Wednesday, July 17, 2019

SERIKALI YATOA SHILINGI BILIONI 2.2 KUJENGA JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA SIMIYU


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya kujenga jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma za kulaza wanawake na watoto.

Waziri Ummy ameyasema hayo Julai 16, 2019 wakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la maabara, jengo la upasuaji ambalo pia litakuwa na huduma za mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.

Amesema wagonjwa wengi ni wanawake na watoto wadogo hivyo ni vema wakajengewa wodi  huku akibainisha pia kuwa Serikali imeshatoa shilingi bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la maabara na jengo la upasuaji ambalo pia litakuwa na huduma za mionzi unaotarajia kukamilika mwezi Oktoba 2019.

“Tulianza na ujenzi wa jengo la OPD, na awamu ya pili namshukuru Mhe. Rais ametoa shilingi bilioni 5.7 kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu kwa ajili ya ujenzi wa jengo la maabara, jengo la upasuaji ambalo pia litakuwa na huduma za mionzi”

“Sasa hivi tuna shilingi bilioni 2.2 kwenye akaunti ya Hospitali na tutaanza kujenga jengo la mama na mtoto, ili tuanze kulaza wagonjwa maana hata ukiangalia wagonjwa wengi  ni wanawake na watoto wadogo, hili la wodi za watu wengine nalo pia tunalibeba” alisema Waziri Ummy.

Aidha, Mhe. Waziri amepongeza wakala wa Majengo TBA mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza miradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa huku akimtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kurejesha fedha zilizokatwa kodi(withholding tax) wakati akilipa TBA gharama za ujenzi, ili zifanye kazi ya ujenzi maana TBA kama Taasisi ya Umma haipaswi kukatwa fedha hizo.

Naye Meneja wa TBA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Likimaitare Naunga amesema ikiwa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 204 zilizokatwa kama kodi “Withholding Tax” zikirejeshwa zitasaidia kununua vifaa vya kukamilishia majengo hayo.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, ambayo yataendelea kuboresha huduma kwa wananchi, ambapo pia ameishukuru wizara ya afya kwa kuendelea kusimamia kwa karibu ujenzi wa majengo hayo.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo amesema CCM kama wasimamizi wa utekelezaji wa Ilani wanashukuru kwa namna Serikali inavyotekeleza ilani katika kuboresha huduma za afya Mkoani Simiyu na ameahidi kuwa wataendela kufuatilia  na kusimamia  kwa karibu ili kuhakikisha huduma bora zinatolewa.
MWISHO
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Meneja wa Wakala wa Majengo nchini TBA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi. Likimaitare Naunga (katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) kuhusu Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu wakati wa  ziara ya Waziri huyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakioneshwa ramani ya jengo la Upasuaji wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.


 Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya(kushoto) ) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia mbele) kuhusu Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu wakati wa  ziara ya Waziri huyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.

Sehemu ya mbele ya Jengo la Upasuajia ambalo sehemu itatumika kama Jengo la Mionzi ambalo linaendelea kujengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Sehemu ya mbele ya Jengo la Maabara ambalo linaendelea kujengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wakiangalia kitu kwa makini katika Jengo la Upasuajia ambalo sehemu itatumika kama Jengo la Mionzi ambalo linaendelea kujengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya(wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia mbele) kuhusu Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu wakati wa  ziara ya Waziri huyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakikagua jengo la Upasuaji wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakielekea kukagua jengo la Upasuaji wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) kuhusu Ujenzi wa jengo la upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu wakati wa  ziara ya Waziri huyo yenye lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakioneshwa ramani ya jengo la Upasuaji wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Majengo ya Maabara, upasuaji na mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, Julai 16, 2019 Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!