Na
Stella Kalinga
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama amefungua kiwanda cha kusindika maziwa kinachoendeshwa na kikundi cha Vijana wa Meatu kilichopo wilayani
humo Mkoa wa Simiyu.
Akizungumza
na Vijana hao wanaosindika maziwa ya Meatu (MEATU MILK), Waziri Mhagama
amewataka kuutunza mradi huo ili uwe mradi mkubwa wa kuwaingizia mapato wao na
Serikali kwa ujumla.
Mhagama
amesema kwa kadri mradi huo utakavyokuwa mkubwa ndivyo wafugaji wa Wilaya ya
Meatu na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla watakavyonufaika kwa kupata soko la uhakika
la maziwa.
Aidha,
Waziri huyo amewataka Viongozi wote wa wilaya kuunga mkono juhudi zilizofanywa
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka za kuwatengenezea vijana mazingira mazuri ya kutekeleza
shughuli mbalimbali za maendeleo yao, ikiwa ni pamoja na kushughulikia
upatikanaji wa mitaji na mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Wakati
huo huo Waziri Mhagama ameahidi kuwa
Ofisi yake itatoa mkopo wa shilingi 30,000,000 kwa lengo la kuwasaidia vijana
hao kuongeza uzalishaji ili kupanua soko la maziwa yao ndani na nje ya Mkoa.
“Mhe.
Mkuu wa Mkoa Ofisi ya Waziri Mkuu itawapa mkopo vijana wa “Meatu Milk”ili
wapanue uzalishaji; Wizara yangu itatoa mikopo kwa vijana walio tayari
kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia
kuwapa ajira na kujikwamua kwenye umaskini” alisema Mhagama.
Akizungumza
na wananchi wa wilaya ya Meatu kabla ya kumkaribisha Waziri Mhagama Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa huo umejipanga kuzalisha bidhaa
mbalimbali kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.
“Tumejichagua
kuwa pacha wa Mhe. Rais katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa
Vitendo na tumedhamiria kuwa miongoni mwa mikoa mitano inayofanya vizuri katika
uchumi”, alisema Mtaka.
Akiwasilisha
taarifa ya mradi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kwa Mhe. Waziri, kiongozi wa kikundi cha Meatu
Milk Lightness Benedicto amesema Halmashauri imewapa mtaji na kuwajengea uwezo
kwenye teknolojia za usindikaji, ufungishaji wa bidhaa za maziwa pamoja na
elimu ya ujasiriamali.
Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Mbuzi ameahidi kuwaongezea
mtaji wa shilingi 5,000,000 vijana hao pamoja na kuwasaidia kukutafuta soko la
uhakika kwa maziwa watakayosindika.
Mradi
wa kiwanda cha kusindika maziwa Meatu wenye vijna 18 hadi sasa umegharimu jumla
ya shilingi 34,903,000 kati ya hizo shilingi 10,000,000 ni michango ya
wanachama kutoka kwenye gawio la fedha za mkopo uliotolewa na Wizara yenye
dhamana na vijana,shilingi 24,903,000 ni mkopo kutoka kwenye 5% ya mapato ya
ndani ya Halmashauri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi zawadi ya maziwa Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe. Maudline Castico mara baada ya kuzindua kiwanda cha maziwa Meatu |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mhe. Fabian Manoza akipokea zawadi ya maziwa kutoka kwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kuzindua kiwanda cha maziwa Meatu |
0 comments:
Post a Comment