndogo Mjini Bariadi,  ishara ya kumkaribisha, (kushoto) Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya viongozi, watumishi na wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokelewa Ikulu ndogo Mjini Bariadi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya viongozi, watumishi na wananchi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokelewa Ikulu ndogo Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!