Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini leo amesaini mikataba ya ujenzi wa miradi nane itakayojengwa
na Wakala wa Majengo (TBA) kupitia Kikosi chake cha Ujenzi (Building Brigade) katika makao Makuu ya Mkoa
Mjini Bariadi, Wilaya ya Busega na Itilima.
Mikataba iliyosainiwa
ni pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje la Hospitali ya Mkoa(OPD)
litakalojengwa kwa gharama ya shilingi
1,191,721,678.00, Nyumba ya Mkuu wa Mkoa (shilingi 273,390,082.99), Nyumba ya
Katibu Tawala Mkoa(shilingi 266,269,130.29), Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya
Itilima (shilingi 141,196,144.51) na Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Busega
(shilingi 238,061,242.06).
Mikataba mingine ni ya
mradi wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega litakalojengwa
kwa shilingi 1, 390,030,338.57,
ukamilishaji wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa kwa shilingi
128,247,283.79 pamoja na Ujenzi wa Nyumba 10 za Makatibu Tawala Wasaidizi wa
Sekretarieti ya Mkoa kwa gharama ya shilingi 841,540,642.50, ambapo kwa sasa
mradi huu utaanza na ujenzi wa nyumba tatu.
Akizungumza na wataalam
kutoka Wakala wa Majengo(TBA) na Makao Makuu na Mkoa wa Simiyu kabla ya kusaini
mikataba hiyo, Sagini amewataka wataalam hao kuhakikisha majengo yote
yanajengwa kwa ubora na kwa muda uliowekwa katika mikataba hiyo.
Meneja wa Kikosi cha
Ujenzi cha TBA, Humphrey Killo amesema kikosi hicho kitajenga majengo yote kwa
ubora unaotakiwa na ndani ya muda ulipoangwa kwa kuwa kushindwa kuzingatia muda
kutawaongezea gharama ambazo hazipo kwenye mikataba.
Aidha, Killo amesema
katika gharama za ujenzi wa majengo hayo watazingatia bajeti waliyokubaliana na
mteja wao ambaye ni Katibu Tawala Mkoa na kutakuwa na timu itakayofuatilia
matumizi ya fedha katika kila kazi itakayofanyika kwa kuwa wana viwango vya chini
ikilinganishwa na wakandarasi wengine.
Ukamilishaji wa ujenzi
wa miradi hii unatofautiana kulingana na mikataba iliyowekwa kuanzia leo tarehe
04/05/2017 ambapo Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje la Hospitali ya Mkoa(OPD)
litajengwa katika kipindi cha miezi sita(06), Nyumba ya Mkuu wa Mkoa miezi sita(06),
Nyumba ya Katibu Tawala Mkoa miezi sita(06), Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya
Itilima miezi minne(04), Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Busega miezi mitano (05), Jengo
la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega miezi sita(06) ,ukamilishaji wa Ujenzi wa
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa miezi miwili (02) na Nyumba 10 za Makatibu
Tawala Wasaidizi wa Sekretarieti ya Mkoa miezi sita (06).
Katibu Tawala Mkoa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akisaini moja ya mikataba ya ujenzi wa miradi nane
(08) ya Ujenzi inayotarajiwa kutekelezwa na Wakala wa Majengo (TBA) Mkoani
Simiyu.
|
Kaimu
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Miundombinu, Mhandisi.Deusdedit Mshuga
akichangia jambo wakati wa zoezi la kusaini mikataba ya ujenzi wa miradi nane
(08) ya Ujenzi inayotarajiwa kutekelezwa na Wakala wa Majengo (TBA) Mkoani
Simiyu.
0 comments:
Post a Comment