Tuesday, July 2, 2019

RC MTAKA ATOA WITO KWA WADHAMINI WA SIMIYU JAMBO FESTIVAL KUENDELEZA TAMASHA HILO


Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa Mkurugenzi wa Jambo Food Produsts Company, Mhe. Salum Khamis na wadhamini wengine waliojitokeza kudhamini Tamasha la Simiyu Jambo Festival kuliendeleza tamasha hilo kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa mkoa wa Simiyu kuendeleza vipaji vyao katika sanaa, utamaduni na michezo.

Mtaka ameyasema hayo wakati akifunga Tamasha hilo Juni 30, 2019  Mjini Bariadi ambalo lilihusisha mashindano ya ngoma za asili (Mbina Wagika na Wagalu), mashindano ya baiskeli kwa wanawake na wanaume, mashindano ya mdahalo kwa wanafunzi wa shule za sekondari na mbio fupi(fun run).

“ Namshukuru sana Mkurugenzi wa Jambo Food Products Company Salum Khamis ambaye amekuwa mdhamini kwa miaka mitatu mfululizo kwenye tamasha  hili, nimuombe yeye na kampuni yake waendelee kuunga mkono juhudi hizi kwenye eneo la michezo na burudani, sisi ni viongozi leo tupo kesho hatupo, ni vizuri jambo hili ambalo tumelianzisha kampuni yake iendelee kulimiliki kama makampuni mengine ya vinywaji yanavyofanya” alisema ikaliendeleza.

Akizungumzia Kauli Mbiu ya Simiyu Jambo Festival: WEZESHA MTOTO WA KIKE ATIMIZE NDOTO ZAKE, INAWEZEKANA KUZUIA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO; Mtaka amesema ni vema watoto wa kike walindwe ili waweze kuepuka mimba za utotoni na kufikia ndoto zao.

Akizungumza na wananchi wakati wa Tamasha la Simiyu Festival Mdhamini Mkuu wa Tamasha hilo Mkurugenzi wa Jambo Food Products Company Salum Khamis amesema Kampuni yake itaendelea kudhamni tukio hilo na kuahidi kuendeleza tamasha hilo.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) mkoani Simiyu, Dkt. Amir Batenga  amesema moja ya ahadi za shirika hilo ni kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao hivyo kupitia  kauli mbiu ya tamasha hilo shirika hilo lilifikisha ujumbe kwa vijana na wanaamini kila kijana anaweza kutimiza ndoto zake.


Katika tamasha hilo washiriki zaidi ya 150 walishiriki mbio za baiskeli na mshindi wa kwanza  kilometa 150 wanaume alijinyakulia kitita cha shilingi 1,000,000/=, kilometa 80 wanawake shilingi 700,000 na walemavu kilometa tano shilingi 500,000/=, huku ngoma za asili Wagika na Wagalu kila kikundi kilijipatia shilingi 1,000,000/=

Simiyu Jambo Festival mwaka 2019 imedhaminiwa na Jambo Food Products Company, Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani-UNFPA, NGM Gold Mine Limited, NGS Petroleum, Alliance Ginneries Limited, Busega Mazao Limited, Maswa Standard Chalk, Ms Hotel,  Vetreces Company Limited na NHIF.
MWISHO

Baadhi ya washiriki wa mashindano ya baiskeli wakianza mashindano hayo katika Eneo la Salunda Mjini Bariadi wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Juni 30, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye namba 0413) akiwaongoza baadhi ya viongozi na wananchi katika mbio fupi za kilometa tano wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival liliofanyika Juni 30, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Jambo Food Products Company, Salum Khamis akimkabidhi zawadi ya shilingi milioni moja kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya mbio za baiskeli kilometa 150 wanaume katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto )na viongozi wengine wakifurahia jambo katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Msanii wa Kundi la BASEKI Mjini Bariadi akionesha umahiri wake wa kucheza na nyoka aina ya chat,  katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Washindi wa tatu wa mashindano ya baiskeli kilometa 150 wanaume wakisubiri kupokea zawadi zao, wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye fulana iliyoandikwa Jambo kifuani ) akicheza pamoja na viongozi na wananchi wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye fulana iliyoandikwa Jambo kifuani ) akicheza pamoja na viongozi na wananchi wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi cheti  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kwa naiba ya wadhamni wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival wanaotoka Bariadi katika tamasha hilo lililofanyika Juni 30, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Kampuni ya NGM Gold Mine Ltd,  Bw. Gungu Silanga kama ishara ya shukrani kwa kukubali kudhamini Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi chetI cha shukrani  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) mkoani Simiyu, Dkt. Amir Batenga  kwa niaba ya shirika hilo kwa kukubali kudhamini Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye kipaza sauti) na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mbio za baiskeli kwa watu wenye ulemavu, katika Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) mkoani Simiyu, Dkt. Amir Batenga  akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi ambapo Shirika hilo lilikuwa moja ya wadhamini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akimkabidhi chetI cha shukrani  Mwakilishi wa Shirika la Friedkin  Conservation Fund Ltd kwa niaba ya shirika hilo kwa kukubali kudhamini Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwa wameshika baadhi ya baiskeli zilizotolewa na Wheelchair Foundation wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye namba 0413 ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mkoani hapa na washiriki wa mashindano yam bio za baiskeli walemavu kilometa tano, wakati wa Tamasha la Simiyu Jambo Festival lililofanyika Juni 30, 2019 Mjini Bariadi.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!