Friday, August 3, 2018

WAZIRI TIZEBA: WAANDAAJI WA NANENANE ANDAENI MAONESHO YATAKAYOSAIDIA WANANCHI KULETA TIJA KATIKA UZALISHAJI


Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba amewataka Waandaaji wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane hapa nchini kuhakikisha kuwa kuanzia mwaka 2019 wanaandaa maonesho hayo katika sura mpya itakayoleta mabadiliko chanya kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili waweze kuzalisha kwa tija.
.
Waziri Tizeba ameyasema hayo Agosti 03, 2018 katika Uwanja wa Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki, uliopo Nyakabindi Bariadi, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 yanayofanyika Mkoani Simiyu.

Amesema ni vema waandaaji hao wakatoka katika maonesho ya mazoea ya kuwaonesha wakulima na wadau  vipando mbalimbali pasipo kuwapa elimu ya namna yakufikia uzalishaji wanaouona katika maonesho, badala yake maonesho hayo yatumike kuwafundisha wananchi na kubadilishana uzoefu.

“Kuanzia nanenane ya mwaka huu na zinazofuata, wandaaji wazipe sura mpya hata tunapowaomba wadau mbalimbali kuchangia maandalizi wawe wananamini kuwa tutakachokifanya kitaleta  mabadiliko chanya kwa wakulima, wafugaji na wavuvi wa nchi hii”alisema Tizaba.

Aidha, Dkt. Tizeba amekubaliana na mpango wa viongozi wa Mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga kufanya maonesho kila baada ya miezi mitatu katika Uwanja wa Nyakabindi ili kuwapa fursa wananchi ya kuendelea kujifunza badala ya kusubiri kila wiki ya nanenane kila mwaka.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema dhamira ya Mkoa huo na kanda ya Ziwa ya Mashariki ni kuendelea kufanya maonesho Teknojia za Kilimo  Biashara katika Uwanja wa Nyakabindi jambo ambalo litawapunguzia Watanzania kwenda nje ya nchi kujifunza teknolojia hizo.

“Tutafanya maonesho hapa kila baada ya miezi mitatu, kupitia maonesho yatakayofanyika eneo hili, tutawapunguzia wananchi safari za kwenda nje ya nchi  kufuata teknolojia za kilimo Biashara” alisema Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka amesema Waoneshaji waliopo Uwanja wa Nanenane Nyakabindi wameomba kuongezewa siku mpaka kufikia Agosti 11 badala ya Agosti 08 kama ilivyo kawaida, jambo ambalo lilikubaliwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima amesema matarajio ya viongozi wa Kanda ya Ziwa Mashariki ni kuyafanya maonesho ya nanenane kanda hiyo kuwa mnara wa mafanikio katika sayansi na teknolojia na namna ambavyo kilimo kinachozingatia kanuni bora kinavyochangia mabadiliko chanya ya mfumo wa Watanzania waanotegemea kilimo.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ametoa wito kwa wananchi kufika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Nyakabindi ili kupata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kwa kuwa kwa sasa waoneshaji wa teknolojia mbalimbali wapo uwanjani hapo.
  
Maadhimisho ya Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima Nanenane mwaka 2018 yanayofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu ni ya 25 kufanyika hapa nchini na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amesema maonesho hayo yatafanyika miaka mitatu mfululizo, mwaka 2018, mwaka 2019 na mwaka 2020.
MWISHO


Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akipewa maelezo kuhusu teknolojia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi  kwenye ufunguzi wa maonesho ya NaneNane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akizungumza na wataalam wa Kilimo wa JKT alipotembelea mabanda ya JKT ya  maonesho ya NaneNane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane Kitaifa mwaka 2018, katika Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akiangalia namna mashine hiyo pichani inavyochuja mafuta, mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Mkoa wa Mara, wakati wa Ufunguzi wa maonesho ya NaneNane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akipokea maelezo kutoka kwa wataalamu wa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia ) na viongzo wengine wakishangilia jambo, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.


Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba(wa pili kulia) akipewa maelezo juu ya samani iliyotengenezwa na VETA, baada ya kutembelea banda la Maonesho  la VETA, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba(mwenye skafu) na viongozi wengine wakielekea kwenye mabanda  ya maonesho wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wananchi, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akipokea maelezo mara baada ya kutembelea banda la Maonesho la NBC , wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adamu  Malima (aliyenyosha mkono kuelkea mazao) akizungumza jambo wakati walipotembelea Kitalu cha Kilimo cha Wizara ya Kilimo, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
 Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba (kulia) akiangalia baadhi ya nyaraka za Wizara ya Mifugo na Uvuvi , wakati alipotembea banda la Wizara hiyo , wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018

Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba (katikati ) akizungumza na  Wataaamu wa  MWIBA HOLDINGS LTD , wakati alipotembea banda la Mwekezaji huyo, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akiangalia teknoljia ya ufugaji wa samaki alipotembelea mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ,  kwenye ufunguzi wa maonesho ya NaneNane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba (katikati) akiwa katika Uwanja wa Nanenane wa Kanda ya Ziwa Mashariki kwa ajili ya ufunguzi wa maonesho ya NaneNane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akipokea maelezo mara baada ya kutembelea banda la Maonesho la NMB, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.


Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akinywa maziwa ya Meatu, mara baada ya kutembelea Jengo  la  Maonesho la Mkoa wa Simiyu, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.

Kwaya ya AICT Bariadi ikiimba wimbo maalum kwa ajili ya Nanenane, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.



Baadhi  ya  Madiwani wa Mkoa wa Simiyu wakitunza Mkuu wa Mkoawa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  na kumpongeza kwa utendaji wake, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.

Kikundi cha Ngoma za Asili cha BASEKI kikitoa burudani , wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
:-Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mhe. Mashimba Ndaki akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (kushoto) akicheza pamoja na wasanii wa Eliza Band, wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akifuatilia jambo, wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhe. Andrew Chenge  akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, mhe. Enock Yakobo, akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt. Joseph Chilongani akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt. Seif  Shekalaghe akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Baadhi ya wananchi na madiwani wakisikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Baadhi  ya  Madiwani wa Mkoa wa Simiyu wakitunza Mkuu wa Mkoawa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  na kumpongeza kwa utendaji wake, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi akizungumza na wananchi wakati wa ufunguzi wa maoneshoya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu, uliofanyika Uwanja wa Uwanja wa Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo  Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Agosti 03, 2018.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba akipiga ngoma kuashiria ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Nanenane Kitaifa mwaka 2018, zinazofanyika Uwanja wa Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Agosti 03, 2018



Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Charles  Tizeba(wa sita kulia mbele) katika piccah ya pamoja na viongozi na wadau  mbalimbali  baada  ya  kufungua Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018 yanayofanyika mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!