Na Stella Kalinga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye
ulemavu Jenista Mhagama ameziagiza halmashauri zote nchini ambazo hazijatenga
maeneo kwa ajili ya vijana kufanya hivyo mara moja.
Mbali na hilo Mhagama ameziagiza halmashauri nchi nzima kuhakikisha
zinafungua na kuanzisha SACCOS za Vijana na kuzisimamia ili vijana wapate
mikopo yenye masharti nafuu, ikiwa pamoja na kuhakikisha zinatenga asilimia 5
ya mapato ya ndani kama inavyotakiwa.
Waziri Mhagama alitoa maagizo hayo leo Mkoani Simiyu wakati akiongea na mamia
ya wananchi na vijana wa Mkoa huo mjini Bariadi katika ufunguzi wa maadhimisho
ya wiki ya vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani hapa.
Mhagama amesema kuwa mpaka sasa ni halmashauri 72 zimeshatenga hekari 84037
kati 185 kwa ajili ya vijana katika shughuli za kilimo, ufugaji na kibiashara,
ili kuweza kujiletea maendeleo ya kiuchumi.
“ ..kupitia maadhimisho haya ninaagiza halmashauri zote nchini ambazo
zinafahamu bado hazijatenga maeneo haya kuhakikisha wanatenga mara moja…na
kuwapatia vijana kwa ajili ya kufanya shughuli hizo” Alisema Waziri
Aidha Waziri huyo aliongeza kuwa bado kuna halmashauri nchini zimeshindwa
kutekeleza maagizo ya serikali ya kuanzisha SACCOS za Vijana, ambapo mpaka sasa
ni halmashauri 113 tu ambazo zimeanzisha SACCOS hizo kati ya 185, huku zikiwa
zimetenga jumla ya shilingi Bilioni.3.9 kwa mwaka wa fedha 2016/17 na akazitaka
halmashauri zingine kuanzisha SACCOS hizo na kutenga fedha za Vijana mara moja.
Awali akimkaribisha Waziri huyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka
amesema kuwa mkoa huo umeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli la kuifanya Tanzania kuwa
ya viwanda kwa kuanzisha viwanda viwili vidogo; kiwanda cha kutengeneza chaki
kilichopo wilaya ya Maswa na cha
kusindika Maziwa kilichopo Meatu.
Mtaka amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuufanya mkoa huo kuwa wa mfano
na kuwa miongoni mwa mikoa mitano ya kutumainiwa kibiashara ambao viongozi
mbalimbali wataenda kujifunza namna unavyotekeleza.
Hata hivyo Waziri Mhagama alimpongeza Mkuu wa mkoa huyo na kusema kuwa
amekuwa kiongozi wa kwanza kutekeleza agizo la Rais, na kumuahidi kuwa ofisi ya
Waziri Mkuu iko tayari kusaidia juhudi hizo hata kwa kutoa fedha za kuwawezesha
vijana.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye ulemavu
amewataka Wakuu wa mikoa , wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri kote
nchini kuwa chachu na kiungo muhimu katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kutokomeza
unyanyapaa na vitendo vya ukatili, wanavyofanyiwa watu wenye ualbino ili nao
waweze kufanya shughuli za maendeleo bila uoga kama ilivyo kwa baadhi yao.
Wiki
ya vijana itahitimishwa pamoja na Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Kifo
cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, tarehe 14 Oktoba, 2016 Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
|
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye
ulemavu Jenista Mhagama (wa tano kushoto) viongozi mbalimbali ngazi ya taifa na
Mkoa wakipokea maandamano ya vijana katika Uzinduzi wa Wiki ya Vijana, Uwanja wa Sabasaba Mjni Bariadi.
|
Baadhi ya Vijana wa Mkoa wa Simiyu wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali
kwa Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye
ulemavu Jenista Mhagama ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Wiki ya
Vijana Mjini Bariadi.
|
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye
ulemavu Jenista Mhagama, akivishwa skafu na vijana wa skauti wa Mkoa wa Simiyu baada ya kupokea maandamano ya amani ya vijana katika Uzinduzi wa Wiki ya
Vijana, Uwanja wa Sabasaba Mjni Bariadi.
Kikundi
cha Brass Band cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani Dar es Salaam
wakiwaongoza vijana katika maandamano ya amani kuelekea uwanja wa Sabasaba
Mjini Bariadi ambapo wiki ya vijana imezinduliwa rasmi leo
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza kabla ya kumkaribisha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu Mhe.Jenista
Mhagama (Mb), azungumze na Vijana na Wananchi wa Mkoa huo wakati wa Uzinduzi wa
Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mbele) akiwaongoza viongozi wa
Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu kuimba
pamoja na Kwaya ya Walimu wa Bariadi iliyotoa burudani wakati wa Uzinduzi wa
Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi.Kutoka kushoto (wa tatu)
Waziri Jenista Mhagama, (wa tano) Naibu Waziri Anthony Mavunde na (wa sita)
Naibu Waziri Abdallah Possi.
|
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye
ulemavu Jenista Mhagama na viongozi wengine wakicheza pamoja na msanii Alphonce
Seme (Mzee wa Madodoso) wakati wa Uzinduzi
wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi.
|
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa saba kushoto) na viongozi wengine wa kitaifa na kimataifa wakiimba pamoja na Kwaya ya Walimu wa Bariadi iliyotoa burudani wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi.
|
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akitambulisha viongozi wa
Kitaifa na Kimataifa (hawapo pichani) walioshiri katika uzinduzi wa wiki ya Vijana Mkoni Simiyu.
|
|
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Wizara ya nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye ulemavu , Jemasi Kajugusi akizungumza na Vijana na Wananchi wa wa Mkoa wa Simiyu wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la linaloshughulikia idadi ya watu
duniani, Christina Mwanukuzi akiwasilisha salamu za Mkurugenzi huyo kwa Vijana
na Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa
mwaka 2016, Mjini Bariadi.
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiimba wimbo wa mkoa huo na Vijana
wa Halaiki waliotoa burudani wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka
2016, Mjini Bariadi.
|
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakitoa burudani ya nyimbo wakati
wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi.
|
Mwakilishi wa Vijana Diana Rose Lyimo akisalimiana na viongozi mara baada
ya kuwasilisha maaazimio ya vijana wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa
mwaka 2016, Mjini Bariadi.
|
Amosi Manyama Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon
akitoa salamu za Katibu Mkuu huyo kwa Vijana na Wananchi wa Mkoa wa Simiyu
wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi.
|
|
|
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye
ulemavu Jenista Mhagama akipewa maelezo na Maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
NEC alipotembelea banda la tume hiyo wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa
mwaka 2016, Mjini Bariadi |
|
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu sera, bunge, kazi, ajira na wenye
ulemavu Jenista Mhagama akipewa maelezo na Kijana mgunduzi juu ya kifaa alichokigundua
kinachotumika kupima mwendokasi wa magari, alipotembelea banda la Vijana hao wakati
wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi
|
|
Wasanii wa Kikundi cha burudani cha BASEKI cha Mjini Bariadi wakitoa
burudani wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016, Mjini Bariadi.
|
: Viongozi wa kimkoa, kitaifa na kimataifa wakiimba pamoja na Kwaya ya
Walimu wa Bariadi iliyotoa burudani wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa
mwaka 2016, Mjini Bariadi.
|
Kikundi cha Brass Band kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani
wakiwaogoza vijana wa mkoa wa Simiyu katika
maandamano ya amani yaliyofanywa kuelekea uwanja wa Sabasaba Mjini
Bariadi, katika Uzinduzi wa Wiki ya Vijana kitaifa mwaka 2016.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
0 comments:
Post a Comment