Friday, October 14, 2016

RAIS SHEIN : SERIKALI IMEJIPANGA KUKUSANYA MAPATO NA KUPUNGUZA MISAADA YA WAHISANI



Na Stella Kalinga
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amesema Serikali imejipanga  kukusanya  na kutumia Mapato na rasiliamali zake  kwa maendeleo ya wananchi ili kupunguza na hatimaye kuondokana na kupewa misaada ya wahisani.

Rais Shein amesema hayo leo wakati alipowahutubia  na wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla kwenye  maadhimisho ya  Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu.

Rais Shein amesema Serikali haiko tayari kukubali misaada ya baadhi ya wahisani ambao wamekuwa wakitoa na kuambatanisha na masharti yasiyotekelezeka  ambayo yapo wa ajili ya kuharibu mipango ya maendeleo.

Aidha, Rais Shein amesema ili kufikia azma hiyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimejidhatiti kuimarisha uwajibikaji kwa watumishi wa umma, kubana mianya yote ya rushwa na upotevu wa mapato na fedha zitakazookolewa zitaelekezwa katika shughuli za kiuchumi na huduma za jamii.

Sanjali na hilo Mhe. Dkt. Shein ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ya kusimamia uchumi wa nchi na kupambana na watu wenye tamaa na lengo la kuhujumu uchumi.

Dkt. Shein amesema juhudi hizo za Serikali zina nia ya kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii ambapo alizitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar kuwajibika ipasavyo katika ukusanyaji wa mapato.

“Tumeanza kuwawajibisha watumishi wasio waadilifu wapo waliotangazwa na ambao hawajatangazwa, bado tunaendelea kuwachunguza wengine “alisema Rais Shein.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama amesema  Mwenge wa uhuru mwaka 2016 umebaini ubadhilifu na udanganyifu katika miradi ya maendeleo katika Halmashauri saba nchini, hivyo akaelekeza hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma zichukuliwe kwa watakaobainika kuwa chanzo cha ubadhilifu huo.

Katika kutekeleza Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru, mwaka 2016, “Vijana ni nguvu kazi ya Taifa; Washirikishwe na kuwezeshwa” Mhe.Mhagama amesema mikoa ya Simiyu, Njombe,Mwanza, Ruvuma, Mbeya na Mtwara imetekeleza agizo la Serikali la kuhakikisha vijana wote nchini wanawezeshwa kwa kuwapa mitaji na kuwajengea uwezo wa kuendesha miradi mbalimbali.

Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wake umedhamiria kuwawezesha vijana kujiairi kwa kutumia fursa zilizopo ikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa kila wilaya chini ya Kauli Mbiu “Wilaya moja bidhaa moja”, ambapo hadi sasa Wilaya ya Maswa ina kiwanda cha kuzalisha chaki na Meatu kiwanda cha kusindika maziwa.

Maadhimisho ya  Kilele cha Mbio za Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa mwaka 2016 yalitanguliwa na Ibada ya Kumuombea Hayati Baba wa Taifa iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi, ambapo Askofu wa Jimbo la Shinyanga,  Liberatus Sangu amewaasa Watanzania kumuenzi Baba wa Taifa kwa  kupinga rushwa, ubaguzi na kudumisha amani na utulivu nchini.


Jumla ya Miradi  1,342 yenye thamani ya shilingi bilioni 498.8 imewekewa mawe ya Msingi  na mingine kuzinduliwa na Mwenge wa uhuru mwaka 2016 na kuanza kutoa huduma kwa wananchi, Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 zitazinduliwa katika Mkoa wa Katavi na kuhitimishwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016, Ndg. George Mbijima  wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, zilizofanyika kitaifa Mkoani Simiyu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipanda katika jukwaa maalum kwa ajili ya kupokea Mwenge wa uhuru kutoka wa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Mwaka 2016, Ndg. George Mbijima.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwahutubia  na wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, zilizofanyika kitaifa Mkoani Simiyu
Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakielekea kumkabidhi Mwenge wa Uhuru wa uhuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akizungumza  na wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, zilizofanyika kitaifa Mkoani Simiyu.
Waziri wa Kazi,Uwezeshaji, Vijana, Wazee,Wanawake na Watoto wa Zanzibar , Mhe. Moudline Castico akizungumza  na wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa Maadhimsho ya  Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za mkoa kwenye maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu
: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na  Viongzi wa mkoa wa Simiyu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na, Mawaziri wenye dhamana ya Vijana Zanzibar (kushoto) na Jamhuri ya Muungano (kulia) ,Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (pili kushoto), Mwenyekiti wa CCM mkoa, Dkt.Titus Kamani na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga(mstari wa pili kushoto)

Vijana wa Halaiki wakionesha maumbo ya vitu mbalimali katika onesho lao maalum wakati wa maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa Dini walishiriki katika maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu

Vijana wa Halaiki wakionesha maumbo ya vitu mbalimali katika onesho lao maalum wakati wa maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu.


Vijana wa Halaiki wakionesha maumbo ya vitu mbalimali katika onesho lao maalum wakati wa maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo ya utangulizi kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kutembelea mabanda ya maonesho ya vijana.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipewa maelezo na kijana kutoka kikundi cha Meatu Milk alipotembelea Banda la Vijana wa Meatu mkoani Simiyu wanaosindika maziwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akipewa maelezo na kijana mgunduzi wa teknolojia ya umwagiliaji wa matone alipotembelea mabanda ya vijana, Uwanja wa SABASABA mjin Bariadi.

Askofu wa Jimbo Kuu la Shinyanga, Liberatus Sangu akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri na Viongozi wa Serikali walioshiriki Ibada Maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.
Askofu wa Jimbo Kuu la Shinyanga, Liberatus Sangu akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa madhehebu mbalimbali  walioshiriki Ibada Maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.


Askofu wa Jimbo Kuu la Shinyanga, Liberatus Sangu akitoa dua ya kumuombea Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere kwenye maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu.

Askofu wa Jimbo Kuu la Shinyanga, Liberatus Sangu na Mapadri wakiwa katika Ibada Maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akiwatambulisha viongozi wa Serikali (hawapo pichani)walioshiriki katika Ibada Maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.



Askofu wa Jimbo Kuu la Shinyanga, Liberatus akiongoza  Ibada Maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.

Baadhi ya Waumini walioshiriki Ibada Maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akitoa salamu za Serikali walioshiriki katika Ibada Maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwl.Julius K.Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Yohana Mjini Bariadi.

Kikundi cha Burudani cha SAKWE kutoka Wilaya ya Bariadi wakitoa burudani kwenye kwenye maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru,  Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere na Wiki ya vijana, yaliyofanyika kitaifa Mkoani Simiyu.


Kwaya kutoka Kanisa la Kotoliki Mjini Bariadi wakiimba wimbo maalum wa Hayati Baba wa Taifa wakati wa ibada ya kumbukumbu ya kifo chake kilichotokea mika 17 iliyopita.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!