Na
Stella Kalinga
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama amefungua kiwanda cha kutengeza chaki kinachoendeshwa na
kikundi cha Vijana cha Maswa Family kilichopo wilayani Maswa Mkoani Simiyu.
Akizungumza
na wananchi wa Wilaya ya Maswa waliyojitokeza kushuhudia zoezi hilo la
ufunguzi, Mhagama amempongeza Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony Mtaka na watendaji
ngazi ya Mkoa na wilaya waliowasaidia vijana hao kuendeleza wazo lao na kufikia
hatua waliyopo sasa, hali iliyowatengenezea ajira na kuwapatia kipato.
Waziri
Mhagama amewataka vijana hao kufanya kazi kwa bidii, kutoingiza masuala ya
kisisasa na maslahi binafsi katika uendeshaji wa mradi ili waweze kufikia
malengo yao.
Katika kuunga mkono juhudi za Kikundi hicho
cha Maswa Family Waziri Mhagama ameahidi kuwa Wizara yake itawapatia mkopo wa
shilingi 30,000,000 ili ziweze kuwasaidia kuongeza mtaji na uzalishaji.
Awali
akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri huyo, Mkuu wa Mkoa huo amesema Serikali
mkoani humo imejipanga kuonesha kuwa Watanzania wana uwezo wa kutengeneza vya kwao
kwa kutumia malighafi za hapa nchini.
Mtaka
amesema Mkoa wake ni wa kutekeleza hivyo viongozi wake wamejipanga kutekeleza
ili kufikia azma ya kuwa miongoni mwa mikoa mitano inayotumaini kiuchumi hapa
nchini, badala ya kufungua semina, warsha na makongamano ya
wajasiriamali ambayo hayawasaidii wanachi katika kuinua uchumi wao.
Naye
Waziri Mhagama ametangaza rasmi kuwa kiongozi yeyote asimualike katika kufungua
warsha, semina na makongamano ya ujasiriamali badala yake wamuite kufungua na
kuona utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa vijana kama alivyofanya
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
“Kwa
hali hiyo naomba nitangaze rasmi sasa na ninaamini ujumbe huu utafika nchi
nzima kuwa, kiongozi yeyote tangu wewe
Mhe Mkuu wa Mkoa umeamua kufanya maamuzi haya, asinialike kufungua kongamano wala warsha, kuanzia
leo nialikwe kuyafanya kama haya uliyoyafanya kwenye Mkoa wa Simiyu na wilaya ya Maswa” alisema Mhagama.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira
Mhe Anthony Mavunde ambaye ametangaza kuwa balozi wa Chaki zinazotengezwa
Maswa(MASWA CHALKS) amewataka vijana kutimiza wajibu wao kwa kujishughulisha na
kuacha kulamu Serikali.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Mhe. Stanslaus Nyongo amesema yeye pamoja na
mbunge mwenzake wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mhe. Mashimba Ndaki watasimamia na
kuhakikisha mafungu yote yanayotolewa kwa ajili ya wanawake na vijana wa Maswa
yanawafikia na kuwanufaisha.
Kiwanda
cha kuzalisha chaki cha Maswa kimegharimu zaidi ya milioni 37 na kinaweza
kuzalisha katoni 128 kwa siku, ambapo zaidi ya shule za Msingi na Sekondari 600
za mkoa wa Simiyu na za mikoa ya jirani zinaweza kunufaika na kiwanda hiki.
0 comments:
Post a Comment