Wednesday, August 8, 2018

SERIKALI YAONDOA ZUIO LA KUUZA MAZAO NJE YA NCHI

Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa amesema Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi  ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini.

Mhe. Mkapa amesema hayo katika Kilele  cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Mkoani Simiyu,  Uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi ambapo alikuwa mgeni Rasmi akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

“Ninachukua fursa hii kuwafahamisha kuwa Serikali imeondoa zuio la kuuza Mazao ya Chakula nje ya nchi    ikiwa ni njia nyingine ya kuongeza soko la mazao ya wakulima hapa nchini, hata hivyo mazao hayo yatauzwa nje ya nchi kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu”alisema.

Aidha,  amesema Serikali inawakumbusha wananchi wote kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula wakati wa kuuza mazao yao ili kujihakikishia usalama wa chakula katika kaya zao.

Mkapa pia amesema Serikali ina mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la pamba kutoka tani 121,000 mwaka 2016/2018 hadi kufikia tani milioni moja mwaka  2020.

Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ametangaza rasmi kuwa Maonesho ya Nane nane Kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo hadi mwaka 2020 yatafanyika kanda mpya  Kanda ya Ziwa Mashariki katika Uwanja wa Nyakabindi Bariadi, huku akisisitiza kuwa maonesho hayo yafanyike Kimataifa kwa kushirikisha nchi jirani zinazoizunguka Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema  Mkoa wa Simiyu  utaendelea  kulipa kiupaumbele zao la Pamba na mwaka ujao uzalishaji utaongezeka kutoka kilo milioni 70 hadi kufikia kilo 150.

“Simiyu tunajivunia wananchi wachapa kazi wenye uthubutu na Simiyu inajengwa na Wanasimiyu, mwaka jana tumezalisha kilo milioni 70 za pamba, kwa mwaka huu sasa hivi msimu ukiwa umefikia katikati tuna kilo milioni 85, mwakani tunatarajia kuzalisha kilo zaidi ya 150” alisema

Ameongeza kuwa wananchi wamelima chakula cha kuwatosheleza si watu wa kuomba chakula cha msaada huku akiupambanua Mkoa wa Simiyu kuwa ni mkoa pekee ambao watu wake wanafanya biashara saa 24.

Maonesho ya Nanenane Mwaka 2018 yaliwashindanisha wakulima na wafugaji mmoja mmoja, Taasisi, Wakala, Mashirika ya Umma na Binafsi, Wizara pamoja na Halmashauri 21 za Mikoa ya Simiyu Mara na Shinyanga ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imekuwa ya tatu kati ya hizo 21.
Kauli mbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka 2018 “ WEKEZA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”

MWISHO
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akizungumza na wananchi  katika Kilele  cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa Simiyu ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Vijana wa Skauti wakimvisha Skafu Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa mara baada ya kuwasili Bariadi katika Uwanja wa Nyakabindi kuhitimisha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka katika Kilele  cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akiwapungia mkono wananchi (hawapo pichani), katika Kilele  cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 , katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akikagua Banda la Jeshi la Magereza wakati alipotembelea baadhi ya mabanda katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi., katika Kilele  cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Simiyu, katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Mtaalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Kilimo akitoa maelezo kwa  Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa kuhusu Teknolojia ya Ufugaji wa Samaki kupitia Vizimba.
Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizaba akizungumza na wananchi  katika Kilele  cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa mwaka 2018 Simiyu ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Mkulima kutoka Wilaya ya Maswa akipokea zawadi yake ya fedha taslimu katika Kilele  cha Maonesho ya Nane nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi,  kwa kuwa mkulima bora kutoka Wilayani Maswa.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akikagua Banda la Jeshi la Magereza wakati alipotembelea baadhi ya mabanda katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akikagua Banda la Jeshi la Magereza wakati alipotembelea baadhi ya mabanda katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa. Elisante Ole Gabriel akitoa maelezo kwa Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa, alipotembelea mabanda ya wizara hiyo, katika Kilele  cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akisalimiana na Mbunge wa Bariadi, Mhe Andrew Chenge baada ya kuwasili Bariadi katika Uwanja wa Nyakabindi kuhitimisha Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2018.

Kutoka kushoto, Waziri wa Kilimo,Mhe.Dkt. Tizeba, Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiungan na viongozi na wananchi kuimba wimbo wa TAIFA, katika Kilele  cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Mtaalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Kilimo akitoa maelezo kwa  Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa kuhusu Teknolojia ya Ufugaji wa Samaki kupitia Vizimba, katika Kilele  cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Kanali Hassan Mabena(kushoto) akipokea kikombe cha JKT kuwa mshindi wa jumla kutoka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa, kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Meja Jenerali, Martin Busungu, katika Kilele  cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Vijana wa JKT Lwamkoma mkoani Mara wakifurahi Ushindi wa Jeshi hilo kupata kombe la mshindi wa kwanza wa jumla, katika Kilele  cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Serikali ya Msumbiji, mara baada ya kuhitimisha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa mwaka 2018 Simiyu, katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.

 Meneja wa TANESCO  Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Rehema Mashinji akipokea cheti ikiwa ni miongozi mwa mashirika yaliyofanya vizuri katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa mwaka 2018 Simiyu, katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.
Waziri wa kilimo, Mhe.Dkt. Charles Tizeba akitoa maelezo juu ya masuala ya ufugaji wa ng’ombe kisasa  kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa(wa pili kushoto) katika Kilele cha Nanenane 
Kutoka kushoto, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally., Waziri wa Kilimo,Mhe.Dkt. Tizeba, Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamin William Mkapa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack wakiungana na viongozi na wananchi kuimba wimbo wa TAIFA, katika Kilele  cha Maonesho ya Nane Nane Kitaifa ,katika uwanja wa Nyakabindi, Halmashauri ya Mji  wa Bariadi.


0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!