Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri
Mkoani Humo kuandaa mipango mikakati katika Halmashauri zao.
Sagini ameyasema hayo wakati
akifungua mafunzo ya siku tatu ya uandaaji wa Mipango mikakati ya Mamlaka za
Serikali za Mitaa Mkoani humo yanayofanyika Lamadi wilayani Busega, chini ya
Mpango wa Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa(PFMRP).
Amesema wakurugenzi
wote wahakikishe wanatumia rasilimali zilizopo katika maeneo yao kuhakikisha
kuwa wanakamilisha uandaaji wa mipango mikakati hiyo.
“ Niwaombe Wakurugenzi
Watendaji kuepuka visingizio vya kutokuwa na fedha kutekeleza jambo hili na
badala yake mjipange kwa kutumia rasilimali tulizonazo” amesema.
Aidha, amesema Mpango
Mkakati ni muhimu kwa kila Halmashari kwa kuwa unasaidia Halmashauri kufikia
malengo ya kuanzishwa kwake na kuboresha utoaji huduma za kiuchumi na kijamii kwa
wananchi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg.Abdallah
Malela amesema mafunzo hayo yatawasaidia
wao kama viongozi na watendaji wengine katika Halmashauri zao kutekeleza
shughuli mbalimbali za maendeleo zikiwemo za uanzishwaji na uendeshaji wa viwanda kimkakati.
Wakati huo huo pia
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea
kutenga maeneo ili kuwezesha utekelezaji wa Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
Mkoani humo.
Mafunzo ya uandaaji wa
Mipango mikakati ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) Mkoani
yamewahusisha Wakurugenzi, Wataalam wa Idara ya Kilimo, Fedha, Mipango na
Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri zote sita (06) za mkoa huo (Halmashauri
ya Wilaya ya Bariadi, Busega, Itilima, Maswa, Meatu na Halmashauri ya Mji
Bariadi).
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (wa pili kulia) akizungumza na
washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mipango mikakati ya Halmashauri mkoani humo
yaliyofanyika Lamadi wilayani Busega
0 comments:
Post a Comment