Thursday, July 4, 2019

RC MTAKA ATAKA MADIWANI ITILIMA WALIPWE MADENI KABLA YA MUDA WAO KUMALIZIKA


Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Itilima kuhakikisha inawalipa madiwani wake malimbikizo ya madeni kupitia fedha za makusanyo ya pamba mwaka huu ili kuondoa usumbufu ambao unaweza kujitokeza pindi watakapokuwa wamemaliza muda wao. 

Mtaka ameyasema hayo Julai 02, 2019 wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza maalumu la madiwani llililokuwa na agenda moja ya  kujadili hoja 39 za ukaguzi zilizoibuliwa na mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali ( CAG).

 “ni vyema madeni ya waheshimiwa madiwani yakalipwa  kwa wakati  ni ngumu kujadili vitu vya kimaendeleo wakati wao wanadai,  huwezi kushugulikia ya wengine wakati yako hayako vizuri,  ikumbukwe  wamebakiza muda mfupi baraza livunjwe  …si vyema wakatoka madarakani huku wakiwa wanadai”alisema Mtaka na kuongeza kuwa .

“Mkurugenzi hakikisha kipaumbele kwenye makusanyo ya pamba unalipa  madeni ya waheshimiwa hawa (madiwani) hakikisha unahuisha bima zao, lakini kingine hakikisha unatenga fedha kwa ajili ya uchaguzi ” aliongeza.

Awali akisoma taarifa ya ripoti ya mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG ) mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Elizabeth Gumbo alisema kwa mwaka wa fedha 2018/19 hoja zilizoibuliwa ni 39 na kuongeza kuwa hoja 24 kati ya 39 zilizoibuliwa zilitolewa mapendekezo na kuwasilishwa kwa mkaguzi na mthibiti mkuu wa hesabu za serikali kwa ajili ya uhakiki.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mhe. Daudi Nyalamu  amesema madiwani wanadai zaidi ya shilingi milioni 360  huku akiongeza tayari halmashauri imaishajipanga kulipa madeni yote kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo.

Nao baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa kata ya Lugulu Robert Jongela   na gertuda ngokolo diwani wa viti maalum kutoka kata ya ikindilo wamesema madeni yao ni ya muda mrefu tangu mwaka 2016 hadi 2019 hivyo kupitia kauli ya mkuu wa mkoa huo  imewapa   faraja na hatua hiyo imetoa tumain jipya la kupata stahiki zao,
            MWISHO  
         Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Madiwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakati wa Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019


         

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Mhe. Daudi Nyalamu akifungua Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo akiwasilisha taarifa katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019                 


Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza kabla ya kumkaribish Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani  Halamshauri ya Wilaya ya Itilima chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019.

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, MHE. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, MHE. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019
Baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, MHE. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika Kikao maalum cha Baraza la Madiwani chenye lengo la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2017/2018 Julai 2, 2019

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!