Tuesday, August 21, 2018

RC MTAKA AKABIDHI MWENGE WA UHURU MKOANI SHINYANGA


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Taleck  na kumhakikishia Kiongozi wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 Ndg. Charles Kabeho  kuwa atachukua hatua dhidi ya mapungufu yaliyobainika wakati Mwenge wa Uhuru ukipitia baadhi ya miradi ya maendeleo mkoani Simiyu.

Mtaka amesema ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na Kiongozi wa Mbio za  Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 Ndg. Charles Kabeho  yatafanyiwa kazi,ikiwa kuna mahali pa kuchukua hatua,  hatua stahiki zitachukuliwa na ikiwa kuna mahali pa kufanya maboresho ili miradi hiyo itekelezwe katika viwango vinavyokidhi haja ya kutoa huduma kwa wananchi, Serikali ya mkoa itahakikisha inasimamia.

“Ndugu Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 na wakimbiza Mwenge wenzako, tunawashukuru kwa kuwa sehemu ya jicho la tatu kwenye miradi inayotekelezwa ndani ya mkoa, niwahakikishie kwamba tutachukua stahiki pale ambapo palionesha ukakasi kwenye taarifa zetu na pale ambapo mliona kunahitajika hatua ili miradi iweze kufanya kazi kwa ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi tutachukua hatua” alisema Mtaka.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Kabeho amewashukuru viongozi na wananchi wa Mkoa wa Simiyu kwa ushirikiano waliompa yeye na wakimbiza Mwenge wenzake walipokuwa Simiyu.

Aidha, Kabeho alitoa rai kwa watumishi wa Umma kuachana na kufanya kazi kwa uzembe na mazoea badala yake wafanye kazi kwa weledi na bidii, hususani katika usimamizi wa miradi ili iweze kutekelezwa kwa wakati katika viwango vya ubora unaotakiwa na wananchi wapate huduma kwa wakati.

Mwenge wa Uhuru umekabidhiwa katika kijiji cha Wishiteleja katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo ukiwa mkoani Simiyu ulipitia miradi 36 yenye thamani ya shilingi bilioni 8.4.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Taleck katika Kijiji cha Wishiteleja wilayani Kishapu mkoani Simiyu Agosti 20, 2018. 



0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!