Friday, July 19, 2019

SERIKALI YAKUBALIANA NA WANUNUZI KUNUNUA PAMBA SHILINGI 1200, YAKUBALI KULIPA FIDIA BEI IKISHUKA SOKO LA DUNIA

Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba amesema Serikali imekaa na wanunuzi wa pamba na kwa pamoja wamekubali kuanza rasmi kununua pamba kwa bei elekezi ya shilingi 1200 na ikiwa kutakuwa na hasara watakayopata kutokana na bei ya zao hilo kushuka katika soko la dunia (baada ya Agosti 15,  2019 ) Serikali itafidia.

Mhe. Mgumba ameyasema hayo katika nyakati tofauti wakati akiwa kwenye ziara yake ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba katika Wilaya ya Bariadi na Maswa Mkoani Simiyu.

Amesema awali wanunuzi wengi walisita kununua pamba kwa bei kubwa na kuuza kwa bei ndogo  kutokana na kushuka kwa bei ya pamba katika soko la dunia, lakini Serikali kwa kuwathamini wakulima, imesema pamba itanunuliwa kwa shilingi 1200 na ikiwa kuna hasara zozote za kibiashara watakazopata wanunuzi baada ya tarehe 15/08/2019 serikali itafidia.

“Tumekubaliana na wanunuzi kuwa waingie rasmi sokoni wanunue kwa bei elekezi ya shilingi 1200 kama kuna kushuka bei au  kutakuwa na hasara yoyote  hayo Serikali itabeba lakini wao waendelee kununua pamba kupitia vyama vya ushirika, msikubali kuuza pamba yenu chini ya bei ya shilingi 1200” alisema Mhe. Mgumba.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mhe. Festo Kiswaga amesema tayari wanunuzi wawili ambao ni NSAGALI na NGS Company wamepeleka fedha katika Vyama vya ushirika vya Msingi wilayani Bariadi na wanunuzi wengine wanaendelea kwenda kununua.

Nao wakulima waliotembelewa na Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo wameiomba Serikali kutoa mbegu, dawa na viuatilifu kwa wakati ili waweze kuongeza tija katika uzalishaji jambo ambalo Mhe. Mgumba alilitolea ufafanuzi kuwa linaendelea kushughulikiwa kwa kusajili wakulima ili kujua idadi kamili ya wakulima na kutoa pembejeo za kutosha kulingana na idadi ya wakulima.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa kilimo, Mhe. Omary Mgumba ametoa pole kwa wakulima wa Kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa kwa naiba ya Serikali kutokana na tatizo walilopata la kuunguliwa na pamba yao katika ghala ya Chama cha Ushirika cha msingi na kuelezwa kusikitishwa sana na tukio hilo.

Akitoa salamu hizo za pole kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema Serikali imesikitishwa sana janga hilo na iko pamoja nao, huku akitoa wito kwa wanachama wa Chama cha Ushirika cha Msingi  kuchukua tahadhali ya moto katika maeneo waliyokusanya pamba.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe ametoa wito kwa wanachama wa vyama vya ushirika kuchagua viongozi waadilifu.

MWISHO

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa mkoani Simiyu, alipofika kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wakulima wa pamba mara baada ya kufika katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Nyaumata Mjini Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.
Baadhi ya wakulima wa pamba wakipeleka pamba yao katika Chama cha Ushirika cha Msingi cha Nyaumata Mjini Bariadi.



Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(wa tatu kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba(wa nne kushoto) azungumze na wakulima wa pamba wa Kijiji cha Mbiti wilayani Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(wa tatu kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba(wa nne kushoto) azungumze na wakulima wa pamba wa Kijiji cha Mbiti wilayani Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa mkoani Simiyu, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (hayupo pichani) alipofika kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wakulima wa pamba wa Kijiji cha Mbiti wilayani Bariadi, wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa ununuzi wa zao la pamba.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa mkoani Simiyu, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (hayupo pichani) alipofika kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani humo, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.
Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa mkoani Simiyu, akiwasilisha hoja yake kwa  Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (hayupo pichani) alipofika kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika  ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba kijijini hapo kuwapa pole kwa niaba ya Serikali, wakulima wa pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika ghala la  Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Shinyanga Mwenge wilayani Maswa mkoani Simiyu, alipofika kijijini hapo kuwapa pole wakulima wa pamba kutokana na pamba yao iliyokuwa imekusanywa katika ghala la Chama cha Ushirika kuteketea kwa moto siku kadhaa zilizopita.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!