Tuesday, August 21, 2018

HALMASHAURI ZAKARIBISHA WAWEKEZAJI KWENYE VIWANJA VINAVYOPIMWA MKOANI SIMIYU


Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Busega na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu zinawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kuwekeza kwenye jumla ya viwanja 3758 vilivyopimwa na vinavyotarajiwa kupimwa kwa nyakati tofauti.

Hayo yamebainishwa na Viongozi wa Halmashauri hizo katika kikao cha tathmini ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru Viongozi,watumishi na wadau mbalimbali waliofanikisha, kilichofanyika Agosti 20, Mjini Bariadi.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo amesema Halmashauri yake inatarajia kupima viwanja 758 katika eneo la Maperani, huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akibainisha kuwa Halmashauri hiyo kuanzia Septemba Mosi, 2018 itaanza kupima viwanja 1000 katika eneo la Malampaka.

Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Kabuko amesema Halmashauri hiyo imeanza kupima viwanja 2000 Agosti 20, 2018  katika eneo ambalo liko umbali wa chini ya kilomita moja kutoka Ziwa Victoria, pia imetenga ekari zaidi ya 2000 kwa ajili ya uwekezaji na akasisitiza kuwa ardhi itatolewa bure kwa wawekezaji watakaotaka kujenga viwanda.

Viongozi hao  wametoa wito kwa wafanyabiashara, wawekezaji wa ndani na nje ya mkoa wa Simiyu,Taasisi, mashirika, makampuni na wananchi kujitokeza kununua viwanja hivyo kwa ajili ya kuviendeleza kwa uwekezaji na kubainisha kuwa maeneo yote yanayotarajiwa kupimwa Bariadi, Maswa na Busega ni ya kimkakati katika uwekezaji.

"Kuanzia tarehe 01 Septemba, tutaanza kupima viwanja 1000 katika eneo la Malampaka Maswa, ni eneo la kimkakati katika uwekezaji kwa sababu patapitiwa na Standard Gauge(Reli ya Kisasa) na patajengwa dry port (bandari kavu), nitoe wito kwa wafanyabiashara kuja kununua viwanja Malampaka kwa ajili ya kufanya uwekezaji mbalimbali; kwa wale wawekezaji watakaotaka kujenga viwanda sisi Maswa tutatoa ardhi bure" alisema Dkt. Sagamiko.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa Wafanyabiashara wa Mkoa huo kuwekeza katika Ujenzi wa Hoteli, Nyumba za kulala wageni na kumbi za mikutano hususani katika Eneo la Uwanja wa Nanenane Nyabindi na maeneo mengine, ili kukabiliana na changamoto ya malazi kwa kuwa Simiyu imepewa heshima ya kuwa Mwenyeji wa Maonesho ya Nanenane kwa miaka mitatu mfululizo.

Amesema pamoja na kuwa mwenyeji wa Maonesho Nanenane Kitaifa yapo matukio mengine yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu, ikiwa ni pamoja na Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 2018, Maadhimisho ya  Kimataifa ya siku ya watu wenye Ulemavu Desemba 2018, Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya hapa nchini mwaka 2019 na mengine mengi yatafuata baada ya hapo hivyo maandalizi ni muhimu..

Amesema Serikali mkoani humo kupitia Halmashauri zake  imedhamiria kuwekeza katika ujenzi wa sehemu za malazi lakini inaendelea kuweka msukumo kwa wafanyabishara kuwekeza si tu katika ujenzi wa nyumba za kulala wageni na hoteli, bali katika ujenzi wa vituo vya mafuta, maeneo ya utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za chakula na huduma za kibenki.

Mmoja wa Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu Bw. Malongo Midimu amesema wako tayari kuwekeza  mkoani hapa na akaomba Serikali pamoja Taasisi za Kifedha zikiwemo Benki kuondoa vikwazo na urasimu pale wanapohitaji masuala hayo

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ametoa wito kwa Wafanyabiashara kujipanga katika uwekezaji kwa kuwa Simiyu inabadilika na inaendelea kufunguka ambapo amebainisha kuwa kukamilika kwa Ujenzi wa miundombinu kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa eneo la Igegu wilaya ya Bariadi, barabara ya Maswa-Bariadi kutachangia ukuaji wa uchumi wa Mkoa.

Kikao cha Tathmini ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018, Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, kiliwahusisha Viongozi na Watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya, Watumishi na Wadau mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu kikiwa na lengo la kushukuru na kutambua mchango wa wadau wote muhimu waliofanikisha maonesho hayo.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi  na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara na Mjumbe wa NEC  Taifa kupitia Mkoa wa Simiyu Bw. Gungu Silanga akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mfanyabiashara wa Mjini Bariadi, Bw. Clement Mlanda akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Mhe. Juliana Mahongo  akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.

Katibu wa Umoja wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Bi. Christina Matulanya akizungumza katika kikao cha  Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi  na Watendaji wa Chama na Serikali, Wafanyabiashara na wadau wengine wakiwa katika kikao cha tathmini ya  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka 2018 mkoani Simiyu,  kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akizungumza katika Kikao cha Tathmini  Maonesho ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa mwaka2018 mkoani Simiyu na kuwashukuru  Viongozi  na watendaji wa Chama na Serikali, wafanyabiashara na wadau wengine walioshiriki katika kufanikisha  maonesho hayo,  kilichofanyika Mjini Bariadi..

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!