Thursday, August 2, 2018

NAIBU WAZIRI MWANJELWA AHIMIZA WANANCHI KUPANDA MITI KUTUNZA MAZINGIRA, KUEPUKA UKAME


Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa ametoa wito kwa wananchi  hapa nchini kupanda miti kwa wingi ili kuboresha mazingira, kutunza uoto wa asili, kuwa na uhakika wa mvua na kuepukana na ukame.

Ushauri huo ameutoa katika Uwanja wa Nyakabindi katika Maonesho ya Kilimo na Sherehe ya Wakulima Nane nane wakati wa zoezi la kupanda miti, lililofanyika leo Agosti 02, 2018

Mwanjelwa amesema ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi zoezi la upandaji hapa nchini linapaswa kuwa endelevu kwa wananchi.

"Tumepanda miti hii kwenye Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Bariadi ni sehemu ya uhamasishaji kwa viongozi na wananchi wote kupanda miti, nitoe rai kwa viongozi na wananchi wote mkoani Simiyu kuendeleza zoezi hili ili maana tukipanda miti  tunaboresha mazingira, tunapata mvua ya uhakika, kuboresha uoto wa asili hata mifugo yetu inapata malisho" alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa  Elisante Ole Gabriel amesema upandaji wa miti una uhusiano Mkubwa na mifugo katika Ustawi wa malisho, huku akitoa wito kwa uongozi wa Mkoa wa Simiyu kuendeleza zoezi hili ili kumuunga mkono Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuifanya Tanzania kuwa ya kijani.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema mkoa unatarajia kupanda miti zaidi ya milioni tatu .


Katika hatua nyingine Naibu waziri wa Kilimo  ametembelea  Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  kulipongeza jesho hilo kwa namna linavyopambana na majanga ya moto na kusisitiza kuendelea kutoa elimu ya  mara kwa mara kwa wananchi juu ya kukabiliana na majanga ya moto.

MWISHO

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akipanda mti katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, katika zoezi lililofanyika leo Agosti 02, 2018. 
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akiumwagilia maji mti alioupanda katika Uwanja wa nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, katika zoezi la viongozi kupanda miti lililofanyika leo Agosti 02, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akipanda mti katika Uwanja wa nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, katika zoezi lililofanyika leo Agosti 02, 2018.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa. Elisante Ole Gabriel akipanda mti katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu katika zoezi lililofanyika leo Agosti 02, 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akisisitiza jambo juu ya umuhimu wa upandaji miti, katika zoezi la upandaji miti lililofanyika Agosti 02, 2018, katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Kilimo kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti, katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Bw. Martin Malima akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipotembelea banda la maonesho la Mamlaka hiyo, katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 02, 2018.
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Titu Kamani (kulia) na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba(wa tatu kulia)wakiwa na viongozi wengine, wakitembelea mabanda ya maonesho ya Taasisi mbalimbali, katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 02, 2018.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kutembelea banda la maonesho la UTT,  katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 02, 2018
:- Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akipokea maelezo kutoak kwaMaafisa wa Wizara ya Fedha, alipotembelea banda la maonesho la wizara hiyo katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 02, 2018.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!