Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema iwapo Mpango wa Huduma ya Afya ngazi ya Jamii
utatumika vizuri utasaidia kuokoa Afya na maisha ya wananchi wengi Mkoani humo.
Mtaka ameyasema
hayo katika kikao kilicho wahusisha Viongozi ngazi ya Mkoa,Wilaya, watendaji wa
Kata, Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Itilima na Mji wa
Bariadi, ambacho kililenga kutoa elimu kuhusu utekelezaji wa mpango wa huduma
ya Afya ngazi ya Jamii mkoani humo.
Mtaka
amesema mwamko wa kupata huduma za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya
kwa wananchi katika maeneo mengi mkoani humo uko chini, hivyo mpango huu wa kutoa huduma
ngazi ya kaya utasaidia kuhamasisha wananchi kutafuta huduma za afya katika
vituo hivyo badala ya kutegemea tiba za kienyeji.
“Tukitumia
huduma hii ya Afya Majumbani vizuri itasaidia sana, tukifika mahali ambapo
jamii yetu itapata mwamko wa kupata matibabu katika vituo stahiki vya afya
tutakua tumeokoa jamii yetu, kwa sababu bado
wapo wanaoamini kupata matibabu katika tiba za kienyeji; tungehitaji wananchi
wetu huduma ya kwanza kwenye afya iwe vituo vyetu kutolea huduma za afya na
siyo tiba mbadala” amesema Mtaka.
“........kwa
sisi ambao tunatengeneza Mkoa wetu katika Uchumi, Uchumi ni Afya wananchi hawawezi
kufanya kazi wakajenga uchumi kama hawatakuwa na afya njema” alisisitiza.
Aidha,
Mtaka amewataka Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji kufanya utambulisho wa
kutosha wa wahudumu wa afya ya Msingi ngazi ya jamii watakaokuwa wakitoa huduma
kwa wananchi katika maeneo yao ili wataalam hao wasije wakapata madhara yoyote
wakati wakitekeleza majukumu yao.
Mkuu
huyo wa Mkoa pia amewataka wananchi kuachana na taratibu za kimila zinazoathiri
utendaji wa watumishi wa Umma ikiwemo kutumia mahakama za kimila (dagashida) na
akawataka viongozi hao kuwasaidia wananchi kubadilika ili wahudumu wa afya
ngazi ya Jamii watakaopelekwa katika maeneo yote ya mkoa huo watekeleze
majukumu yao bila vikwazo vyovyote.
Wakati
huo huo Mtaka ameomba Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF lisaidie katika
kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii walipewa mafunzo, ili wasaidie kutoa
huduma na kupunguza changamoto ya upungufu wa watoa huduma wakati Serikali
ikiendelea kushughulikia suala hilo.
Vile
vile ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa afya ikiwemo Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kushughulikia suala la upatikanaji wa vifaa
ili watoa huduma ngazi ya jamii watakapowafikia wananchi waweze kutoa huduma
stahiki kwa wakati.
Kwa upande wake Afisa wa Mpango wa Huduma ya
Afya ngazi ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt.Ama Kasangala amesema Wizara imetengeneza miongozo ya kuwafundisha
wahudumu hao wanapokuwa kazini ili waimarike na kutoa huduma nzuri.
Naye
Kaimu Mratibu wa Mpango wa Huduma ya Afya Ngazi ya Jamii, Dkt. Bahame Ntelemko
amesema mpango umelenga kuwatumia wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kusaidia
kuboresha huduma za afya hususani katika huduma za mama wajawazito na uzazi kwa
ujumla.
Dkt.
Ntelemko amesema kwa mwaka 2016 wanawake takribani 45 walipoteza maisha
kutokana na masuala ya uzazi ambapo vifo vingi vinatokana na ukosefu wa elimu
ikiwemo kutojua umuhimu wa kuwahi katika vituo vya kutolea huduma, ambapo
amesema uwepo wa huduma katika kaya utasaidia kupunguza idadi ya vifo hivyo.
Mafunzo
yanayofanywa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika lisilo la
Kiserikali la AMREF, kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii
ngazi ya Jamii Mkoa wa Simiyu, yameshawafikia Watendaji wa Kata, Mitaa na
Vijiji zaidi ya 350.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji katika kikao
cha kutoa elimu kwa viongozi hao kilichofanyika Mjini Bariadi kuhusu utekelezaji
Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii
ngazi ya Jamii Mkoani humo.
Dkt.Ama
Kasangala kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, akizungumza
na Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji katika kikao cha kutoa elimu kwa viongozi
hao kilichofanyika Mjini Bariadi kuhusu utekelezaji
Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii
ngazi ya Jamii Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) na Dkt.Ama Kasangala
kutoka Wizara ya
Afya wakiteta jambo katika kikao cha kutoa elimu kwa
viongozi hao kilichofanyika Mjini Bariadi kuhusu utekelezaji Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii ngazi ya Jamii
Mkoani humo.
Baadhi ya Watendaji
Kata, Mitaa na Vijiji kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika kikao cha kutoa elimu kwa
viongozi hao kilichofanyika Mjini Bariadi kuhusu utekelezaji Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii ngazi ya Jamii
Mkoani humo.
Baadhi ya Watendaji
Kata, Mitaa na Vijiji kutoka kwa Halmashauri ya Mji Bariadi wakimsikiliza Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika kikao cha kutoa elimu kwa viongozi
hao kilichofanyika Mjini Bariadi kuhusu utekelezaji Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii ngazi ya Jamii
Mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja
na Baadhi ya Watendaji Kata, Mitaa na
Vijiji kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe.Anthony Mtaka(wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi
wa Mkoa, Wizara ya Afya na Watendaji Kata, Mitaa na Vijiji kutoka kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima
Baadhi
ya Watendaji Kata, Mitaa na Vijiji kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika kikao cha kutoa elimu kwa
viongozi hao kilichofanyika Mjini Bariadi kuhusu utekelezaji Mpango wa Huduma za Afya ya Jamii ngazi ya Jamii
Mkoani humo
0 comments:
Post a Comment