Friday, July 5, 2019

MADAM RITA, HOYCE TEMU, SAIDA KESSY KUAMUA MISS SIMIYU 2019


Rita Paulsen, Hoyce Temu (Miss Tanzania 1999) na Saida Kessy (Miss Tanzania 1997) wanatarajiwa kuwa majaji wa Shindano la kumsaka Miss Simiyu 2019, litakalofanyika kesho Julai 06, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
.
Hayo yamesemwa Julai 04, 2019 na Mkurugenzi wa Simiyu Talent Compay Ltd, Bi. Zena Mchujuko ambalo linaandaa shindano hilo kwa kushirikiana na Grace Entertainment, wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Bariadi

Amesema kama waandaaji wameamua kuwaleta majaji  hao ambao ni mahiri na wenye uzoefu katika masuala ya ulimbwende ili kupata Miss Simiyu ambaye atakuwa na uwezo kuuwakilisha mkoa katika Shindano la Miss Tanzania.

“Tumeamua kuwaleta majaji hawa kwa sababu ya uzito wa tukio lenyewe, uzoefu na umahiri wao, lengo letu ni kutoa Miss Simiyu atakayeweza kutuwakilisha katika Miss Tanzania  na tuna uhakika kila mshiriki atapata haki yake” alisema Mchujuko.

Aidha, Mchujuko amesema Mgeni Rasmi katika Shindano la Miss Simiyu 2019 atakuwa ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kwa upande wa Burudani Mwanamuziki wa Kizazi kipya Nasib Abdul alimaarufu Diamond Platinum atatumbuiza shindano hilo.

Kwa upande wake mwalimu  wa washiriki wa Miss Simiyu 2019  Doreen Robert Pastory  alibainisha kuwa majaji hao wanastahili kuwajaji warembo hao  huku akiongeza kuwa suala la urembo linatakiwa kuchukuliwa kama ajira nyingine badala ya kuchukulia kama jambo la kihuni ambapo alitoa rai kwa Mikoa mingine kuiga jambo hilo kwani ni ajira kama zilivyo ajira nyingine.

Naye mmoja wa washiriki Rebeka Manoti amesema wamefundishwa kwa kuzingatia maadili mema, hivyo wana matarajio makubwa ya kupata mlimbwende atakayepeperusha vyema tasnia hiyo ya urembo kimkoa ,kitaifa na kidunia.

Jumla ya warembo 15 watachuana katika shindano hilo na kiingilio itakuwa Shilingi 10,000 (Regular),Shilingi 50,000(Corparate) na Shilingi 100,000(VIP), na Mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Shilingi Milioni moja na washiriki wengine pia watapatiwa zawadi.
MWISHO
Mkurugenzi wa Simiyu Talent Compay Ltd, Bi. Zena Mchujuko ambayo inaandaa shindano hilo kwa kushirikiana na Grace Entertainment, akizungumza na waandishi wa habari Julai 04, 2019 Mjini Bariadi.


Washiriki wa Shindano la Miss Simiyu 2019 linalotarajiwa kufanyika kesho Julai 06, 2019 Mjini Bariadi.

Mwalimu  wa warembo wanaoshiriki Shindano la Miss Simiyu 2019, Bi. Doreen Robert Pastory akizungumza na waandishi wa habari Julai 04, 2019 Mjini Bariadi kuhusu shindano la Miss Simiyu litakalofanyika kesho Julai 06, 2019 Mjini Bariadi.



0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!