Thursday, January 9, 2020

MWEKEZAJI KUTOKA INDIA AONESHA NIA KUWEKEZA KILIMO CHA MPUNGA, KIWANDA CHA KUCHAKATA MPUNGA SIMIYU


Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala ameonesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega mkoani Simiyu, ambapo anatarajia kuwekeza katika eneo lenye ukubwa wa ekari zipatazo 2000.



Akizungumza na viongozi na watendaji wa Mkoa wa Simiyu baada ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye fursa ya uwekezaji katika kilimo cha mpunga wilayani Busega, Bw. Agarwala amesema mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla ina rasilimali nyingi hivyo ikiwa Makampuni kutoka India yatafanya kazi kwa kushirikiana na Watanzania rasilimali hizo ziatakuwa na manufaa kwa Watanzania.

“Mkoa wa Simiyu na Tanzania kwa ujumla ina rasilimali za kutosha ambazo zipo kwa ajili ya kuwanufaisha Watanzania wenyewe hivyo  kinachohitajika ni teknolojia, uwekezaji, ushirikiano kutoka Serikalini kufanya haya yote yatokee; baada ya ziara hii ninaamini tukiyatekeleza kwa juhudi yale tuliyokubaliana mkoa huu utaendelea kwa kasi,” alisema Agarwala.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemhakikishia mwekezaji huyo upatikanaji wa eneo la ekari 2000 kwa ajili ya uwekezaji na kubainisha kuwa malengo ya mkoa ni kuhakikisha wilaya ya Busega inakuwa mzalishaji mkuu wa chakula katika mkoa kwa kuwa ndiyo wilaya yenye ziwa Victoria ndani ya Mkoa.

Aidha, pamoja na kutoa ushirikiano kwa mwekezaji kutimiza azma yake Mtaka amesema Serikali ya Mkoa imezungumza na Benki ya CRDB kuona uwezekano wa kuwawezesha wakulima wa mpunga wilayani Busega hususani walio kando ya ziwa Victoria kupitia dirisha la kilimo ili waweze kulima kisasa kupitia umwagiliaji.

Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Bw. Lusingi Sitta amesema Benki iko tayari kumuunga mkono mwekezaji na wakulima wa wilaya ya Busega  kupitia dirisha la kilimo kutokana na wilaya hiyo kuwa na maeneo mazuri na chanzo cha uhakika cha maji (Ziwa Victoria), ambapo alibainisha kuwa tayari benki hiyo ina uzoefu wa kuwezesha miradi mbalimbali ya kilimo cha umwagiliaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo amesema wao kama chama wanaunga mkono juhudi za watu wanaoitika huku akiongeza kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri kwenye kilimo hususani cha mpunga hivyo ujio wa mwekezaji huyo mkoani hapa utasaidia kuongeza tija kwenye zao hilo.

Katika hatua nyingine  baadhi ya wakulima wamesema kuwa ujio wa mwekezaji  huyo utawasaidia wao kuzalisha kwa tija ikilinganishwa na awali," tukianza kulima kilimo cha umwagiliaji tunaamini tutavuna mavuno mengi maana tutalima zaidi ya mara moja kwa msimu" alisema Monika Msabila

"Kuna kipindi mavuno yanashuka kama mvua zikiwa chache sasa ujio wa mwekezaji huyu tumeupokea maana atatusaidia na sisi kulima kilimo cha umwagiliaji na kuacha kutegemea mvua pekee " alisema Simon Ngelela mkazi wa Kijiji cha Shigala wilayani Busega.

Katika hatua nyingine mwekezajI alipata fursa ya kutembelea kiwanda kinachomilikiwa na Mwekezaji mzawa, Deogratius Kumalija ambacho kinaongeza thamani kwenye mazao ya chakula hususani mpunga na mahindi Busega Mazao Limited  kilichopo wilayani Busega.
MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akitoa maelezo kwa Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(wa tatu kulia)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega, wakati alipotembelea kuona moja ya maeneo yenye fursa ya uwekezaji huo jana Januari 08, 2020  wilayani Busega  
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Kabuko (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya eneo la Mwamanyili kwa Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(wa tatu kulia)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega, wakati alipotembelea kuona moja ya maeneo yenye fursa ya uwekezaji huo jana Januari 08, 2020  wilayani Busega  .  
 Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(wa tatu kulia)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega, akiangalia  mchele unaochakatwa  na kiwanda cha Busega Mazao wakati alipotembelea kuona moja ya maeneo yenye fursa ya uwekezaji huo jana Januari 08, 2019  wilayani Busega  .  

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akitoa maelezo kwa Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(wa tatu kulia)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega, wakati alipotembelea kuona moja ya maeneo yenye fursa ya uwekezaji huo jana Januari 08, 2020 wilayani Busega  

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(wa tatu kulia)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega, wakati alipotembelea kuona moja ya maeneo yenye fursa ya uwekezaji huo jana Januari 08, 2020  wilayani Busega  

 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu (kushoto) akisalimiana Mwekezaji kutoka nchini India, Bw. Vivek Aragwala mara baada ya kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza leo Januari 08, 2020 ambaye atafanya ziara ya siku moja mkoani Simiyu yenye lengo la kuangalia maeneo ya uwekezaji katika kilimo cha mpunga na ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mpunga, (kulia) ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Abdallah Kirungu aliyefuatana na mwekezaji huyo.

 Bi. Monica Msabila mkulima wa mpunga kutoka Kijiji cha Shigala wilayani Busega akitoa maelezo ya kilimo hicho kwa Mwekezaji kutoka nchini India, Bw. Vivek Aragwala ambaye anatarajia kuwekeza katika kilimo cha mpunga na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani humo, pamoja na viongozi wengine wa mkoa alioambatana nao katika ziara yake ya kuona maeneo yenye fursa ya uwekezaji huo jana Januari 08, 2020.  

 Baadhi ya viongozi na watendaji wa wilaya ya Busega na mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Mwekezaji kutoka nchini India, Bw. Vivek Aragwala ambaye anatarajia kuwekeza katika kilimo cha mpunga na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega (wa nane kulia)  mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye fursa za uwekezaji huo jana Januari 08, 2020 .

 Bw. Simon Ngeleja mkulima wa mpunga kutoka Kijiji cha Shigala wilayani Busega akitoa maelezo ya kilimo hicho kwa Mwekezaji kutoka nchini India, Bw. Vivek Aragwala (kushoto) ambaye anatarajia kuwekeza katika kilimo cha mpunga na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani humo, pamoja na viongozi wengine wa mkoa alioambatana nao katika ziara yake ya kuona maeneo yenye fursa ya uwekezaji huo jana Januari 08, 2020.
 Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(kushoto)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega, akiangalia  unga wa sembe moja ya bidhaa  inayozalishwa  na kiwanda cha Busega Mazao wakati alipotembelea kuona moja ya maeneo yenye fursa ya uwekezaji anaotaka kufanya,  jana Januari 08, 2020  wilayani Busega.
 Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(katikati)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Abdallah Kirungu aliyefuatana na mwekezaji huyo baada ya kutembelea na kuona moja ya maeneo yenye fursa ya uwekezaji anaotaka kufanya,  jana Januari 08, 2020  wilayani Busega.

 Sehemu ya kiwanda cha kuchakata nafaka cha Busega Mazao Limited kilichopo wilayani Busega Mkoani Simiyu.
 Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(katikati)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia), Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta(kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo baada ya kutembelea na kuona moja ya maeneo yenye fursa ya uwekezaji,  jana Januari 08, 2020  wilayani Busega.
Sehemu ya eneo la Mwamanyili wilayani Busega linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ambalo lilitembelewa na Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(katikati)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega Januari 08, 2020.
 Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(wa tatu kulia)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega akizungumza na baadhi ya viongozi na watendaji mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuona moja ya maeneo yenye fursa ya uwekezaji anaotaka kufanya,  jana Januari 08, 2020  wilayani Busega.
 Mwekezaji kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala(kushoto)  ambaye anatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga kupitia umwagiliaji na kujenga kiwanda cha kuchakata mpunga wilayani Busega akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia), baada ya kutembelea na kuona maeneo yenye fursa ya uwekezaji,  jana Januari 08, 2020  wilayani Busega.
Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!