Saturday, May 6, 2017

VIONGOZI, WABUNGE WA MKOA WA SIMIYU WAKUTANA DODOMA KUJADILI UJENZI WA UCHUMI WA VIWANDA

Viongozi wa Mkoa wa Simiyu,  wamekutana na Wabunge wa Mkoa huo mjini Dodoma katika kikao maalum  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu.

Pamoja na kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau hao kuhusu Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu, kikao hicho pia kilikusudia kupata baraka za Wabunge wa Mkoa huo juu ya miradi ya uanzishwaji wa Viwanda katika Halmashauri zote sita.

Katika kikao hiki  wajumbe wamepata fursa ya kupitia maandiko ya miradi ya uanzishwaji wa viwanda yaliyowasilishwa na Wakurugenzi wa Halmashauri zote sita; viwanda ambavyo vitajengwa katika maeneo tofauti ya Mkoa wa Simiyu chini ya utekelezaji wa Kauli Mbiu ya "Wilaya Moja Bidhaa Moja".

Miradi iliyowasilishwa ni pamoja na upanuzi wa Kiwanda cha kutengeneza Chaki wilayani Maswa, Upanuzi wa kiwanda cha kusindika maziwa wilayani Meatu ambapo kiwanda hicho kitaongeza uzalishaji wa maziwa   yakiwemo maziwa ya unga.

Miradi mingine ni ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vifungashio wilayani Maswa,kiwanda cha kutengeneza sabuni za maji,miche na za unga wilayani Itilima, kiwanda cha kutengeneza Tomato sauce na Chill sauce Busega, kiwanda cha kusaga nafaka na kupaki unga katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi na kiwanda cha kuchakata ngozi na bidhaa za ngozi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.

Wabunge wa Mkoa wa Simiyu chini ya Uenyekiti wa Mbunge wa Bariadi,Mhe.Andrew Chenge kwa pamoja wamepongeza juhudi zinazofanywa na viongozi na watendaji mkoani humo na kuunga mkono miradi yote ya uanzishwaji wa Viwanda , ambapo hatua inayofuata sasa ni kufanyika kwa Upembuzi Yakinifu kwa miradi hiyo na kuanza utekelezaji.

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imedhamiria kuhakikisha azma ya Serikali ya awamu ya tano ya Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda inatekelezwa kwa vitendo.

Naye Katibu Tawala Mkoa,Ndg Jumanne Sagini amesema Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii ya (ESRF) wataanza kufanya upembuzi yakinifu wa mradi wa upanuzi wa kiwanda cha kutengeneza chaki na watakamilisha katika kipindi cha wiki wiki mbili, wakati upembuzi yakinifu kwa miradi mingine utafanywa na kukamilika katika kipindi cha  miezi miwili.

Kikao hiki kimehusisha baadhi ya wajumbe ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,Wabunge wa Mkoa huo, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa Halmashauri, Maafisa Mipango na Wanasheria wa Halmashauri zote za mkoa huo,wataalam wa masuala ya Viwanda pamoja na wadau wengine wa Uwekezaji kutoka NSSF.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Anthony Mtaka akizungumza na viongozi na Wabunge wa mkoa huo kikao maalum  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Simiyu ambaye ni Mbunge wa Bariadi Mhe.Andrew Chenge akizungumza na viongozi na Wabunge wa mkoa huo kikao maalum  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Anthony Mtaka (aliyesimama)akizungumza na viongozi na Wabunge wa mkoa huo kikao maalum  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu, kilichofanyika leo Mjini Dodoma.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu (aliyesimama) Ndg.Jumanne Sagini  akifafanua jambo mbele ya  viongozi na Wabunge wa mkoa huo katika kikao maalum  cha  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Dodoma
Baadhi ya viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kikao maalum  cha  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika Mjini Dodoma
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Bariadi,Ndg.Melkizedek Humbe akiwasilisha andiko la Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Kusaga nafaka na kufungasha unga kwa viongozi na Wabunge wa mkoa wa Simiyu, katika kikao maalum  cha  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima , Ndg.Mariano Mwanyigu akiwasilisha andiko la mradi wa uanzishwaji wa Kiwanda cha kutengeneza sabuni  kwa viongozi na Wabunge wa mkoa wa Simiyu  katika kikao maalum  cha  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya yaBusega , Ndg.Anderson Njiginya akiwasilisha andiko la mradi wa uanzishwaji wa Kiwanda cha kutengeneza Tomato sauce na Chili sauce   kwa viongozi na Wabunge wa mkoa wa Simiyu  katika kikao maalum  cha  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika Mjini Dodoma
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa , Dkt.Fredrick Sagamiko  akiwasilisha andiko la mradi wa upanuzi wa Kiwanda cha kutengeneza chaki na kiwanda cha kutengeneza vifungashio    kwa viongozi na Wabunge wa mkoa wa Simiyu  katika kikao maalum  cha  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Busega, Mhe.Dkt.Raphael Chegeni akichangia jambo katika kikao maalum  cha kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu , Ndg.Fabian Manoza  akiwasilisha andiko la mradi wa upanuzi wa Kiwanda cha kusindika maziwa kwa viongozi na Wabunge wa mkoa wa Simiyu  katika kikao maalum  cha  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika Mjini Dodoma.
Kaimu Meneja wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Hifandi ya Jamii wa NSSF, Bi.Radhia Tambwe akichangia jambo katika kikao maalum cha  kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika Mjini Dodoma, (kushoto) Mtalaam wa Viwanda, Ndg.Ndaki Munyeti.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi , Mhe.Mashmba Ndaki  akichangia jambo katika kikao maalum  cha kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe.Njalu Silanga  akichangia jambo katika kikao maalum  cha kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM)Mkoa wa Simiyu, Mhe.Esther Midimu  akichangia jambo katika kikao maalum  cha kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM)Mkoa wa Simiyu, Mhe.Leah Komanya  akichangia jambo katika kikao maalum  cha kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki , Mhe.Stanslaus Nyongo  akichangia jambo katika kikao maalum  cha kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Kisesa na Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mhe.Luhaga Mpina  akichangia jambo katika kikao maalum  cha kujadili na kupata uelewa wa pamoja juu ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Mkoani humo, kilichofanyika leo Mjini Dodoma.



0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!